Nardo ni nini? (Yohana 12:3)

by Admin | 7 May 2024 08:46 am05

Jibu: Turejee..

Yohana 12:3 “Basi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya NARDO SAFI yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu.

4  Basi Yuda Iskariote, mmojawapo wa wanafunzi wake, ambaye ndiye atakaye kumsaliti, akasema,

5  Mbona marhamu hii haikuuzwa kwa DINARI MIA TATU, wakapewa maskini”

“Nardo” ni jamii ya mmea mdogo ujulikanao kama “Nardostachys”. Mmea huu hutoa maua madogo ya rangi ya “Pinki” (Tazama picha juu), na vijimatunda vidogo vyeusi ambavyo ndivyo chanzo cha mafuta aina ya “Nardo” yanayotumika kutengenezea madawa ya asili pamoja na marhamu (yaani Perfumes/pafyumu) iliyo ya gharama kubwa kuliko nyingine nyingi.

marhamu ya Nardo

Pafyumu iliyotengenezwa kwa “Nardo”, ilikuwa ni ya gharama kubwa na hata sasa ni ya gharama kubwa kutokana na upatikanani wa mimea hiyo.

Mimea ya Nardostachy, inapatikana katika safu za milima ya Himalaya, iliyopo nchini Nepali, na sehemu chache za “nchi ya India” pamoja na “Uchina”.  Na inamea kuanzia kwenye kimo cha Mita 3,000 mpaka mita 5,000 kutoka katika usawa wa bahari (Mita 5,000 ni karibia na kimo cha Mlima Kilimanjaro).. Hivyo upatikanaji wake ni mgumu sana, kutokana na sehemu chache unazomea na kimo unapopatikana!.

Kutokana na sababu hizo, ndizo zinazoifanya Marhamu ya Nardo kuwa ya gharama. Mpaka hapo tutakuwa tumeshafahamu kuwa ile Marhamu yule mwanamke aliyompaka Bwana iliagizwa kutoka mbali sana (maana yake nje ya Israeli) na ilikuwa ya gharama sana… Dinari 300 ni sawa na shilingi Milioni 6 za kitanzania.

Mistari mingine inayozungumzia Marhamu ya Nardo ni pamoja na Wimbo ulio bora 1:12, na 4:13-14

Sasa kufahamu kwa urefu ni nini tunajifunza kupitia tukio la mwanamke yule kukivunja kile kibweta fungua hapa >>AKAKIVUNJA KIBWETA AKAIMIMINA KICHWANI PAKE.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

AKAZIDI KUENDELEA KATIKA HEKIMA NA KIMO.

Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?

Biblia inamaana gani iliposema “Dhambi ilipozidi, Neema ilizidi kuwa nyingi Zaidi”.

GHARAMA YA UFALME WA MBINGUNI.

SI KILA KILICHO HALALI KINAFAA.

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/05/07/nardo-ni-nini-yohana-123/