Nini tofauti ya Uwezo na Uweza kibiblia?

by Admin | 10 April 2022 08:46 pm04

Jibu: Uwezo na Uweza ni kitu kimoja.. tofauti ni kwamba kimoja kinatumika kwa Mungu na kingine kwa wanadamu.

Wanadamu na wanyama na shetani na malaika na viumbe vingine vyote vinao UWEZO wa kufanya mambo. Lakini havina UWEZA wa kufanya jambo.

Mwenye UWEZA wa kufanya jambo ni Mungu tu peke yake.

Mwanadamu ana UWEZO wa kuua lakini wa kuurudisha Uhai hana…kwasababu kuurudisha uhai ndani ya mtu kunahitaji UWEZA, na UWEZA huo anao Mungu tu.

1 Wakorintho 6:14 “Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa UWEZA wake”.

Vile vile mwanadamu na shetani wanao UWEZO wa kuipotosha roho, lakini Kuiokoa hawawezi!..Kwasababu kuiokoa roho ya Mwanadamu inahitajika UWEZA na sio UWEZO. NA Uweza huo ni Mungu tu! Ndio anao.

Warumi 1:16 “Kwa maana siionei haya Injili; KWASABABA NI UWEZA WA MUNGU UULETAO WOKOVU, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia”.

Swali ni je!..Unawatumainia wenye UWEZO au mwenye UWEZA?.

Shetani anao uwezo wa kukupa mali lakini si Uzima wa milele!, Wanadamu wana uwezo wa kukupotosha lakini wa kukuokoa hawawezi.

Mwanadamu anao uwezo wa kutibu, lakini kuponya hawezi, Mwenye Uwezo wa kuponya nk Mungu tu peke yake.

Unaweza kusoma pia juu ya Uweza wa Mungu katika Nehemia 1:10, Nehema 9:32, Marko 12:24, na Matendo 8:10.

Kwanini usimtumainie huyo mwenye uweza wa kufanya mambo yote, huyo ndio wa kumtumainia na vile vile wa kumwogopa..

Luka 12:5 “Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha kumwua mtu ana UWEZA wa kumtupa katika Jehanum; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo”.

Na sasa UWEZA huo wa kiungu upo juu ya Bwana Yesu Kristo pekee, ambaye mamlaka yote ya mbinguni na duniani, amekabidhiwa yeye.

Isaya 9:6 “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,Tumepewa mtoto mwanamume; Na UWEZA wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani”.

Je umempokea Yesu?..kama bado unasubiri nini?

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

Tofauti ya deni na dhambi ni nini?

Roho Mtakatifu ni nani?.

NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?

MFANYE BWANA YESU MWENYEJI MAISHANI MWAKO.

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/04/10/nini-tofauti-ya-uwezo-na-uweza-kibiblia/