Hazama ni nini katika biblia?(Ezekieli 16:12, Kutoka 24:47)

Hazama ni nini katika biblia?(Ezekieli 16:12, Kutoka 24:47)

Hazama ni nini?


Hazama ni pete ya puani.

Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi;

Mwanzo 24:47, Kutoka 35:22,

Na pia ukisoma Ezekieli sura ya 16 yote utaona jinsi Mungu anavyolilinganisha taifa la Israeli na msichana ambaye alipozaliwa tu alitelekezwa porini na wazazi wake akiwa hata hajakatwa kitovu chake. Na Bwana alipokuwa anapita (hapa akijifananisha na mwanaume fulani), alimwona na kumuhurumia, akamchukua na kwenda kumtunza, akamkuza,  akafanya naye maagano kuwa atakuwa wake, akamkuza vizuri sana, akawa mrembo sana, akamvisha mavazi mazuri, na kumpamba kwa kila aina ya mapambo ikiwemo hazama na vikuku, lakini baadaye alipokuja kuwa mtu mzima alikengeuka na kuanza kuzini na wanaume wengi, na kuwa kahaba wa kipindukia, ..

Ezekieli 16:11 “Nikakupamba kwa mapambo pia, nikatia vikuku mikononi mwako, na mkufu shingoni mwako.

12 NIKATIA HAZAMA PUANI MWAKO, na pete masikioni mwako, na taji nzuri juu ya kichwa chako.

13 Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; na mavazi yako yalikuwa ya kitani safi, na hariri, na kazi ya taraza; ulikula unga mzuri, na asali, na mafuta; nawe ulikuwa mzuri mno, ukafanikiwa hata kufikilia hali ya kifalme.

14 Sifa zako zikaenea kati ya mataifa kwa sababu ya uzuri wako; kwa maana ulikuwa mkamilifu, kwa sababu ya utukufu wangu niliokutia, asema Bwana MUNGU”.

Lakini sasa mfano huo haumaanishi kuwa wanawake wa ki-kristo wanaruhusiwa kujipamba hapana, kumbuka huo ni mfano tu ambao Mungu aliutoa kuonyesha ni jinsi gani Israeli taifa lake alilolipamba rohoni kwa utukufu wake, tangu zamani, baadaye likaja kukengeuka kuabudu miungu mingine tofauti nay eye.

Biblia inasema..

1Petro 3:1 “Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;

2 wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.

3 Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;

4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu”.

Umeona, mwanamke wa kikristo hapaswi kuweka hazama, au vikuku, au lipstick, au wanja, au mikufu, au hereni mwilini mwake, badala yake mapambo haya anapaswa ayahamishie rohoni, kwa matendo mema. Ndivyo biblia inavyoagiza.

Kwahiyo kama wewe ulikuwa unaweza hazama au vipini puani mwako, ni vyema ukaacha. Ishi sasa maisha ya kama wanawake wacha Mungu walivyoyaishi. Mapambo yasikusababishe uikose mbingu.

Shalom.

Tazama tafsiri ya maneno mengine chini.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

MASERAFI NI NANI?

Jabari ni nini, kama linavyotumika kwenye biblia?

Pomboo ni nini katika biblia?(Kutoka 25:5, Ezekieli 16:10)

Naomba kujua nini maana ya kuteguka uvungu wa paja?

WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.

NJONI, NUNUENI MLE NA MNYWE.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments