Kwanini Bwana Yesu alisema “Msimwamkie mtu njiani”?

Kwanini Bwana Yesu alisema “Msimwamkie mtu njiani”?

Bwana Yesu alimaanisha nini kusema, msimwamkie mtu njiani? (Luka 10:4).. Na wakati huo huo alisema katika Mathayo 5:47, kuwa “tukiwaamkia ndugu zetu tu!, tunatenda tendo gani la ziada”.

Jibu: Labda tuanzie kusoma kuanzia mstari wa kwanza…

Luka 10:1 “Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe.

2 Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake.

3 Enendeni, angalieni, nawatuma kama wana kondoo kati ya mbwa-mwitu.

4 Msichukue mfuko, wala mkoba, wala viatu; WALA MSIMWAMKIE MTU NJIANI”.

Mwalimu anapotoa tangazo kwa wanafunzi wake na kuwaambia… “si ruhusa kuzungumza na mtu yeyote ndani ya chumba cha mtihani”.. Kwa kusema hivyo hajamaanisha kuwa “si ruhusa kuzungumza na mtu kila mahali” Hapana!.. bali ni katika chumba cha mtihani tu!..wakiwa mahali pengine wanaweza kuzungumza..

Na kadhalika Bwana hakuwakataza wanafunzi wake “kuwaamkia/kuwasalimia watu kabisa”..hapana!..bali wanapokuwepo katika “Safari ya uinjilisti” hapo ndipo “Alipowazuia wasiamkie amkie watu njiani”.

Sasa kwanini awazuie kufanya hivyo, wakiwa katika safari ya kwenda kuhubiri?

Ni kwasababu salamu zinacheleweza lile kusudi, na ni rahisi kumhamisha mtu kifikra kutoka katika mawazo ya kwenda kuhubiri mpaka kuanza kufikiri mambo mengine tofauti na yanayohusu injili anayokwenda kuhubiri..

Hebu tengeneza picha Mwanafunzi mmojawapo wa Bwana Yesu, anakwenda kuhubiri, halafu njiani anapita karibu na nyumba ya Mjomba wake..halafu anaingia kumsalimia, na katika mazungumzo anapewa taarifa mbalimbali aidha za misiba, au za watu wengine au nyingine zozote..

Au anapewa jukumu lingine la kufanya huko anakokwenda, labda anaambiwa ukifika mahali fulani naomba uninunulie kitu fulani, ukirudi nipitishie hapa, au ukifika mahali fulani nisiaidie kuulizia hili au lile, au ukifika sehemu Fulani kumbuka kumsalimia mtu Fulani, au huko unakokwenda kuwa makini nako kuna hatari n.k..

Ni wazi kuwa kuanzia huo wakati na kuendelea mawazo ya yule mwanafunzi yatakuwa yametawaliwa na yale aliyoyasikia kutoka kwa ndugu yake huyo, na yale ya injili yatakuwa yamemezwa…

Kwahiyo ili kulizuilia hilo.. ndipo Bwana akasema… “Msiwaamkie watu njiani”.. ili mawazo yao na akili zao ziwe katika Injili wanayokwenda kuihubiri..

Lakini watakapomaliza safari yao hiyo ya injili wapo huru kuwaamkia watu wowote pasipo kupendelea sawasawa na Neno hilo la Bwana katika Mathayo 5:47

Kadhalika na sisi, tunapokuwa katika uinjilisti, hatupaswi kuuchanganya na mambo mengine, tunapokuwa katika kuifanya kazi ya Mungu, hatuna budi akili zetu, mawazo yetu, kuyafunga yasiingiliwe na mawazo mengine.. (kadhalika tunapokuwa katika ibada ni sharti kuzima simu, ili kuongeza umakini katika kuomba, kusifu na kusikiliza Neno).

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

BADO TUTAHITAJI TU KUSAIDIANA.

UKIOKOKA, JIANDAE KUPITISHWA USIPOPATAZAMIA.

Karama ya pili inayozungumziwa katika 2Wakorintho 1:15 ndio ipi?

Je shetani ana uwezo wa kujua mawazo ya mtu?

Kuhubiri injili kwa husuda na fitina ndio kupi?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments