Kuota unavua samaki, kunamaanisha nini?

by Admin | 13 December 2024 08:46 am12

Jiunge  >>>  WHATSAPP  <<< kwa mafundisho.

Ikiwa ndoto hii inakujia mara kwa mara, Au imekujia kwa uzito fulani, basi hwenda Mungu anasema na wewe rohoni. Ndoto hii inaweza kuja katika maumbile mengi. Wengine wanaota wakivua samaki kwa mikono, wengine kwa ndoano, wengine kwa wavu, wengine wakivua samaki wadogo/wakubwa. n.k. Kwa vyovyote vile maadamu ni kuvua basi maudhui yake ni moja.

Kiroho, uvuvi humaanisha kuwavuta watu kwa Kristo kwa kazi ya injili.

Yesu alipokutana na wale thenashara, wengi wa hao walikuwa wakifanya kazi ya uvuvi. Hivyo hiyo ilikuwa ni njia rahisi ya Yesu kuwaeleza kusudi lake timilifu juu ya hicho wanachokifanya.

Ndio maana siku ile alipomfanyia Petro muujiza ule wa kupata samaki wengi, baada ya kutaabika usiku kucha bila kupata chochote, Yesu alimwambia usiogope tangu sasa utakuwa mvuvi wa watu.

Luka 5:10

[10]na kadhalika Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, waliokuwa washirika wa Simoni.Yesu akamwambia Simoni, Usiogope, tangu sasa utakuwa ukivua watu.

Kuonyesha kuwa uvuvi wa nje, ni ufunuo wa uvuvi wa rohoni.

Utaona hata huduma ya malaika siku ile  ya mwisho ya kuwatenga watu waovu na wema inafananishwa na huduma ya uvuvi wa samaki.

Mathayo 13:47-50

[47]Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna;

[48]hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa.

[49]Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki,

[50]na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Hivyo kwa namna moja au nyingine ikiwa umeokoka  basi Bwana anakutaka uhihubiri injili, kwa wengine kwasababu wakati huo umefika kufanya hivyo. Usiangalie uzoefu wako, kwasababu kumshuhudia Kristo hakutegemei uzoefu bali nia ya upendo. Na Mungu mwenyewe ameahidi kukusaidia kunena uwashuhudiapo watu.

Lakini kama hujaokoka, basi Yesu anakuita na anaona wito wako kutokea mbali, kwamba ukawahubirie wengine. Hivyo ni wajibu wako kumtii na kuupokea wokovu ili kusudi hilo alilolipanga ndani yako alifanikishe juu yako, haijalishi ndoto hii umeota mtu wa dini gani au imani gani, iwe mwislamu, mhindu, mshirikina. Maana umeota msalaba. Ujue Kristo anakuita akuokoe.

Ikiwa upo tayari sasa kumpokea Yesu basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala hiyo.

>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UVUVI BORA HAUCHAGUI, CHA KUVUA.

TENGENEZA  NYAVU ZAKO, OSHA NYAVU ZAKO.

CHAMBO ILIYO BORA.

Kuota unakimbizwa.

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/12/13/kuota-unavua-samaki/