WALA HAKUACHA MTU ACHUKUE CHOMBO KATI YA HEKALU.

by Admin | 27 June 2023 08:46 am06

Karibu tujifunze biblia.

Leo tutajifunza moja ya taratibu illiyokuwa inaendelea katika Hekalu la Mungu ambayo haikuwa inampendeza Mungu.

Tusome,

Marko 11:15  “Wakafika Yerusalemu, naye akaingia ndani ya hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza na kununua ndani ya hekalu, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao wauzao njiwa;

16  WALA HAKUACHA MTU ACHUKUE CHOMBO KATI YA HEKALU”.

Maandiko haya ni maarufu tunapoyasoma husuani mahali hapo Bwana alipowafukuza waliokuwa wanauza njiwa na waliokuwa wanabadili fedha.

Lakini tukizidi kujifunza, tutaona sio kundi hilo tu Bwana alilolifukuza na kuliadhibu. Bali kulikuwa na kundi lingine pia ambalo lilikuwa linapandisha harufu mbaya mbele za Mungu.  Na kundi hilo ni lile la watu waliokuwa WANACHUKUA CHOMBO NDANI YA HEKALU.

Sasa kuchukua Chombo kunakozungumziwa hapo si “KUIBA VYOMBO VYA HEKALUNI au KUHAMISHA CHOMBO NDANI YA HEKALU” Hapana! Bali ni KUPITA au KUKATISHA na Chombo ndani ya Hekalu, Na chombo ni kitu chochote cha kubebea bidhaa au kurahisisha kazi kama makapu, au matenga au baiskeli.

Sasa mahali hekalu lilipojengwa lilikuwa linatengenisha sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni Bethsaida (mahali palipokuwa na soko kubwa la kondoo) na Sehemu ya juu ya “Mji wa juu”. Hivyo watu waliotoka Mjini kuelekea Bethsaida sokoni walianza tabia ya kukatiza katika ukumbi wa hekalu kama njia ya mkato (shortcut) ya wao kufika Bethsaida.

Kwahiyo kulikuwa na kundi kubwa la watu wanaokatiza pale wakiwa na vyombo vyao kila siku, Kwaufupi paligeuzwa kuwa njia, mtu yeyote alipita, wezi walikatiza, wahuni walipita, wasengenyaji walikatiza na stori zao za kuwasema wengine, waliotaka kwenda sokoni kuweka vimeza vya Kamari walikatiza kila siku na meza zao, matapeli ndio shortcut yao  hiyo n.k

Tabia ambayo Bwana Yesu hakupendezwa nayo!. Hivyo akasimama pia katika maingilio na matokeo ya Hekalu akawazuia wote waliokuwa wanakatiza!.. Huenda pia nao walitandikwa na kile kikoto!!.

Sasa tabia kama hiyo pia inaendelea katika nyumba za Mungu leo (Makanisani), utakuta kuna miingiliano ya watu wanaokatiza katiza na wanaozunguka zunguka!, wasio na fikra habari na mambo ya kiMungu… Wengi wa hao hawapiti kwa lengo la kumsogelea Mungu bali kwasababu ya shughuli zao, na biashara zao na ajenda zao, wanaouza chakula wanaingia wanavyotaka, wanaouza viatu wanaingia wanavyotaka, watoto wanaotaka kucheza kutoka huko nje basi eneo la kanisa ndio ukumbi wao n.k.. ni muhimu kuwa makini sana!!

Ni lazima, kuifanya Nyumba ya Mungu kuwa nyumba ya Mungu… kama tu sisi hatupendi watu wakatize kwenye maeneo ya Nyumba zetu, tena tunawaza wakati mwingine tuzungushe uzio vipi kwa Mungu??. Kama tu sisi tunapenda watu waziheshimu nyumba zetu vipi kwa Mungu?..

Na pia nyumba ya Mungu si jengo tu bali pia miili yetu, maandiko yanasema miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu (1Wakorintho 3:16, na 1Wakorintho 6:19). Ikiwa na maana kuwa pia miili yetu sio NJIA YA KILA MTU KUKATIZA!!!!.. (Maana yake si chombo cha zinaa wala kuchezewa).

1Wakorintho 6:15  “Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!

16  Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.

17  Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.

18  Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe”.

Itunze na kuiheshimu nyumba ya Mungu (Mwili wako mwenyewe pamoja na Jengo unalokusanyikia).

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

NI NANI ALIYEKUPA MAMLAKA HII UYATENDE HAYA?

TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?

Mlango uitwao “Mzuri” Unaozungumziwa katika Matendo 3:2 ndio upi?

Ni nani aliyemshawishi Daudi akawahesabu Israeli? Ni Mungu au shetani?

KAA MAJANGWANI.

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/06/27/wala-hakuacha-mtu-achukue-chombo-kati-ya-hekalu/