Dusumali ni nini katika biblia?

by Admin | 22 Machi 2022 08:46 mu03

Dusumali ni nini?, Mafurungu ni nini?, na Matalasimu ni nini?.. kama tunavyosoma katika Isaya 3:20?


Jibu: Tusome,

Isaya 3:20 “na dusumali, na mafurungu, na vitambi, na vibweta vya marashi, na matalasimu”

 1. Dusumali ni nini?

Dusumali ni aina ya mavazi ambayo yalikuwa yanavaliwa kichwani..ambayo yalikuwa yanatengenezwa na malighafi tofauti tofauti kulingana na tamaduni za jamii husika. Na waliokuwa wanazivaa sana ni watu mashuhuri au viongozi wa jamii hiyo…Kwajamii za maeneo ya Afrika, dusumali zilikuwa zinatengenezwa na manyoya ya ndege(Tazama picha juu).. Maeneo ya Misri, zilikuwa zinatengenezwa kwa vitambaa maalum.

 2. Mafurungu ni nini?

Mafurungu ni urembo unaofungiwa katika miguu ya wanawake..(Tazama picha chini).

mafurungu

 3. Matalasimu ni nini?

Matalasimu ni vitu ambavyo watu wanavivaa shingoni, au wanajifungia katika sehemu za miili yao, kama kinga yao. (kwa lugha ya sasa zinaweza kuitwa hirizi).

Lakini mavazi haya yote ni ya kidunia.. na watu wa Mungu waliookoka (wakiume na wakike) hawapaswi kuyavaa, kwani ni machukizo, ndio maana utaona hapo katika hiyo isaya mlango wa 3, Bwana anasema atawapiga wavaao hayo, kwasababu matendo yao yanaendana na mavazi yao..

Isaya 3:16 “Bwana akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienenda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao;

17 Basi, kwa hiyo, Bwana atawapiga binti za Sayuni kwa pele za utosini, na Bwana ataifunua aibu yao”.

18 Siku hiyo Bwana atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao;

19 na pete za masikio, na vikuku, na taji zao;

20 na dusumali, na mafurungu, na vitambi, na vibweta vya marashi, na matalasimu;

21 na pete, na azama”

Biblia inasema miili yetu ni HEKALU LA ROHO MTAKATIFU. Na si Nyumba tu!..bali hekalu (1Wakorintho 6:19)..Kama ni hekalu maana yake halipaswi kuvikwa hirizi, halipaswi kuvikwa vitu vya kikahaba.. kwani Mafurungu pamoja na vikuku na hazama, walikuwa wanavaa makahaba..

Kama binti wa kiMungu unapenda kujipamba basi biblia imetoa mwongozo mzuri wa namna ya kujipamba na kupendeza..

1Timetheo 2:9 “Vivyo hivyo wanawake NA WAJIPAMBE KWA MAVAZI YA KUJISITIRI, PAMOJA NA ADABU NZURI, NA MOYO WA KIASI; SI KWA KUSUKA NYWELE, WALA KWA DHAHABU NA LULU, WALA KWA NGUO ZA THAMANI;

10 BALI KWA MATENDO MEMA, KAMA IWAPASAVYO WANAWAKE WANAOUKIRI UCHAJI WA MUNGU”.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Kikuku/vikuku ni nini katika biblia?

Hazama ni nini katika biblia?(Ezekieli 16:12, Kutoka 24:47)

PINDO LA VAZI LAKE SASA LIMEREFUSHWA.

Ni nani aliyesema Nitume mimi? katika (Isaya 6:8)

Shubaka ni nini kibiblia? (Mithali 7:6)

Rudi nyumbani

WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/03/22/dusumali-ni-nini-katika-biblia/