Jibu: Ijapokuwa zipo sifa nyingi za MITI zinazoipa vigezo vya kuweza kuwakilisha UZIMA au MAUTI…Lakini sifa kuu inayoweza kusimamia nafasi hiyo ni UREFU wa MAISHA.
Mti ndio kiumbe hai pekee kilichoumbwa na MWENYEZI MUNGU kinachoishi muda mrefu kuliko vyote.
Tembo ni kiumbe hai lakini miaka yake ya kuishi ni 80 tu, Kasuku ni miaka 90, kunguru ni miaka 90, kobe ni miaka 200 lakini MITI inafika mpaka miaka 2,000..
Ipo miti yenye miaka zaidi ya elfu chini ya Jua, na bado inaendelea kuzaa matunda yenye ubora ule ule, na zaidi ya yote MITI haisogei ipo palepale, lakini unaishi muda mrefu.
Tofauti na Jiwe, lenyewe Lipo kwa muda mrefu (hata miaka elfu) lakini haliishi (halina uhai), halizai wala haliongezeki liko vile vile siku zote…kama tu mifupa ya mfu iliyopo kaburini kwa mamia ya miaka.
Sasa kwa sifa hiyo ya MTI kuishi muda mrefu, ikiwa bado inaendelea kuzaa matunda yale yale na ikiwa bado ipo eneo lile lile moja..ndio inayoifanya ichukue sifa ya kusimamia UZIMA wa Daima au MAUTI ya daima.
Kwamba tunapotafakari maisha ya MTI (jinsi yalivyo marefu na usivyosogea). Hali kadhalika Mauti ya mtu aliye katika dhambi ni ya DAIMA, na hukumu yake ni ya Daima, vile vile UZIMA wa MTU aliye ndani ya MUNGU ni wa daima na usio badilika.
Sasa huu MTI wa uzima ni nini? Au upo wapi?..
MTI wa uzima ni YESU KRISTO, leo lifahamu hili, Nitakuhakikishia hilo kimaandiko.
Maandiko yanasema Kristo ndiye hekima ya MUNGU.
1 Wakorintho 1:23 “bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi;
24 bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni KRISTO, nguvu ya Mungu, na HEKIMA YA MUNGU”.
Umeona hapo?..KRISTO ni HEKIMA ya MUNGU na kama Kristo ni Hekima ya MUNGU, basi yeye ni MTI wa UZIMA kama maandiko yasemavyo katika Mithali 3:18.
Mithali 3:13 “Heri mtu yule aonaye HEKIMA, Na mtu yule apataye ufahamu……
18 Yeye ni MTI WA UZIMA kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashikamanaye naye”
Kumbe YESU KRISTO ni MTI wa UZIMA, na ana heri kila amshikaye!!!… naam si ajabu tuonapo anatajwa kama Mkuu wa Uzima (Matendo 3:15).
Si ajabu tusomapo kuwa hakuna mwingine mwenye Uzima zaidi yake yeye (Yohana 10:10) na yeye lpekee ndiye njia na Uzima (Yohana 14:6).
Si ajabu kusikia kuwa kila anayemkimbilia anapata uzima wa milele (Yohana 3:16, Yohana 6:47).
Kwaufupi hakuna UZIMA nje ya YESU KRISTO, aliyekufa na kufufuka na kupaa mbinguni, yeye ndiye MTI uishio Milele, na kwake yeye kuna Uzima.
Je unao uzima wa milele?…je umeupata huu Mti?..kama bado mkaribishe YESU maishani mwako na akufanye kiumbe kipya na ukabatizwe kwa maji tele na kwa jjina lake YESU.
Shalom.