by Devis Julius | 7 May 2024 08:46 am05
Malaika watakatifu waliopo mbinguni, wanaompa Mungu utukufu usiku na mchana, ni WAALIMU wazuri wa SIFA, na KWAYA kwetu!.. Hao wamewekwa ili kutufundisha sisi namna ya kumwimbia Mungu katika viwango vya kimbinguni. Huenda wasitufundishe namna ya kuhubiri, lakini katika kusifa, wanayo mafunzo kwaajili yetu.
> FUNZO LA KWANZA: Wanajisitiri!.
Malaika wa Sifa, (yaani Maserafi na Makerubi) sehemu kubwa ya mbawa walizopewa wanazitumia kujisitiri.. na wanajisitiri kuanzia kichwani mpaka miguuni…wanaposimama mbele za MUNGU KUMPA UTUKUFU..
Isaya 6:1“Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.
2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; KWA MAWILI ALIFUNIKA USO WAKE, NA KWA MAWILI ALIFUNIKA MIGUU YAKE, NA KWA MAWILI ALIRUKA”
Ikimaanisha kuwa kabla ya kupeleka sifa mbele za MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi, kigezo cha kwanza ni KUJISITIRI!!. Lakini leo hii watu watasimama mbele za MUNGU kumwabudu na kumsifu, vifua vikiwa wazi, mgongo ukiwa wazi, mapaja yakiwa wazi, mauongo yakiwa wazi..na wanawake vichwa vikiwa wazi..
Swali la kujiuliza je ni nani amewafundisha hayo????.. kuabudu, na kusifu wakiwa nusu uchi, je wamefundishwa na nani?..na Malaika watakatifu wanaomwimbia Mungu au nani?..jibu rahisi ni kwamba wamefundishwa na shetani, na wanayempa sifa si MUNGU wa Mbinguni bali ni shetani wa duniani na kuzimu!.
> FUNZO LA PILI: Wanahubiri utakatifu.
Malaika wa Sifa mbinguni, (Maserafi na Makerubi) wanaonekana “wakiitana” (maana yake wakiambiana) Mtakatifu…Mtakatifu… Mtakatifu…
Na zingatia hili: si kwamba walikuwa wanamwambia Mungu, kwamba ni Mtakatifu!!.. la! Walikuwa wanaambiana wao!.. maana yake wanakumbushana wao kwa wao!, wanajitangazia na kuwatangazia wengine kuwa Bwana ni mtakatifu, hivyo “kila mmoja adumu katika huo utakatifu”..kwasababu Mungu ni mtakatifu na hakai katika uchafu..
Ufunuo 6:3 “Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake”.
Huo ndio wimbo wa MALAIKA mbinguni usiku na mchana!!… UTAKATIFU, UTAKATIFU, UTAKATIFU…
Na ndizo zinazopasa kuwa NYIMBO za watakatifu waliopo duniani… Sio kumwambia Mungu MTAKATIFU!!, Kana kwamba tunampa taarifa asiyoijua!!… yeye tayari ni mtakatifu na atabaki kuwa hivyo daima… bali tunapaswa tujikumbushe na kujitangazia sisi kuwa MUNGU NI MTAKATIFU, NA HIVYO TUZIDI KUJITAKASA… SIFA ZA NAMNA HIYO NDIZO ZINAZOMPENDEZA MUNGU!!..
Na sio mtu unaimba huku una mambo mengine ya kando kando!!.. sio unaimba huku unaishi na mke/mume ambaye si wako, sio unaabudu na kuimba kwaya huku ni mzinzi na mwabudu sanamu na unafanya mambo mengine yaliyo machukizo.
Neno la Mungu linasema pasipo huo utakatifu, hakuna mtu atakayemwona MUNGU…
Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”.
Nyimbo au Mahubiri yasiyohubiri utakatifu ni “Ngojera za ibilisi:”.. zinazotoa thawabu za kishetani, haihitaji kuwa mchawi ndio uwe wa shetani… kumwimbia tu ibilisi tayari wewe ni wake!..kuhubiri huku unasifia na kuzitenda dhambi wewe ni wa shetani.
Kama una karama ya uimbaji acha usanii, kazi ya MUNGU lebo!!, si brand! Ni huduma..kwahiyo usijitengeneze na kuwa mfano wa wasanii wa kidunia ambao wamepewa lebo na brandy na shetani ili wafanye mapenzi yake. (Hao wanahitaji kusaidiwa waokoke, na sio kuigwa).
Ukiamua kumwimbia MTAKATIFU aliye juu, VAA NGUO KAMILI!!!, HUBIRI UTAKATIFU, ISHI UTAKATIFU..
BWANA ATUSAIDIE!
Maran atha!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
NIONDOLEENI KELELE ZA NYIMBO ZENU (Amosi 5:23)
MAKABURI YAKAFUNUKA; IKAINUKA MIILI MINGI YA WATAKATIFU WALIOLALA;
NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.
TAFUTA KWA BIDII KUWA MTAKATIFU.
UTUKUFU WA MUNGU NI KITU GANI?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/05/07/malaika-ni-walimu-wa-sifa-kwetu-tujifunze-kwao/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.