by Admin | 5 October 2022 08:46 pm10
SWALI: Huu mstari una maana gani?
Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana”.
JIBU: Mstari huo unatupa picha kuwa, kumbe vipo vitu vya kurithishwa, lakini pia kuna vitu ambavyo hatuvipati kwa kurithishwa..
Kwamfano, hapo anasema mali; kama nyumba, magari, kazi, hivi vitu mtu anaweza kuvipata kutoka kwa wazazi wake,..Lakini linapokuja suala la MKE MWENYE BUSARA. Sio jambo la kurithishwa, au kutafutiwa na wazazi, au kupatwa kwa njia ya mali, au kwa uzuri, au kwa cheo, au kwa nguvu..Hapana, bali mke mwenye busara anatoka kwa Mungu tu! Na si sehemu nyingine.
Kumbuka hapo anasema ‘mke mwenye busara’..Sio ‘mke’…ikiwa na maana, ‘mke’ anaweza kupatikana popote tu pale, hata bar, kazini, barabarani, disco, vyuoni, mtaani, n.k. utampata.. Lakini mwenye busara, hatoki pengine isipokuwa kwa Bwana tu.
Ndio kama huyu aliyezungumziwa katika Mithali 31:10-31..Ambaye sifa zake ni; Kumcha Bwana siku zote, kuwahurumia maskini na wahitaji, Kuishi vyema na watumwa wake, kuwa msaidizi kwa mumewe, asiye mvivu n.k. Biblia pia inasema katika 1Petro 3:1-6 mke mwenye busara ni Ni mtiifu kwa mumewe, mpole, mtulivu, ajisitiriye, aitunzaye nyumba yake.
Hivyo kumpata huyu, wala usijichoshe kwa njia za vitu au mali. Bali nenda mbele za Bwana, mwombe, mshirikishe, mpango wako, kisha yeye mwenyewe atamsogeza kwako, na utamfurahia.
Kumbuka: Kinyume chake pia ni kweli. Mume mwenye busara, hapatikani pengine popote isipokuwa kwa Bwana tu. Mume mwenye busara, ni Yule amchaye Bwana, ampendaye mke wake, kama nafsi yake mwenyewe, ailindaye familia yake, aihudumiaye nyumba yake.(Waefeso 5:25). Hivyo yakupasa umwombe Bwana, kabla ya kuchukua maamuzi ya kutafuta mke/mume.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI.
WANA-NDOA: Baba Mkwe, Na mama Mkwe.
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)
Je! taratibu za kufunga ndoa [yaani harusi] ni agizo la Mungu au ni mapokeo tu ya kibinadamu?
Biblia inakataza kuapa kabisa, lakini kwanini watu wanaapa mahakamani na katika vifungo vya ndoa?
MAMBO MANNE,YANAYODHOOFISHA UOMBAJI WAKO.
KUMJUA YESU SI KUPATA UZIMA WA MILELE.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/10/05/bali-mke-mwenye-busara-mtu-hupewa-na-bwana/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.