Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri.

by Admin | 14 December 2021 08:46 pm12

SWALI: Nini maana ya huu mstari

Kumbukumbu 27: 24 “Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina”.


SWALI: Kulingana na sheria ya wayahudi, kosa lolotela kumdhuru mwenzako, liwe ni dogo au kubwa, lilipoonekana, adhabu yake ilitolewa palepale kulingana na kosa lenyewe.. kwamfano ukimng’oa mwenzako jino, na wewe pia uling’olewa la kwako, ukimtoa jicho, na lako pia linatolewa, ukiua na wewe pia uliuliwa,..hapo ndipo uovu ulipoweza kuondoka juu ya mtu.

Lakini kulikuwa na makosa mengine watu waliyafanya kwa siri, ambayo hayakuwa rahisi kugundulika kwa wazi, wanashangaa tu labda mtu kafa, wakidhani ni siku yake tu imefika, kumbe aliwekewa sumu siku nyingi ambayo ilikuwa inamuua kwa taratibu..

Sasa watu kama hawa, biblia inasema, wamelaaniwa, kwasababu wanawapiga wenzao kwa siri, wakidhani kuwa hata mbele za Mungu hawataonekana.

Mfano wa watu kama hawa katika biblia ni Yezebeli. Yeye alikwenda kumuua Nabothi Myezreeli, ili tu alipate shamba lake, akawaajiri watu wa kushuhudia uwongo waseme wamemsikia Nabothi amemtukana Mungu na mfalme, ili watu wampige mawe afe, na kweli akafanikiwa adhma yake, na watu hawakujua lolote.

Lakini Mungu alijua, ndipo akamtuma nabii Eliya kumtolea hukumu yake. Na kumwambia mbwa watamla maiti yake. Na kweli ndivyo ilivyokuja kuwa (1Wafalme 21).

Mwingine ni mfalme wa Daudi, yeye alimuua askari wake aliyeitwa Uria kwa siri akidhani kuwa Mungu hatamwona. Alichofanya ni kumwambia mkuu wake wa majeshi amweke, Uria mahali penye vita vikali, kisha wamuache mwenyewe, ili azidiwe na majeshi ya adui auliwe, na kweli, njama zake zilifanikiwa, lakini Mungu akamrudia Daudi na kumpa adhabu kali sana, na doa ambalo mpaka leo hii sisi tunalisoma (2Samweli 11).

Hata leo, watu wanawapiga wenzao kwa siri, kwa kuwawekea vikwazo mbalimbali, lakini kwa nje wanajifanya wapo Pamoja na wao kuwasaidia, tukiwa watu wa hivi Mungu atatulaani. Halikadhalika Wachawi wote wapo chini ya hii laana, kwasababu mchana wanacheka na wenzao kinafki, lakini usiku wanazunguka huku na huko kuwanga, na kuwasababishia wenzao madhara, na kuvuruga mipango ya watu wanaotaka kumtafuta Mungu.

Hivyo tuwe makini sana, ni heri uadhibiwe na mwanadamu, kuliko kuangukia katika laana za Mungu mwenyewe. Kwasababu yeye ndiye anayeichunguza mioyo ya watu. Ili tuweze kuishinda hii hali, hatuna budi kumaanisha kumfuata Kristo kweli kweli katika Maisha yetu. Hapo ndipo tutakapoweza kuishi Maisha ya upendo na wengine.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Mlima Gerizimu na Ebali ni ipi, na umuhimu wao rohoni ni upi?

Nini maana ya mstari huu: (Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake.Mithali 27:14 )?

MAAGIZO AMBAYO HAYAJAAGIZWA!

Ni SIRI gani Paulo aliyokuwa anaimaanisha katika Waefeso 5:32?

Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2021/12/14/na-alaaniwe-ampigaye-mwenzake/