Wale Nyoka wa Moto jangwani, walikuwa ni wa namna gani?

by Admin | 5 January 2022 08:46 pm01

Wale Nyoka waliowadhuru wana wa Israeli jangwani walikuwa wana maumbile ya moto au?. Maana maandiko yanasema walikuwa ni Nyoka wa moto, Na kama walikuwa wenye maumvile ya moto, waliwaumaje watu na walitokea wapi? Walishushwa au?

Jibu: Tusome,

Hesabu 21:6 “BWANA akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa”

Neno “moto” hapo halijatumika kuelezea maumbile (yaani miili) ya hao nyoka, kwamba wana miili iliyoundwa kwa malighafi ya moto, hapana!. Bali limetumika kuelezea “Rangi” ya hao Nyoka, kwamba wana rangi ya moto.

Rangi ya moto, inafananishwa na rangi ya “Shaba”. Mtu anaposema “sahani ile ni ya shaba” na anayesema “sahani ile ni ya moto” Ni kitu kimoja, wote wanamaanisha kitu kimoja.

Ndio maana baada ya pale utaona Musa anaagizwa atengeneze nyoka wa shaba, kuwakilisha rangi ya hao nyoka.

Hesabu 21:8 “Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi.

9 Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi”.

Nyoka hao wenye rangi ya moto, ni jamii ya Nyoka maarufu sana wenye sumu kali wanaopatikana jangwani, hadi leo wapo (Ni nyoka wa asili kabisa), maisha yao ni jangwani tu hawawezi kuishi mahali pengine, na huwa wanajificha chini ya mchanga, na kubakisha sehemu ndogo tu ya kichwa juu, hivyo si rahisi kuonekana.
Na endapo mtu akipita na bahati mbaya akakanyaga mchanga mahali ambapo nyoka huyo kajificha, basi aling’atwa na hakukuwa na matibabu.

Hivyo kwa hitimisho, walikuwa ni nyoka wa asili, isipokuwa rangi yao ni ya Moto (au shaba).

Lakini pamoja na hayo kulikuwa na ufunuo mkubwa juu ya tukio hilo lililowatokea wana wa Israeli, na huyo nyoka wa shaba, mpaka akaitwa Nehushtani.

Kwa maelezo marefu juu ya Nehushtani, unaweza kufungua hapa>> NEHUSHTANI.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312 Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/01/05/wale-nyoka-wa-moto-jangwani-walikuwa-ni-wa-namna-gani/