LAKINI MAKINDA WAWEZA KUYATWAA UWE NAYO.

LAKINI MAKINDA WAWEZA KUYATWAA UWE NAYO.

Ulishawahi kujiuliza ni nini Mungu anafundisha wana wa Israeli nyuma ya agizo hili? Tunalolisoma katika Kumbukumbu 22:6

 “Kiota cha ndege kikitukia kuwa mbele yako njiani, katika mti wo wote, au chini, chenye makinda au mayai, naye koo ameatamia juu ya makinda, au juu ya mayai, usimtwae yule koo pamoja na makinda;  7 sharti umwache yule koo aende zake, lakini makinda waweza kuyatwaa uwe nayo; ili upate kufanikiwa, ufanye siku zako kuwa nyingi”.

Bwana aliwapa agizo, endapo mtu yeyote akipita, njiani au karibu na kichaka, kisha akakutana na kiota cha ndege koo kimelala pale karibuni, kinatekeka kirahisi, kiasi kwamba unaweza kuwachukua wote, bila nguvu yoyote.Basi hapo, walipewa sharti, wasiwe na tamaa ya kuwachukua wote,  bali wamwache koo aende zake akaendeleze uzao, lakini wale makinda anaweza kuwachukua na kuwafanya wake. Hivyo kwa kitendo hicho tu, mtu anajiongezea siku za kuishi duniani.

Ufunuo wake ni upi Katika Ukristo na katika maisha?

1) Katika Maisha.

Ni mara ngapi tunaona watoto wa jamaa zetu, wamekuwa mayatima, au wazazi wao wapo katika hali ya kutojiweza kupitiliza, mpaka wanashindwa kuwamudu watoto wao, lakini sisi tunapita hatuna muda nao kisa tu sio sisi tuliowazaa . Tunawaona watoto wale wakiangamia pamoja na wazazi wao. Bwana anatushauri, tusifanye hivyo, ni heri tusiwajali wale wazazi, tuwaache, tusiwape kitu chochote, lakini wale watoto tuwahurumie, kwani tukifanya hivyo, Mungu atatubariki na kutuongezea siku za kuishi duniani.

Watu wengi tunadhani, kuwaheshimu tu wazazi, ndio tunapata siku nyingi za kuishi, lakini ukweli ni kwamba, ukiwajali  pia watoto wa asiyejiweza, utajiongezea siku pia za kuishi duniani.

2) Katika ukristo.

Vilevile katika ukristo. Ipo mikusanyika mingi, Yapo makanisa mengi, zipo huduma nyingi, ambazo haziwaweki watu katika mstari wa wokovu wa kweli, viongozi wao ni vipofu, hivyo na wale wanaoongozwa pia watakuwa ni vipofu, na mwisho wa siku wote watatumbukia shimoni. Sasa ikiwa wewe ni mchungaji au mkristo, na unaona mwenzako mahali alipo anapotezwa..Usikae kimya, na kusema wale sio washirika wangu, au wale sio wa dhehebu langu, au wale sio wa dini yetu..Bali unapaswa kuwaeleza ukweli, uwavute katika mahali sahihi ili uokoe roho zao..

Yawezekana ikawa ni ngumu kumgeuza kiongozi, hivyo usihangaike naye sana ikiwa utashindwa kumfikia, lakini wale makinda hakikisha unawajuza njia sahihi. Hiyo itakuongezea siku zako za kuishi hapa duniani.

Katika siku hizi za mwisho, watu wengi wamewekwa sehemu za hatari, wengine wameaminishwa katika watu, wengine vitu, wengine katika dini, wengine taasisi..lakini Kristo hayupo kabisa mioyoni mwao. Hawamjui, hawalifahamu Neno, hawajui nyakati wanazoishi, dini walizopo ni za kipagani. Sasa hii ni hatari sana, tunapoona wakiendelea katika kudanganywa na viongozi wao ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao. Hivyo sisi tuwe wa kwanza kulihubiria hili kundi la Mungu, litoke huko lirudi kwenye Neno.

Bwana atusaidie shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

KOIKOI ANGANI AJUA NYAKATI ZAKE ZILIZOAMRIWA.

Uzima wa milele ni nini?

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU WATOTO.

NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?

Watu wenye ulemavu wa akili, wataenda mbinguni?

Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang’anywa watoto wake.

MTEGO HUTEGWA BURE, MBELE YA MACHO YA NDEGE YE YOTE.

Thenashara ni nini? (Marko3:16)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Ereve Ngoy
Ereve Ngoy
1 year ago

Shalom
Kupanga uzazi ni vibaya?