Ni kelele gani zinazozungumziwa hapo katika Waefeso 4:31.

Ni kelele gani zinazozungumziwa hapo katika Waefeso 4:31.

Waefeso 4:31 “Uchungu wote na ghadhabu na hasira NA KELELE na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya”.

Kelele zinazozungumziwa hapo ni kelele za  “Maneno” , kelele za “Maombi” na kelele za “Nyimbo”

1.KELELE ZA MANENO.

Hizo ni zile kelele zinazotokana na malumbano yasiyo na msingi wa kiroho, au mashindano ya maneno. Watu wagomvi huwa wana kelele, watu wabishi huwa wana kelele, watu wakorofi huwa wana kelele, na yote ni matunda ya dhambi ambayo hayapaswi kuwa ndani ya mtu aliyokoka.

2. KELELE ZA MAOMBI

una mambo ambayo mtu akiomba ni kelele mbele za Mungu, na mfano wa hayo ni yale yasiyotokana na Neno, maana yake mtu anaomba kitu kwa tamaa zake na ambacho si mapenzi ya Mungu, na tena anatumia sauti kubwa, (maombi kama haya ni kelele mbele za Mungu na pia hayana majibu.)

Yakobo 4:3 “Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu”.

3. KELELE ZA NYIMBO.

Amosi 5:23 “NIONDOLEENI KELELE za nyimbo zenu; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu”.

Si nyimbo zote ni kelele mbele za Mungu, zipo zinazomtukuza Mungu na wanaoimba pia wanamtukuza Mungu.. Lakini zipo nyimbo ambazo hazimtukuzi Mungu ingawa zina majina na sifa za kumtukuza Mungu,

Vile vile zipo nyimbo ambazo zina maneno mazuri ya kumtukuza Mungu, lakini wanaoimba ni watu wasio na mahusiano yoyote na MUNGU, nyimbo za namna hiyo ni KELELE mbele za MUNGU.

Vile vile nyimbo zenye midundo ya kidunia, lakini zina maneno ya kibiblia, hizo nazo ni kelele, na si kelele tu bali pia ni machukizo.

Jihadhari na kelele.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NIONDOLEENI KELELE ZA NYIMBO ZENU (Amosi 5:23)

WAKINYAMAZA HAWA, MAWE YATAPIGA KELELE.

Nini maana ya Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu?

LAKINI USIKU WA MANANE, PAKAWA NA KELELE.

Je ni kweli Tumejengwa juu ya Mitume na Manabii? (Waefeso 2:20)

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments