Maana ya Mithali 19:11 Busara ya mtu huiahirisha hasira yake.

by Admin | 18 September 2023 08:46 am09

Fahamu Maana ya;

Mithali 19:11 Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa.


Mstari huo unatufundisha mtu aliyejaa  “Busara” moyoni ni mtu wa namna gani..

Anaeleza ni Yule ambaye anaouwezo wa kughahiri hasira yake, na pia kupenda kusemehe makosa. Ambayo ndio sifa ya Mungu, Aliyonayo, soma;

Kutoka 34:6 Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;  7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.

Hivyo na sisi hatuna budi kutokuwa watu wa kukasirika haraka, mpaka ikaleta athari nje, kwamfano umeumizwa na mke/mume wako, tunapaswa tujifunze kuachilia mara moja, lakini pia kusamehe, sio kuweka kinyongo, au uchungu moyoni. Au mtu amefanya kosa la kukuudhi ambalo anastahili adhabu, si vema kuwa wepesi wa kuadhibu bali kuahirisha hasira hizo kwasababu Mungu naye anatusamehe makosa yetu, hatuadhibu kila kosa.

Bwana alisema kusamehe kwetu hakupaswi kuwe na ukomo, alitumia lugha ya hata ‘saba mara sabini’ kwa siku(Mathayo 18:22). Kuonyesha kuwa kusamehe kwetu kunapaswa kuwe endelevu. Ili  tufikie hatua ya Kuona ‘fahari’ katika uwezo wa kusamehe, zaidi ya kuona fahari katika uwezo wa ‘kupata vitu’. Yaani tuhesabu ni watu wangapi tumewasamehe, hapo ndio iwe furaha yetu. Na kwamba tuipime busara yetu kwa kiwango cha kuiharisha hasira zaidi ya uwezo wa ‘kuwa na maneno mengi ya hekima’.

Bwana atusaidie.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

NIFANYE NINI NIWEZE KUDHIBITI HASIRA?

Mungu anatufundisha kusamehe mara saba sabini, ila Kwanini yeye hakumsamehe Adamu alipoasi?

TAFUTA HEKIMA, MAARIFA, UFAHAMU NA BUSARA.

BWANA SI MWEPESI WA HASIRA, LAKINI BWANA NI MWINGI WA HASIRA.

KWANINI TUWE WENYE BUSARA KAMA NYOKA?

SIKU YA HASIRA YA BWANA.

Wivu ni nini na kuna aina ngapi za Wivu?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/09/18/maana-ya-mithali-1911-busara-ya-mtu-huiahirisha-hasira-yake/