Yesu alipopanda kuomba kwanini atokewe na Musa na Eliya na sio manabii wengine?

by Admin | 8 June 2023 08:46 am06

SWALI: Katika ule mlima mrefu, aliopanda Yesu na wanafunzi wake kuomba, kwanini atokewe na Musa na Eliya na sio manabii wengine? Mfano wa Isaya au Samweli?


JIBU: Awali ya yote yeye kutokewa na wale watu halikuwa Kwa lengo lake. Bali Kwa lengo la wale wanafunzi aliokuwa nao,  Ili kutimizi mambo yafuatayo.

1 ) Kutimiza unabii mkuu uliomuhusu yeye.

a) Unabii wa kwanza ni ule alioutoa Musa kuwa atakuja Nabii mwingine kama yeye na kwamba watu wamsikilize..

Kumbukumbu la Torati 18:15

[15]BWANA, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye.

Soma pia Matendo 3:22-25,. Hivyo wayahudi walikuwa na matarajio ya kuona mtu anayefanana  na Musa atakayeleta Sheria mpya  akija duniani, lakini akiwa na nguvu na uweza mwingi mfano wa Musa..

Ndio sababu ya Musa kutokea mbele ya wanafunzi wake, ili Mungu awathibitishie huyu ndio yule Musa aliyemnenea habari zake.

b) Lakini pia unabii uliohusu kutangulia Kwa Eliya kabla ya Kuja kwake duniani.

Wanafunzi walikuwa na dukuduku kama huyu, ndiye Kristo aliyetabiriwa au sio, na kama ndio mbona Eliya hajatangulia mbele yake tukamwona? Kwasababu waliambiwa hivyo na waandishi. Lakini sasa walipomwona Eliya mwenyewe amesimama mbele ya Yesu wakaamini lakini bado hawakuelewa..Sasa walipokuwa wanashuka ndio wakapata nguvu ya kumuulizia hilo swali.. Na hili ndio likawa jibu lake.

Mathayo 17:9-13

[9]Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu ye yote habari ya maono hayo, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu.

[10]Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza?

[11]Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote,

[12]ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao.

[13]Ndipo wale wanafunzi walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji.

2) Na Pili ni Kutoa utata Kuwa yeye sio mmojawapo wa manabii wakubwa wa kale wanaodhaniwa.

Utakumbuka kabla ya kupanda mlimani aliwaliza watu kuwa wanamzungumzia kuwa yeye ni nani? Wanafunzi wakamjibu kuwa wanasema yeye ni Eliya, wengine mmojawapo wa manabii wa Kale.n.k. Hivyo kulikuwa na utata mwingi. Lakini siku hiyo alitoa utata huo Soma.Mathayo 16:13-18. 

Mitume walipoona sura za manabii wao wa kale wamesimama mbele ya Yesu, mwenye utukufu mwingi sana kupitia wao. Wakaamini yeye ni zaidi ya manabii wote wakubwa Kwa wadogo waliowahi kutokea katika historia.

3) Lakini pia alikuwa na Lengo la kuwafunulia kuwa atakufa kama mmojawapo wa manabii wakubwa, lakini pia atapaa kama mmojawapo wa manabii wakubwa.

Musa alikufa, lakini Eliya alipaa.

Yesu ndio mtu pekee miongoni mwa wanadamu, aliyekufa, Kisha akazikwa, kisha akafufuka.na mwisho akapaa. Kwa hiyo Ile ilikuwa ni lugha ya kinabii, kueleza hatma yake na ndio maana hata manabii Hao walikuwa wakizungumza mambo yahusuyo kufa kwake na kufufuka.(Luka 9:31).  

Hizo ndio zilikuwa sababu kuu za Bwana kutokewa na manabii wale wawili na sio wengine. Na walipokuwa wanashuka Akawaambia wanafunzi wake wasimwambie mtu mpaka atakapofufuka katika wafu.

Kufunua nini?

SI wote watamwona Yesu katika kilele Cha utukufu wake, isipokuwa wale tu walio na kiu na yeye. Ambao watakuwa tayari kuwa karibu naye wakati wote mfano wa Hawa wanafunzi watatu yaani Yohana, Petro na Yakobo.

Ukimpenda Yesu tumia muda mwingi kuwepo uweponi mwake. Utamjua sana Kwa mapana na marefu yake.

Je! Umeokoka? Je unatambua kuwa hizi ni siku za mwisho na Kristo yupo mlangoni kurudi? Dalili zote zimeshatimia, unasubiri nini usimpe Bwana maisha yako, embu fanya uamuzi leo. Tubu dhambi zako, mgeukie Yesu, Unyakuo usikupite. Ikiwa utapenda upate mwongozo huo, wasiliana nasi kwa namba zetu hizi bure +255693036618 /+255789001312

Shalom

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.

Je Eliya aliandika waraka baada ya kupaa mbinguni?

UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?

Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?

Je! Umeona asali? Kula kadiri ya kukutosha;

KUWA MAKINI, HATUA ZA UNYAKUO ZINAENDELEA.

LAKINI MAKINDA WAWEZA KUYATWAA UWE NAYO.

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/06/08/kwanini-yesu-atokewe-na-musa-na-eliya-na-sio-manabii-wengine/