Mungu anatufundisha kusamehe mara saba sabini, ila Kwanini yeye hakumsamehe Adamu alipoasi?.

Mungu anatufundisha kusamehe mara saba sabini, ila Kwanini yeye hakumsamehe Adamu alipoasi?.

Jibu:  Adhabu iliyompata Adamu na Hawa, haikutokana na hasira ya Mungu!.. bali ilikuwa ni matokeo ya walichokifanya.

Hebu tafakari mfano huu…. “unamwonya mtu asile kitu Fulani kwasababu unajua madhara ya hicho kitu kwamba endapo akikila basi kitamsababishia apofuke macho na hata kufa huko baadaye, kwasababu kina sumu mbaya ndani yake”.

Lakini huyo mtu ambaye ulimtahadharisha asifanye hivyo, hakukusikiliza wewe badala yake akaenda kula hicho kitu ambacho madhara yake ni kupofuka macho na hata kufa. Na siku alipokula wewe ukajua na kwa huzuni  ukaenda kumwuliza kwanini ulikula?..yeye akatoa sababu zake anazozijua yeye, kisha wewe ukamwambia kwamba.. “kwasababu umekula hicho kitu basi macho yako yatapofuka siku si nyingi  na pia utakufa!.

Sasa swali ni je!, kwa wewe kumwambia hivyo kwamba “atapofuka macho na kufa” je umemhukumu, au umemwambia tu mambo yatakayompata kutokana na kitu alichokifanya?.. Au je kwa wewe kumwambia hivyo, kuna uhusiano wowote wa wewe kumsamehe au kutomsamehe?.. Jibu ni la!, wewe umemwambia tu madhara ya alichokifanya na kuanzia pale utaanza kumhurumia na kumtafutia suluhisho ili ile sumu iliyoingia ndani yake iweze kutoka….

Ndicho kilichotokea pale Edeni, adhabu aliyoipata Adamu na Hawa ni kwasababu ya matokeo ya walichokifanya na si kwasababu ya hasira ya Mungu!!. Na Mungu kwa huruma zake, kuanzia pale ndio akaanza mpango wa kumponya mwanadamu kwa madhara aliyoyaingiza katika maisha yake.

Na ndipo akapata mpango bora, ambao huo utaondoa moja kwa moja madhara yaliyoingia ndani ya Mwanadamu, na mpango huo si mwingine zaidi ya ule wa kumtoa Mwanawe wa pekee YESU KRISTO, aje kufa kwa ajili ya dhambi zetu, na kutukomboa, kuanzia hapo Mungu akamtoa Adamu pale Edeni ili amweke katika mpango mpya na ulio kamili, utakaomkamilisha.

Yesu Kristo pekee ndiye tiba ya KIFO  ambacho kilikuwa kimeingia katika maisha yetu tangu siku ile wazazi wetu, Adamu na Hawa walipoasi.

Yohana 11:25  “Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi”

Yesu Kristo ndiye tiba ya mambo yote, ndiye suluhisho la matatizo yote ya maisha, na pasipo yeye sisi hatuwezi kufanya lolote.

Yohana 15:5  “Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote”.

Na nje ya Yesu Kristo hapana wokovu..

Matendo 4:12 “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo”

Je! Umempokea Yesu katika maisha yako?.. je umebatizwa katika ubatizo sahihi? Je umepokea Roho Mtakatifu wa kweli?. Kama bado unasubiri nini?

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

JUMA LA SABINI (70) LA DANIELI

KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

JINA LAKO NI LA NANI?

BASI TUENDELEE KUMJUA MUNGU,NAYE ATATUJILIA KAMA MVUA YA VULI.

KWANINI TUNAPASWA KWENDA KUIHUBIRI INJILI KWA UJASIRI WOTE?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Prince
Prince
1 year ago

Adamu alijikabizi mwenyewe kwa kifo,kwanza kama hangeonja kwa kifo shetani angeonekana kama msema kweli. Lapili composition ya mti waliokatazwa ilikuwa kuyajuwa mema na mabaya baada ya ujuzi huwo kukawa kifo kuvuna ulioyapanda sijaona shida hata kamwe.

Anonymous
Anonymous
1 year ago

Huu Ni ufunuo mkubwa
Nimeelewa vizuri sana
Asante roho Mtakatifu.