AKAKIVUNJA KIBWETA AKAIMIMINA KICHWANI PAKE.

AKAKIVUNJA KIBWETA AKAIMIMINA KICHWANI PAKE.

Yesu alipokuwa nyumbani kwa Yule Simoni mkoma, alitokea mwanamke mmoja na kufanya jambo ambalo lilizua malalamika mengi sana kwa wale waliokuwa pale, kama tunavyoifahamu habari, mwanamke Yule alikuwa na kibweta (kijagi), kilichojaa marhamu(pafyumu), na thamani yake ilikuwa ni kubwa sana, ni sawa na pesa za kitanzania, milioni 6, Mshahara wa mwaka wa mtu anayelipwa vizuri.

Lakini maandiko yanatuambia, mwanamke Yule hakufungua tu kile kifuniko cha kibweta ili aimimine pafyumu  kichwani pa Yesu hapana, bali “ alikivunja kabisa”, kwa namna nyingine aliharibifu kijagi hicho, kuonyesha kuwa hii pafyumu haitatumiwa tena sehemu nyingine yoyote, itaishia yote hapa, na hilo ndio lililowafanya wale watu waliokuwa pale walalamike, na kusema upotevu wote huu wa nini?..

Anaimwaga pafyumu yote kama maji, lakini Yule mwanamke hakujali, aliimaliza yote, mpaka nyumba yote ikiwa inanuka pafyumu.

Tusome kidogo..

Marko 14:3  “Naye alipokuwapo Bethania, nyumbani mwa Simoni mkoma, ameketi chakulani, alikuja mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya nardo safi ya thamani nyingi; akakivunja kibweta akaimimina kichwani pake.

4  Palikuwa na watu waliochukizwa katika nafsi zao wakisema, Kwani kupoteza marhamu namna hii? 5  Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa dinari mia tatu na kuzidi, wakapewa maskini. Wakamnung’unikia sana yule mwanamke.

6  Yesu akasema, Mwacheni; mbona mnamtaabisha? Amenitendea kazi njema;7  maana sikuzote mnao maskini pamoja nanyi, na kila mpendapo mwaweza kuwatendea mema; lakini mimi hamnami sikuzote.

8  Ametenda alivyoweza; ametangulia kuupaka mwili wangu marhamu kwa ajili ya maziko. 9  Amin, nawaambia, Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake”

Nachotaka tuone juu ya habari hii, ni kwamba tunaweza kudhani kuwa ni huyu mwanamke tu, ndiye aliyekuwa na kibweta kile cha thamani,..Ukweli ni kwamba wale wote walikuwa na vibweta vyao, isipokuwa tu katika maumbile tofuati.. kuna mahali walivivunja au watavivunja, na kutumia kwa ajili ya vitu watakavyoviona vya thamani..

Hata sasa, kila mmoja wetu anachokibweta chake, ni suala tu la muda.. Utajiuliza, unamtazama msanii Fulani kwenye tv, anamwaga pesa, na kuwapa makahaba, au ananunua gari la kifahari, halafu wewe unaanza kulalamika na kusema upotevu wote huo wa nini, si ni heri angewasaidia maskini, kuliko kutumia kwa anasa.. Usimlaumu kibweta chake ndio amekivunjia hapo.

Leo hii, utaona, mtu kumtolea Mungu, au kusapoti huduma ambazo zinamsaidia kiroho ni ngumu, hata halifikirii.. Lakini mwanawe akitaka kwenda shule, atahangaika kila mahali kumtafutia ada, au akiumwa, anahitaji kwenda kutibiwa India, atauza, gari mpaka shamba, kusudi kwamba aokoe maisha ya mwanawe..Hicho ni kibweta chake amekivunja.

Kuonyesha kuwa kumbe anaweza kupoteza chochote cha thamani kwa ajili ya kitu cha muhimu. Tujiulize, Utasema mimi sina kibweta cha thamani..Ukweli ni kwamba unacho, bado hujaona mahali pa muhimu pa kukimwaga. Wakati utafika tu,.

Tujiulize, vipi kuhusu Mungu wetu..Yesu wetu aliyetuokoa, twaweza kudhubutu kuwa kama huyu mwanamke? Ambaye alikivunjia kwa Bwana?..Hakujua kwa kufanya vile, injili yake itahubiriwa kizazi baada ya kizazi.. Na Yesu ni yeye Yule jana na leo na hata milele.. Kama alimfanyia huyu, anaweza pia akakufanyia na wewe, kwa namna yako..Lakini ni lazima ukivunje kibweta chako kwake..Kumbuka Bwana anasema maskini manao siku zote,..Unafurahi vipi, Bwana akuhudumie, halafu wewe umuhudumii?

Tafakari.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

NI NANI ATAKAYEUCHUKUA MSALABA WA YESU?

Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?

USICHELEWE KUMPAKA BWANA MARHAMU!

YESU HAYUPO KATIKA MAZINGIRA YALEYALE TU SIKUZOTE, USIJISAHAU.

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
amen
amen
1 year ago

Utukufu kwa Yesu