by Admin | 13 November 2021 08:46 pm11
Je! Kucheza mpira au kushabikia mpira ni dhambi kulingana na maandiko?.
Bwana kutuumba miili yetu hii ili kuishughulisha, hajatuumbia ikae tu bila kujishughulisha..Na njia mojawapo ya kuishughulisha ni kwa kufanya mazoezi.
Na mazoezi hayo yanaweza kufanyika kwa njia ya kawaida au ya kucheza..Kwamfano watu wawili marafiki wanaweza kusimama na kushindana mbio, na mwisho wa mbio wakafurahi na kucheka, hatimaye wakawa wamecheza na hapo hapo kufanya mazoezi.
Sasa kucheza kwa namna hiyo sio dhambi lakini tatizo linakuja mfumo unaochanganyikana na mchezo huo.
Kwamfano mchezo unapohusisha kuvaa kuilimwengu, au matusi, au miziki ya kiulimwengu, au mambo yoyote yasiyo na adabu mchezo huo ni dhambi, na sisi wakristo hatupaswi kuushiriko.
Kwamfano riadha za siku hizi ili wanawake au wanaume washiriki, hawana budi kubaki na nguo za ndani tu!..na sehemu nyingine yote ya mwili kubaki wazi.
Utakuta wanawake wanakimbia riadha wakiwa na chupi tu, na wanaume hivyo hivyo. Sasa michezo ya namna hiyo ni dhambi kushiriki kwa mkristo.
Na kama ni dhambi, basi na hata kuishabikia vile vile ni dhambi.
Kadhalika watu wawili wanaweza kitengeneza mpira wao na kisha kuipiga piga kwa miguu yao kujifurahisha..jambo hilo sio dhambi.
Lakini inapotokea mchezo huo unachanganyikana na mfumo fulani wa kishetani, tayari mchezo huo unakuwa ni najisi kwakristo, kwamfano utakuta mchezo fulani unadhaminiwa na shirika la pombe au la sigara, au la kubeti kiasi kwamba hata sare za mchezo huo ni nembo la mashirika hayo najisi.
Au utakuta michezo mingine ni lazima ihusishe miziki ya kidunia ambayo ni najisi kwa mkristo.
Hapo hatupaswi sisi kama wakristo kushiriki michezo hiyo, wala kuwa wafuasi wa hiyo michezo.
Hivyo kwaasili michezo sio mibaya,
Hata Yakobo alicheza Mieleka na yule Malaika..
Lakini mieleka ya leo ni lazima ubakiwe na nguo za ndani tu!..Na tena siku hizi ni jinsia mbili tofauti zinapigana mieleka, kiasi kwamba huwezi kutazama mara mbili michezo hiyo imejaa matusi na ushetani.
Imefungamana na ushetani kiasi kwamba kitendo cha kuangalia tu tayari umenajisika..
Na siku zinavyozidi kwenda hiyo mifumo inazidi kuongezwa juu ya hiyo michezo na kuharibu kabisa maana ya michezo.
Huko mbeleni, riadha zitakuwa zinafanyika uchi wa mnyama kabisa, tofauti na leo ambapo ni nguo za ndani tu ndio zina sitiri.
Kama tunataka kucheza (sisi kama wakristo), tunaweza kucheza sisi kwasisi bila kutumia mifumo hiyo ya kishetani.
Lakini pia biblia imetuonya kuwa na kiasi, maana yake sio kucheza mpaka unakuwa unafanana na watu wa kidunia.
Vile vile mambo yote tunapaswa kuyafanya kwa utukufu wa Mungu. Ukicheza na mtoto wako inaweza ikatosha, ukicheza na kaka yako inatosha, ukicheza na rafiki zako wawili au watatu inatosha, sio lazima tujichangange na harambee za watu wengi wa kiulimwengu, kushiriki nao michezo iliyojaa unajisi na mizaha.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2021/11/13/je-ushabiki-wa-mpira-ni-dhambi/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.