Thenashara ni nini? (Marko3:16)

Thenashara ni nini? (Marko3:16)

Thenashara ni neno la kiebrania linalomaanisha namba “kumi na mbili” (12). Kwahiyo badala ya kusema watu 12, ni sahihi kabisa kusema “watu Thenashara”, au badala ya kusema “miezi 12” ni sahihi kusema “miezi Thenashara”…badala ya kusema makabila 12 ni sawa na kusema “Makabila thenashara” n.k

Biblia imelitumia Neno hilo Thenashara kuwakilisha wale Wanafunzi 12 wa Bwana Yesu, ambao baadaye waliitwa Mitume.

Marko 3:16  “Akawaweka wale Thenashara; na Simoni akampa jina la Petro;

17  na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye Yakobo, akawapa jina la Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo;

18  na Andrea, na Filipo, na Bartholomayo, na Mathayo, na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Thadayo, na Simoni Mkananayo,

19  na Yuda Iskariote, ndiye aliyemsaliti. Kisha akaingia nyumbani”

Na ni kwanini wanafunzi hawa 12, watenganishwe kwa kuitwa hivyo Thenashara?.. Ni kwasababu Bwana Yesu alikuwa anao wanafunzi wengine wengi zaidi ya 70,

Luka 10:1 “Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe.”

 hivyo ili kuwatofautisha hawa wanafunzi 70 na wale 12 aliowateua kwanza kndio likatumika hilo neno “Thenashara”

Unaweza kulisoma neno hilo pia katika Mathayo 26:14-16, Marko 4:10, Marko 9:35, na Yohana 20:24

Je umefanyika kuwa Mwanafunzi wa Yesu? kwa kutubu dhambi zako zote, na kumaanisha kuziacha na vile vile kuchukua msalaba wako na kumfuata yeye?

Luka 14:27  “Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MPENDEZE MUNGU ZAIDI.

Biblia imemaanisha nini iliposema “hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu”

NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?

Wahuni ni watu gani katika biblia?

SINA PESA SASA, YESU ATANISAIDIA NINI?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments