Karama ya pili inayozungumziwa katika 2Wakorintho 1:15 ndio ipi?

Karama ya pili inayozungumziwa katika 2Wakorintho 1:15 ndio ipi?

Tusome,

2Wakorintho 1:15 “Nami nikiwa na tumaini hilo nalitaka kufika kwenu hapo kwanza, ili mpate karama ya pili

Sio wakati wote neno “karama” linapotumika kwenye biblia linamaanisha “karama ya roho kama vile unabii, uchungaji, ualimu n.k”. Bali karama pia ni neno linalomaanisha “Zawadi au Baraka”.

Kwamfano kuna andiko linasema “karama ya Mungu ni uzima wa milele”.

Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

 Sasa hapo haimaanishi kwamba Mungu karama yake ni “Uzima wa milele” kama sisi karama zetu zilivyo kutoa unabii, au Kunena kwa lugha, au kutabiri nk.

Mungu yeye hana kipawa fulani maalumu, kwasababu vyote vinatoka kwake.

Bali hapo biblia imemaanisha kuwa “Zawadi ya Mungu ni uzima wa milele”..au “Baraka ya Mungu kwetu ni uzima wa milele”

Kadhalika Mtume Paulo aliposema  kuwa “nalitaka kufika kwenu hapo kwanza, ili mpate karama ya pili” hakumaanisha kuwa kuna karama nyingine ya pili tofauti na hiyo ya kitume aliyokuwa nayo,  au nyingine mpya  hivyo anataka kwenda kuwapa, au kuwanufaisha katika hiyo, hapana!, bali alimaanisha “Baraka ya Pili”.

Ni sawa mhubiri aliyeko Dar es Salaam, aende kuhubiri Morogoro, kwa wiki moja na kisha arudi Dar, na ghafla apate tena safari ya kwenda Dodoma kuhubiri baada ya wiki moja wakati kasharudi Dar, bila shaka hawezi kufika Dodoma bila kupita Morogoro, hivyo Mhubiri huyu akawasiliana na wale aliokwenda kuwahubiria hapo kwanza  (Watu wa Morogoro) kwamba atapita tena kuhubiri kwa siku moja na siku inayofuata atakwenda Dodoma.. Hivyo watu wa Morogoro wakawa wamepata Baraka mara mbili. Ndicho Mtume Paulo alichomaanisha hapo!.

Kwamba alishapita kwao (watu wa Korintho) na kuwabariki kwa Mafundisho akaondoka, lakini alitaka tena kupita kwao kwa mara nyingine ya pili wakati anaelekea Makedonia ili wapate Baraka mara mbili.

Maisha ya Paulo yanatufundisha kuwa na bidii na jitihada katika kuifanya kazi ya Mungu, ijapokuwa Paulo alikuwa anapitia vita vikali katika kuhubiri, lakini mara zote alitafuta kurudia kuhubiri mahali ambapo ameshapita kuhubiri.

Matendo 15:36 “Baada ya siku kadha wa kadha Paulo akamwambia Barnaba, Haya! Mrejee sasa tukawaangalie hao ndugu katika kila mji tulipolihubiri neno la Bwana, wa hali gani”.

Bwana atusaidie na sisi tuwe kama watakatifu hawa wa kanisa la kwanza.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Pia kama utapenda uwe unafikiwa na masomo ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP basi bofya hapa ujiunge moja kwa moja  >>>> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?

Kuhubiri injili kwa husuda na fitina ndio kupi?

NA VIUNGO VYETU VISIVYO NA UZURI VINA UZURI ZAIDI SANA.

USIRUDI NYUMA KWA KUITUMAINIA HAKI YAKO.

Talanta ni nini katika biblia (Mathayo 25:14-30)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments