CHAMBO ILIYO BORA.

CHAMBO ILIYO BORA.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia.

Katika uvuvi, upo uvuvi wa kutumia ndoano, na pia upo uvuvi wa kutumia nyavu.

Uvuvi wa kutumia ndoano ni uvuvi ambao unahusisha kukamata samaki mmoja mmoja, Hivyo unachukua muda mrefu kidogo na pia una matokeo madogo. Na katikauvuvi huu ni vitu viwili  tu vinahusika katika kukamata samaki, navyo ni Ndoano yenyewe, pamojana Chambo!.

Na chambo inayotumika ni kipande kidogo cha mnofu ambacho kitamvutia samaki, hivyo kila samaki anaponaswa basi mvuvi hana budi kuweka chambo nyingine kwaajili ya samaki mwingine. Huu ni uvuvi mzuri lakini unamatokeo madogo na unachukua muda mrefu..

Lakini upo uvuvi mwingine usiotumia chambo ya mnofu lakini una matokeo makubwa. Na huo simwingine Zaidi ya uvuvi wa nyavu! naTaa.

Uvuvi huu mara nyingi unafanyika usiku, ambapo wavuvi wanakwenda kwenye bahari kuu na kisha kuwasha TAA ZAO zenye mwanga mkali. Na wanapoziwasha basi wale samaki wanavutiwa naule mwanga na hivyo kusogelea chombo na hatimaye kunaswa katika zile nyavu. Na matokeo yake ni makubwa sana, samaki wanapatikana wengi na kwa muda mfupi.

Hii inatufundisha nini, CHAMBO YA MWANGA ni bora kuliko CHAMBO YA MNOFU. Na sisi tunaohubiri Bwana Yesu katufananisha na wavuvi. Na ulimwenguni bahari. Na kama vile wavuvi wanavyokwenda kuvua  usiku, kadhalika na sisi tunakwenda kuvua watu katika ulimwengu wenye giza nene. (Ulimwengu uliopotea, watu waliozama katikagiza la ulimwengu, ambao shetani kawapofusha macho wasione).

Lakini chambo yetu sisi si minofu ya nyama..Hiyohaitakuwa na matokeo yoyote katikati ya giza nene la bahari kuu. Chambo tunayohitaji ni TAA ZINAZONG’AA SANA.

Mathayo 5:4 “Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.

15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.

16 VIVYO HIVYO NURU YENU NA IANGAZE MBELE YA WATU, WAPATE KUYAONA MATENDO YENU MEMA, WAMTUKUZE BABA YENU ALIYE MBINGUNI”.

Kama vile Taa za wavuvi zinavyovutia samaki wengi wakati wa usiku, kadhalika na sisi MATENDO YETU (ambayo ndio mianga kwa ulimwengu), hayo  ndio yanayohubiri sana na yanayo wavuta wengi kwa Kristo kuliko, miujiza tutakayoifanya, au lugha tutakazoongea, au karama zetu au kingine chochote kile.

Kumbuka siku zote chambo iliyo bora ni TAA ZETU ZINAZOWAKA (Ambayo ndio matendo yetu), kwa jinsi taa zetu zinavyozidi kung’aa ndivyo mianga yetu inapoonekana mbali na kuvutia samakiwengi Zaidi..lakini taa zetu zikiwa hafifu, hakuna samaki yeyote tutakayemvuta kwa nyavu zetu.

Wafilipi 2:15 “mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, walaudanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa KAMA MIANGA katika ulimwengu”.

Je Nuru yako inaangaza katikati ya huu ulimwengu wa giza??

Bwana atusaidie na kutubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.

TENGENEZA  NYAVU ZAKO, OSHA NYAVU ZAKO.

Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

Je ni sahihi kuweka walinzi kulinda mali zetu?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments