Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake, Ni ndugu yake aliye mharabu

by Admin | 19 November 2022 08:46 am11

SWALI: Mstari huu unamaana gani?

Mithali 18:9 “Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake, Ni ndugu yake aliye mharabu”.

JIBU: Mharabu ni neno linalomaanisha “Mharibifu”.. Hivyo hapo anaposema yeye aliye mvivu katika kazi yake ni ndugu yake aliye mharabu. Anaonyesha ni jinsi gani uvivu katika kazi, unavyokwenda sambamba na uharibifu wa vitu/mambo. Kama mtu na ndugu yake.

Kwamfano, mtu anayefanyakazi chini ya ubora, labda tuseme mkandarasi wa daraja, .. Kwasababu, hawi makini na kazi yake, atajenga daraja bovu, sasa licha ya kwamba atapoteza pesa nyingi za watu waliompa hiyo kazi, lakini pia anaweka maisha ya wengi hatarini, siku likikorongoka wengi watapoteza maisha. Sasa huyu hana tofauti na mharibifu, au Yule muuaji.

Watu wengi wamesababishiwa matatizo ya kiafya, kwasababu wamekula vyakula vilivyotengenezwa chini ya ubora. Mtu mvivu hutafuta njia ya mkato, ili kufikia malengo yake, na hiyo ndiyo inayopelekea kusababisha madhara kwa wengine..

Hata katika kazi ya Mungu, watu wengi wakiona jambo walilolitarajia linakawia au linapatikana kwa ugumu, huanza kutafuta njia za mkato kwa  kutunga mafundisho ya uongo, na kutumia njia ambazo Mungu hajaziruhusu, lengo ni ili wawapate watu wengi kiharaka. Hatuwezi  kusubiri, kwa kuomba na kujifunza kwa kipindi kirefu, mpaka tutakapokomaa, badala yake tunaruka madarasa ya Mungu, tunaona njia ya jangwani itatuchosha, haina faida, hatupati chochote, wacha tuifuate njia ya kora .. Matokeo yake tunafanya kazi ya Mungu chini ya ubora, tunawapotosha wengine, kwa elimu na injili gheni.

Maandiko yametutahadharisha sana  katika kuitenda kazi ya Mungu, yanasema.

Yeremia 48:10 “Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Bwana kwa ulegevu..”

Tukiitwa kumtumikia Mungu, katika nafasi yoyote, iwe ni uchungaji, uimbaji, utume, ushemaji n.k. tukubali na gharama zake. Kwamba “tumeaminiwa uwakili” kama alivyosema mtume Paulo, tukijua kuwa siku ya hukumu tutaona hesabu ya utumishi wetu (1Wakorintho 9:16-17). Hivyo tuwe makini katika hilo, tusije tukawa waharibifu, kwa uvivu wetu.

Bwana atusaidie.

 Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Mharabu ni nani katika biblia?

SHAMBA HUWA HALIMTAMBUI WALA KUMSUBIRIA MKULIMA.

Nini maana ya kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua (Mithali 13:12)?

Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu?

Nini maana ya “Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea;?

Je Lutu alikwenda kuwahukumu watu wa Sodoma na Gomora? Kulingana na Mwanzo 19:9?

Je ile nyota ya asubuhi inamwakilisha shetani au Bwana Yesu?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/11/19/yeye-naye-aliye-mvivu-katika-kazi-yake-ni-ndugu-yake-aliye-mharabu/