by Admin | 9 October 2023 08:46 pm10
Mawaa ni nini? Mawaa ni dosari au kasoro iliyo katika kitu, ambayo inapelekea kukifanya kitu hicho kisifae tena, au kikose vigezo.
Kwamfano mtu ambaye ana sifa ya kuwa na uso mzuri halafu, kukatokea jipu shavuni. hapo ni sawa na kusema ana-mawaa. Jipu lile limeuharibu uzuri wake.
Au ukinunua bati la kuwekeza kwenye nyumba yako, halafu ukaona tobo katikati ya bati hilo, tayari lina mawaa, halifai kwa ujenzi. Au shati jeupe halafu likawa na doa dogo jeusi, huo ni mfano wa mawaa, halifai kwa kuvalika.
Vilevile rohoni na sisi pia hatupaswi kuonekana na mawaa ya aina yoyote, Kwamfano katika vifungu hivi; Mungu anatarajia kanisa lake alilolikomboa kutoka katika dhambi lisionekane na mawaa (dosari yoyote) ndani yake
Wakolosai 1:21 “Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa; 22 katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama”
Hivyo wewe kama mkristo uliyeokoka, ni lazima ujue kuwa una wajibu wa kuishi maisha ya utakatifu na ukamilifu, usiseme nimeokolewa kwa neema Yesu alishayamaliza yote, Hivyo unaenda kama utakakavyo, anaitenda kazi ya Mungu huku unaishi na mke/mume ambaye si wako. Wewe una mawaa, na hivyo mbingu huwezi kuiona.
Au unatoa zaka, unaimba kwaya, ni kiongozi wa vijana, na huku unatazama picha za ngono mtandaoni, hapo una-mawaa, Unafunga na kusali, unadumu hekaluni usiku na mchana na huku unakula rushwa kazini kwako. Hapo ndugu una-mawaa.
Hivyo hatuna budi kuwa kanisa la Kristo kwelikweli Bwana analolitazamia lisilo na mawaa wala lawama, wala kunyanzi. Ndivyo tutakavyopokewa kuingia katika uzima wa milele.
Neno hilo utalipata katika vifungu hivi
1Timotheo 6:13 “Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato, 14 kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo”.
Yohana 1:27 “Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa”.
Soma pia
Waebrania 9:14, 2Petro 2:13
Bwana akubariki.
Je! Umeokoka, kama la! Ni nini unachosubiria mpaka sasa, una habari kuwa parapanda inakaribia kulia, Yesu anarudi? Dalili zote zimeshatimia? Fikiri akikukuta katika hali hiyo utamweleza nini? Angali ukweli umeshaujua? Embu tubu leo dhambi zako, mgeukie Kristo, azioshe, akupe uzima wa milele bure.
Ikiwa upo tayari kumpokea Yesu leo akupe uzima wa milele bure, basi fungua hapa ili uweze kupata mwongozo wa sala hiyo. >>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Mikono iliyotakata ni mikono ya namna gani? (1Timotheo 2:8).
TOA SADAKA ISIYO NA KASORO KWA BWANA.
FUNDISHO KUU LA NEEMA YA MUNGU KWETU.
USIPOWATAMBUA YANE NA YAMBRE, KATIKA KANISA LA KRISTO, UJUE UMEPOTEA.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/10/09/mawaa-ni-nini-kama-tunavyosoma-katika-biblia/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.