Maana ya Mithali 9:17 “Maji yaliyoibiwa ni matamu, Na mkate ulioliwa kwa siri hupendeza”

by Admin | 24 August 2023 08:46 pm08

SWALI: Je! mstari huu unaelewekaje? Mithali 9:17 “Maji yaliyoibiwa ni matamu, Na mkate ulioliwa kwa siri hupendeza”


JIBU: Mstari huo unamfunua mtu mwenye asili ya dhambi, jinsi vitu vilivyo kinyume na mapenzi ya Mungu vinavyoweza kupendeza mbele yake zaidi ya vile ambavyo ni sahihi kwake kuvifanya.

Kwamfano katika habari hiyo ukianzia vifungu vya juu utaona vinamweleza mwanamke kahaba, anavyowateka watu kuzini naye. Na mtu mjinga ataona ni sahihi kwenda kwake, lakini mwisho wake ni mbaya. Watu wengi wanaacha ndoa zao nakwenda kuzini nje! Kwasababu wanaona kile wanachokipata huko nje, kina uzuri kuliko kile walichokizoea ndani, wengine wanafanya uasherati, kwasababu wanaona wakingojea mpaka wakati wa ndoa, watakosa mambo mengi. Hao ndio wanaotembea katika usemi huo  “Maji yaliyoibiwa ni matamu, Na mkate ulioliwa kwa siri hupendeza”

Wengine wanaona wakitumia njia ya udanganyifu, ndio zitawafikisha katika malengo yao kwa haraka, kuliko njia za halali, hivyo hujiingiza katika wizi, na magendo.

Lakini ukizidi kusoma mstari unaofuata anasema..

.  Lakini huyo hajui ya kuwa wafu wamo humo; Ya kuwa wageni wake wamo chini kuzimuni.

Maana yake ni kuwa wote wafanyao mambo kama hayo, mwisho wao unakuwa ni kifo, na kuishia kuzimu kabisa. Dumu katika ndoa yako, kataa vya wengine, epuka mambo ya sirini. Yusufu hakukubali kuzini na mke wa boss wake. Lakini Daudi alidanganyika akazini na mke wa kijakazi wake, matokeo yake yakawa na yeye kunajisiwa wake zake vilevile, mtoto wake kufa, na ufalme wake kutikiswa na mwana wake mwenyewe aliyeitwa Absalomu, lakini zaidi sana kupoteza furaha ya wokovu kwa miaka mingi sana. Daudi alijutia makosa yake kwa muda mrefu sana.

Hivyo usipumbazwe na vivutio vyovyote vya dhambi vitakugharimu sana.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Nini maana ya Mithali 27:21  inaposema “mtu hujaribiwa kwa sifa zake?”

Fahamu maana ya Mithali 29:4 “Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; Bali yeye apokeaye rushwa huipindua.

Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)

Jicho ni  nini (Yakobo 3:11)

NI NINI BWANA ANATAZAMIA KILA TUNAPOSHIRIKI MEZA YAKE.

KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.

Ni lini na wapi Ibrahimu aliioona siku ya Bwana akashangilia?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/08/24/mithali-917-maji-yaliyoibiwa-ni-matamu/