by Admin | 6 May 2021 08:46 pm05
Shalom! karibu tujifunze biblia, Neno la Mungu wetu, taa iongozayo miguu yetu na Mwanga wa njia yetu, iendayo mbinguni.
Katika biblia tunaona yapo maagizo mengi ambayo Mungu wetu ametupatia Moja kwa moja, Kwamfano agizo la Upendo!. Hili ni agizo ya kwamba ni lazima tupendane!
1Yohana 3:10 “Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
11 Maana, hii ndiyo habari mliyoisikia tangu mwanzo, KWAMBA TUPENDANE SISI KWA SISI”
Maana yake tusipokuwa na upendo! Hata tufanye nini hatuwezi kuiona mbingu, haijalishi tutanena kwa lugha kiasi gani, haijalishi tutatoa unabii, na kufanya miujiza mikubwa kiasi gani…
1Wakorintho 13: 1 “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
2 TENA NIJAPOKUWA NA UNABII, NA KUJUA SIRI ZOTE NA MAARIFA YOTE, NIJAPOKUWA NA IMANI TIMILIFU KIASI CHA KUWEZA KUHAMISHA MILIMA, KAMA SINA UPENDO, SI KITU MIMI.
3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu”.
Hayo ni maagizo ya moja kwa moja ambayo tumepewa. Lakini pia yapo maagizo ambayo hatujapewa moja kwa moja, lakini tusipoyafanya tutahukumiwa kwayo.
Leo tutajifunza Agizo moja la msingi, ambalo hatujaagizwa, lakini ni wajibu wetu kulitenda….(Tafadhali naomba usome kwa makini huku ufahamu wako ukiupeleka katika kupata kitu kipya na si kutafuta kasoro, akili yako ukiipeleka katika kutafuta kasoro, shetani atakusaidia kuipata, lakini ukiipeleka katika kujifunza basi utapata kitu kipya).
Sasa agizo hilo si linguine zaidi ya “UTOAJI”.
Suala la utoaji limekuwa lango la watu wengi kuingia katika wokovu na kutokea. Wapo ambao wakisikia kuhusu utoaji wanalipokea Neno hilo kwa furaha na kuwasogeza zaidi kwa Mungu na wapo ambao wakilisikia, ndio linawatoa zaidi kwa Mungu..Na ndio linakuwa tiketi/sababu ya kuuacha wokovu kabisa kabisa, kwasababu ndani ya fahamu zao shetani kashawapandikizia mbegu ya kwamba wanataka kunyonywa vya kwao. Hivyo shetani analichukua wazo hilo na kuwahubiria waiache njia ya wokovu au waidharau. Lakini leo nataka tupate akili mpya kuhusu Utoaji, ili itusaidie tusije tukakosa kuingia katika ufalme wa mbinguni.
Kabla ya kuendelea mbele hebu tusome mistari michache, tuilinganishe na mingine kisha tutapata kuelewa kiini cha somo letu la leo. (Katika mistari hiyo zingatia vipengele vilivyoanishwa kwa herufi kubwa)
Mathayo 10:7 “Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.
8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; MMEPATA BURE, TOENI BURE.
9 Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu;
10 wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; MAANA MTENDA KAZI ASTAHILI POSHO LAKE.
11 Na mji wo wote au kijiji cho chote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu mwaminifu; mkae kwake hata mtakapotoka.
12 Nanyi mkiingia katika nyumba isalimuni.
13 Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikilie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi. 14 NA MTU ASIPOWAKARIBISHA wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung’uteni mavumbi ya miguuni mwenu.
15 Amin, NAWAAMBIA, ITAKUWA RAHISI NCHI YA SODOMA NA GOMORA KUSTAHIMILI ADHABU YA SIKU YA HUKUMU, KULIKO MJI ULE”.
Maagizo hayo ni Bwana Yesu aliwapa wanafunzi wake, wakati anawatuma kwenda kuhubiri, akawaambia wanapotoka wasibebe chochote, (fedha au chakula) kwasababu huko wanakokwenda, Mungu atawafungulia mlango wa kuvipata hivyo, maana yake wapo watu watakaoguswa moyo na kuwakaribisha na kuwapa mahitaji yao,kama chakula, fedha, nguo n.k kwasababu sio wote watakuwa na moyo mgumu wa kutoa. Lakini Mwisho wa maagizo hayo anawaambia.. “mtu yeyote asiyewakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung’uteni mavumbi ya miguuni mwenu”. Halafu anamalizia kwa kusema… “Amin, NAWAAMBIA, ITAKUWA RAHISI NCHI YA SODOMA NA GOMORA KUSTAHIMILI ADHABU YA SIKU YA HUKUMU, KULIKO MJI ULE”.
Maana yake ni kwamba kitendo cha wale watu kutowakaribisha (maana yake wasipowafadhili) wala kusikia maneno yao, watapata adhabu kubwa kuliko watu wa Sodoma.
Sasa hebu twende pamoja tena katika Mathayo 25
Mathayo 25:31 “ Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;
32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;
33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto….
41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, ONDOKENI KWANGU, MLIOLAANIWA, MWENDE KATIKA MOTO WA MILELE, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
42 KWA MAANA NALIKUWA NA NJAA, MSINIPE CHAKULA; NALIKUWA NA KIU, MSININYWESHE;
43 NALIKUWA MGENI, MSINIKARIBISHE; NALIKUWA UCHI, MSINIVIKE; NALIKUWA MGONJWA, NA KIFUNGONI, MSIJE KUNITAZAMA.
44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?
45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele”.
Umeona hapo?. Bwana alipowatuma wakina Petro bila kubeba chakula cha safari, lengo lake ni wale wapate riziki kupitia wale watakaowahubiria, ndio maana akamalizia pale juu kwa kusema “MAANA MTENDA KAZI ASTAHILI POSHO LAKE.” Wakina Petro ni watenda kazi, (yaani wanafanya kazi ya kuhubiri), hivyo wanastahili posho zao, yaani riziki zao huko wanakokwenda kuhubiri, ndio maana akawaambia hata wasihangaike kutoka na akiba ya chakula, wala mavazi, kwasababu watavipata huko wanakokwenda.
Lakini chaajabu ni kwamba Bwana Yesu, hajatoa sheria wala hajatoa Agizo kwa wale watakaohubiriwa kwamba ni lazima watoe!!.. Kwamba ni lazima au ni amri kuwafadhili wakina Petro na Mitume wanapohubiri,.. Angeweza kuwaambia wakina Petro kwamba wawaambie watu wanaowahubiria kwamba “Kila mkutano wanaofanya wachangie, au kila mtaa wanaofika, Bwana kasema wapewe chochote”.. Lakini Bwana aliwaambia wasiseme lolote..wao kazi yao ni kutoa bure!, wasipopewa chochote wasonge mbele, wala wasionyeshe kama ni wahitaji!, wala wasiombe ombe!… Lakini mwisho tunaona Bwana anatangaza hukumu kwa wale wote ambao hawakuwakaribisha watumishi hao wa Mungu. Kwamba atawabagua kama mbuzi!
Ni nini tunajifunza hapo?
Yapo maagizo ambayo hayajaagizwa. Unaweza leo ukakwepa kumtolea Mungu, ni kweli hajakulazimisha, wala hajakuwekea kiasi, wala hajakuagiza kwamba ni lazima umtolee, amekaa kimya kuhusu hilo eneo, lakini huna budi kufahamu na kuwa na hekima kwamba ni wajibu wako kumtolea Mungu. Kama huamini kuwa kitendo cha kutomtolea Mungu ni dhambi soma tena hiyo Mathayo 25:31-43. Jiulize ni kwanini Bwana hajawafananisha wale mbuzi na watu wanaomkufuru, au wanaomtukana, au manabii wa uongo, lakini badala yake kawafananisha na watu ambao walikuwa hawamjali kimatoleo.
Ndio siku hiyo utasema.. “Bwana hukusema watumishi wako watoe bure?”… ni kweli alisema hivyo “lakini na wewe hukupaswa kukaa tu bila kuwa na hekima”. Hata mgeni anapokuja nyumbani kwako hatakuja kama anauhitaji, atakuja kama kashiba, au kama hana kiu..Lakini pengine ana njaa, na kiu..na anaweza kuondoka hivyo hivyo, kama wewe hutatumia hekima, angalau kumletea hata glasi ya maji… sio lazima akuambie naomba chakula!..kamwe hutasikia hilo likitoka kinywani mwake kama huyo mgeni ni mstaarabu.. Na Bwana Yesu ni hivyo hivyo, yeye ni mstaarabu wa wastaarabu, na watumishi wake wa kweli ni hivyo hivyo…kamwe hatakuja kwako na kukwambia nina haja na hichi au kile. Ni wajibu wako wewe kulijua hilo. Na kama hutakuwa na hekima ya kutosha ya kuweza kupambanua mambo, basi ni rahisi kuangukia katika hukumu siku ile ya mwisho.
Hilo ni jambo ambalo leo ningependa tulitafakari, leo ndugu. Popote pale ulipo mjali Bwana, pasipo kuambiwa, yapo maagizo ambayo Bwana atatuambia moja kwa moja bila kupinda panda, lakini yapo maagizo ambayo Bwana katuachia sisi wenyewe tuyapambanue, na tuyatekeleze…
Hebu tafakari hapo kanisani kwako, ni nini umefanya tangu umefika!.. kumbuka matendo yako yanatangulia hukumuni. Lakini usipokuwa na hekima kwa kudhani kuwa hakuna haja ya kumjali Bwana kwa matoleo yako, basi siku ile atakuweka katika kundi la mbuzi. Ni heri tukalijua hili mapema, ili siku ile ya mwisho tusije tukazuiliwa.
Hegai 1:4 “Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika”
Bwana atubariki na kutusaidia.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya siku moja kwa Bwana ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja? (2Petro 3:8)

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2021/05/06/maagizo-ambayo-hayajaagizwa/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.