Je ni nyaraka zipi mtume Paulo aliziandikia gerezani?

by Admin | 28 August 2023 08:46 pm08

Kati ya nyaraka kumi na tatu (13) alizoziandika mtume Paulo, Nne (4) kati ya hizo, aliziandika akiwa gerezani. Alipokuwa Rumi, ambapo maandiko yanatuonyesha  alipelekwa na kuwekwa chini ya kifungo maalumu ambacho aliruhusiwa watu kumtembelea lakini pia kuwahubiria injili akiwa katika kifungo hicho cha nyumba.

Matendo 28:16  “Tulipoingia Rumi Paulo alipewa ruhusa kukaa kwake mwenyewe pamoja na askari aliyemlinda…. 30  Akakaa muda wa miaka miwili mizima katika nyumba yake aliyokuwa ameipanga, akawakaribisha watu wote waliokuwa wakimwendea, 28.31  akihubiri habari za ufalme wa Mungu, na kuyafundisha mambo ya Bwana Yesu Kristo, kwa ujasiri mwingi, asikatazwe na mtu”.

Hivyo huko ndipo panaaminika aliandika nyaraka hizi nne. Ambazo ni

  1. Waefeso,
  2. Wafilipi,
  3. Wakolosai,
  4. Filemoni.

Sasa ni kwanini Nyaraka hizi na si nyingine?

Ni kwasababu ya habari za kufungwa kwake, alizozitaja katika nyaraka hizo; Ambazo zinaonyesha mazingira hayo alikuwa kifungoni.

Kwamfano ukisoma vifungu hivi, utaona,

Waefeso 3:1,4:1, Wafilipi 1:13, Wakolosai 4:3, Filemoni 1:10.

Je Ni nini cha kujifunza, katika vifungo vya mtume Paulo?

Yamkini Paulo alitamani awe huru kwa wakati ule ili aendelee kuihubiri injili kwa mataifa yote. Lakini hakujua mpango wa Mungu kwa nyaraka zake. Hakujua kuwa  Mungu atazihifadhi kwa mamia ya miaka, ili ziwe injili kwa vizazi vijavyo. Na matokeo yake ni kuwa nyaraka hizo zimehubiri injili kuliko hata wakati alipokuwa anazunguka mwenyewe kwenye mataifa akiwa huru.

Kwamfano mafunzo yaliyo katika kitabu cha Waefeso, yanatoa mwongozo mzuri kuanzia Viongozi wa kanisa, watakatifu hadi ngazi za kifamilia. Na jinsi gani mtakatifu anavyopaswa avae silaha za haki ili aweze kumpinga adui yake shetani (Waefeso 6:11-18)

Hii ni kuthibitisha maneno yale ya maandiko yanayosema kwamba injili  haifunguki.

2Timotheo 2:9  “Nami katika hiyo nimeteswa hata kufungwa kama mtenda mabaya; lakini neno la Mungu halifungwi

Na wewe pia ujionapo upo katika mazingira yanayokubana kuitangaza injili ya Bwana, usiwe na mawazo ya kukata tamaa, hapo hapo tazama upenyo wowote uutumie, kwasababu wewe umefungwa lakini sauti ya Mungu iliyo ndani yako, inauwezo wa kufika duniani kote, kwa vizazi vyote, hata kama umefungiwa kwenye chumba cha giza, namna gani, injili ya Kristo, inaangusha ngome popote.

Nyanyuka sasa, fanya jambo kwa Bwana, iamini nguvu ya msalaba.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Je! Mtume Paulo alikuwa ni Mrumi, Myahudi au raia wa Tarso?

Je Paulo na Petro walishindania nini? (Wagalatia 2:11).

Tarishi au Matarishi ni akina nani  kwenye biblia?

Je ni kweli Tumejengwa juu ya Mitume na Manabii? (Waefeso 2:20)

SIRI YA KUFANIKIWA KWA MTUME PAULO.

Paulo alikuwa na maana gani aliposema “nimeaminiwa uwakili”

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/08/28/nyaraka-zipi-mtume-paulo-aliziandikia-gerezani/