by Admin | 5 February 2024 08:46 pm02
Swali: Mafuta Mabichi yapoje, na yanafunua nini kiroho?
Jibu: Tureje..
Zaburi 92:10 “Bali pembe yangu umeiinua kama pembe ya nyati, Nimepakwa MAFUTA MABICHI”.
Mafuta mabichi yanayozungumziwa hapo si mafuta ambayo hayajapitishwa kwenye moto yakaiva na kuchemka… La!.. bali ni mafuta yaliyo mapya (yaani freshi) ambayo yayajakaa muda mrefu.
Nyakati za biblia na hata sasa wayahudi wanatumia mafuta ya Mizeituni kwa matumizi ya chakula na ibada.
Asilimia kubwa ya vyakula vya wayahudi na baadhi ya jamii za mashariki ya kati wanatumia mafuta ya Mizeituni kama kiungo cha mboga, na wakati jamii nyingine mbali na hizo wanatumia mafuta ya Alizeti au mimea mingine katika mapishi.
Chakula kilichoandaliwa kwa mafuta mabichi (yaani mapya) ya Mizeituni kinakuwa ni kitamu na chenye ladha… utaona hata ile MANA jangwani, ladha yake ilifananishwa na ladha ya mafuta mapya. (soma Hesabu 8:11).
Vile vile katika shughuli za kiibada, pale ambapo mtu anatawazwa kuwa mfalme basi alipakwa Mafuta haya ya mizeituni kama ishara ya kuruhusiwa kuchukua madaraka hayo,
1Samweli 9:15 “Basi Bwana alikuwa amemfunulia Samweli, siku moja kabla Sauli hajamwendea, akisema,
16 Kesho, wakati kama huu, nitakuletea mtu kutoka nchi ya Benyamini, NAWE MTIE MAFUTA ili awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, naye atawaokoa watu wangu na mikono ya Wafilisti; maana nimewaangalia watu wangu, kwa sababu kilio chao kimenifikilia”
Soma pia1Wafalme 16:12, 1Wafalme 1:34, na 1Wafalme 19:15-16 utaona jambo hilo hilo..
Vile vile makuhani walitiwa mafuta kama ishara ya kuchaguliwa na Mungu kutumika katika nyumba yake.
Zaburi 133:2 “Ni kama mafuta mazuri kichwani, Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake”.
Sasa ilikuwa ni heshima na jambo jema kutiwa mafuta ambayo ni mapya.. Kwani Mafuta ya Mizetuni kama yamehifadhiwa vizuri yanadumu kwa miaka 2 tu, ukipita huo muda yanaharibika na kutoa harufu nyingine. Kwahiyo chakula kilichoandaliwa kwa mafuta yaliyokaa kinakuwa hakina ladha na pia kinatoa harufu mbaya…
Vile vile mtu aliyepakwa mafuta yaliyokaa sana au kuharibika si jambo la utukufu… lakini mafuta mabichi ilikuwa ni jambo la utukufu kwasababu ni freshi.
Sasa mafuta mabichi (yaani mapya) na yale yaliyokaa (yaani ya zamani) yanawakilisha nini sasa kiroho?..
Mafuta yanamwakilisha ROHO MTAKATIFU. Hivyo mafuta yaliyokaa (ya zamani) yanawakilisha utendaji kazi wa Roho Mtakatifu katika Agano la kale… na Mafuta mapya ni utendaji wa ROHO MTAKATIFU katika agano jipya.
Na sisi tunayahitaji mafuta mabichi katika UTUMISHI WETU, na si yale yaliyokaa… kwasababu hayatatufaa sana..
Mafuta mapya yanatufundisha kuwa wakamilifu zaidi na katika kuyafanya mapenzi ya Mungu..kuliko yale ya zamani.
Mathayo 5:27 “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
29 Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
30 Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
31 Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;
32 lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
33 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;
34 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu”.
Je umempokea YESU KRISTO, aliye mjumbe wa Agano jipya?, kumbuka huwezi kuwa na ROHO MTAKATIFU, kama YESU KRISTO hayupo ndani ya maisha yako.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza
Je tunaruhusiwa kujipaka mafuta au kujipulizia marashi?
MAANA YA KRISTO/ JINA KRISTO LINA MAANA GANI?
Je! Ni sahihi kutumia maji ya upako,katika kufanya maombezi?
Mfano wa wanawali kumi(Mathayo 25), unaelewekaje?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/02/05/mafuta-mabichi-ni-mafuta-ya-aina-ganizaburi-9210/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.