NIONDOLEENI KELELE ZA NYIMBO ZENU (Amosi 5:23)

NIONDOLEENI KELELE ZA NYIMBO ZENU (Amosi 5:23)

Amosi 5:23 “Niondoleeni KELELE ZA NYIMBO ZENU; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu”.

Je ni kwamba Mungu wetu hapendezwi na nyimbo tunazomwimbia??

Jibu ni la! Yeye anapendezwa na nyimbo na tena anaketi katika SIFA.

Zaburi 22:3 “Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli”.

Lakini kwanini aseme “niondoleeni kelele za nyimbo zenu?”… Ni wazi kuwa kuna nyimbo ambazo kwa Mungu ni kama kelele.

Sasa ni aina gani za nyimbo ambazo kwa Mungu ni kelele?.

1. NYIMBO ZA UNAFIKI.

Nyimbo za kinafiki ni zile mtu anazoimba kwa kupaza sauti, lakini maisha yake hayaendani na kile anachokiimba, kuanzia, uzungumzaji, uvaaji, utendaji na maisha yake yake siri. Mtu mwenye tabia hiyo halafu akasimama na kuimba nyimbo za kumtukuza Mungu, iwe ni nyimbo alizozitunga yeye, au za mwingine, mtu huyo anapiga kelele mbele za Mungu na hivyo anafanya dhambi.

2. NYIMBO ZENYE MIDUNDO YA KIDUNIA.

Kuna nyimbo ambazo zinafanana sana na za kidunia, kiasi kwamba mtu akisikiliza anafananisha na nyimbo Fulani ya kidunia ambayo alishawahi kuisikia mahali fulani. Nyimbo za namna hiyo ni kelele, na si kelele tu, bali pia ni machukizo… mfano wa hizo ni nyimbo aina ya rege, rap, pop, taarabu na nyingine zinazofanana na hizo, Nyimbo za namna hii zinajulikana kama nyimbo za upuuzi (Amosi 6:5). Hivyo wakristo hatupaswi kutumia midundo hiyo kumwimbia MUNGU.

3. NYIMBO ZINAZOSHIRIKISHA WASANII WA KIDUNIA.

Wasanii wa kidunia ni watu wanaoimba nyimbo za zinazotukuza na kusifia mambo ya ulimwengu huu, na ulimwengu upo chini ya shetani, sasa mtu anayewashirikisha waimbaji hao wa kidunia, waliozoea kumwimbia shetani, kisha wakapewa mashairi ya kumsifu Mungu pamoja na watu wa kiMungu, hizo ni kelele na machukizo mbele za Mungu, haijalishi nyimbo hiyo itakuwa na beti nzuri kiasi gani na ujumbe mzuri kiasi gani, au zenye kumsifia MUNGU kwa kiasi gani,  bado ni kelele mbele za Mungu na hazina matunda yoyote.

Nyimbo zenye kumtukuza Mungu ni zile zilizobeba ushuhuda wa Neno kuanzia kwa MWIMBAJI, beti na mdundo. Na zinapoimbwa zinamtukuza Mungu na kuwabariki wasikiao.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MAONO YA NABII AMOSI.

WAKINYAMAZA HAWA, MAWE YATAPIGA KELELE.

Nini maana ya Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu?

Fahamu maana 1Wakorintho 14:20  “Ndugu zangu msiwe watoto katika akili zenu;

LAKINI USIKU WA MANANE, PAKAWA NA KELELE.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Betty
Betty
4 months ago

Amen…naomba link,hii inaniambia its invalid.
Nimebarikiwa na masomo
Nilikuwa natafuta maana Neno HAKI,nikakuta maelezo mazuri yaliyonibariko