Tofauti ya deni na dhambi ni nini?

Tofauti ya deni na dhambi ni nini?

Katika Marko 6:12 maandiko yanasema…“Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu”… Hizi deni ndio zipi??

Jibu: Mtu aliyekutukana ana deni kwako la kuja kukuomba radhi!..Hilo ni deni lake kwako, awe anajua au hajui…Na kulilipa ni yeye kuja kukuomba wewe radhi!.. Asipokuja kukuomba radhi basi hilo litabaki kuwa deni kwake. (wewe utakuwa unamdai). Labda wewe uamue kumsamehe tu!

Hali kadhalika na sisi tunapomfanyia Mungu dhambi, tunakuwa na deni kwake la KUUNGAMA! (Maana yake kukiri makosa yetu na kuomba radhi kwake)!. Hayo ni madeni kwetu kwa Mungu..

Kwa maana dhambi ni kosa lolote mtu analolifanya dhidi ya Mungu.

Lakini Bwana wetu Yesu alitufundisha kuwa ni lazima tuwasamehe watu madeni yao ili na sisi tusamehewe yetu!.. Maana yake, yale mambo ambayo wangepaswa waje waungame mbele yetu (yaani kukiri na kuomba radhi), wanapoungama basi tunawasamehe, na hata wasipokuja kuomba radhi vile vile tunapaswa tuwasamehe.

Na wakati mwingine watu wanatukosa pasipo hata wao kujua kama wametukosa, hivyo hawawezi kuja kutuomba radhi kwasababu hata hawajui kama wametukosea, (Hivyo wanabakia kuwa na madeni kwetu ambayo hawajui hata kama wanayo)..

Kadhalika na sisi tunamkosea Mungu kwa mambo mengi, ambayo wakati mwingine hatujui kama tunamkosea (Jambo linalotufanya tuwe na madeni mengi mbele za Mungu), hata pasipo sisi wenyewe kujua.

Kwahiyo tunapoomba hiyo sala ya Baba yetu!, na kusema “utusamehe deni zetu”.. Maana yake tunamsihi Mungu atusamehe yale makosa ambayo hatukuyatubia au yale tuliyoyafanya pasipo kujua kuwa ni makosa…Na Mungu ni mwaminifu, anatusamehe…lakini kama tu na sisi tutakuwa tayari kuwasamehe wengine madeni yao.

Swali ni Je!, na wewe umemsamehe yule aliyekutukana au kukusengenya au kukutapeli? au unasubiri aje kukuomba radhi?…nakuambia usingoje!..wewe msamehe hata bila yeye kukuomba radhi, ndivyo na Mungu atakavyokusamehe na wewe makosa ambayo hata wewe hukumwomba radhi!..

Bwana wetu Yesu Kristo, aliwasamehe wale wote, ambao walimsulubisha, (Aliwasamehe pasipo wao kumwomba msamaha).. kwakufanya vile alitupa na sisi kielelezo, kwamba na sisi tuwasamehe wenzetu kama yeye alivyotusamehe. Kwasababu tusipowasamehe watu makosa yao na Mungu wetu hatatusamehe sisi.

Mathayo 18:21“Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?

22 YESU AKAMWAMBIA, SIKUAMBII HATA MARA SABA, BALI HATA SABA MARA SABINI.

23 Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake.

24 Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi.

25 Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni.

26 Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia.

27 Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni.

28 Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia akamkamata,akamshika koo,akisema Nilipe uwiwacho.

29 Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia.

30 Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni.

31 Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka

32 Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi;

33 nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?

34 Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote.

35 Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.”

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.

JE KUNA UISLAMU KATIKA BIBLIA?

Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?

NI KIPI KINAMZUIA MUNGU KUZUNGUMZA NA SISI?

Kwa namna gani mauti hufanya kazi ndani yetu na uzima kwa wengine? (2Wakorintho 4:12).

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments