Kwanini Mungu aliupenda ulimwengu?

by Admin | 4 July 2024 08:46 pm07

Mungu aliupenda ulimwengu kwasababu asili yake upendo, Maandiko yanasema yeye ni UPENDO.

1Yohana 4:16  Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.

Lakini ifahamike kuwa aliposema ameupenda ulimwengu haimaanishi kuwa amependa kila kitu ulimwenguni, ikiwemo mifumo ya ulimwengu huu, hapana, kazi nyingi za ulimwengu ni mbovu, na hivyo hawezi kuzipenda, tena alizikemea (Yohana 7:7), bali aliwapenda walio-ulimwenguni (yaani sisi wanadamu). Bila kujali jinsia zetu, rangi zetu, jamii zetu, mataifa yetu, waovu, na wema, wote alitupenda sawa.

Ni upendo uliodhihirika katika hali yetu ya kupotea. Mahali ambapo tulikuwa hatuna tumaini lolote, hatuna uzima wowote wa milele ndani yetu, tumeteswa na ibilisi, yeye mwenyewe kwa mapenzi yake akatuhurumia, ndipo akatujia tena ili kutuokoa katika hali ya kifo na mauti tuliyokuwa nayo bure.

Na hivyo hakutupenda kwa mdogo tu, bali aliingia gharama. Na gharama yenyewe ni kumtoa mwanawe wa pekee Yesu Kristo, kuja katika mwili wa kibinadamu ili afe kama fidia ya dhambi zetu, ili sisi tupone kwa kifo chake yeye. Tupokee uzima wa milele.

Maana yake mtu yeyote ambaye ataukubali wokovu huo, ulioletwa kwa kufa na kufufuka kwake, basi uzima wa milele unaingia ndani yake. Ndio maana ya hilo andiko;

Yohana 3:16  Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Lakini ijapokuwa uzima umeletwa kwetu bure kwa gharama kubwa, wapo wengine hawaukubali, wakidhani kuwa wataweza kuushinda huu ulimwengu kwa nguvu zao, au kwa dini zao, au kwa matendo yao wenyewe.

Yohana 3:19  Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.

Je! Umeupokea uzima huu wa milele?. Ikiwa bado basi fungua moyo wako sasa, mwamini Yesu, mpokee kama ‘Bwana’ kwako, umfuate kwa moyo wako wote, uokoke, dunia hii ni ya kitambo tu, vilevile kesho yako huijui kama utakuwa hai au maiti. Ikiwa upo tayari kuokoka leo, basi fungua hapa kwa msaada wa mwongozo wa sala ya wokovu >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Ulimwengu wa Roho ni nini? Na mtu anawezaje kuwa wa rohoni?

NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.

(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.

MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/07/04/kwanini-mungu-aliupenda-ulimwengu/