by Admin | 27 January 2025 08:46 pm01
SWALI: Je! watu wanapaswa wakemewe au wasikemewe pale wanapofanya dhambi kulingana na 1Timotheo 5:1 na 20?
JIBU: Tusome,
1 Timotheo 5:1-2
[1]Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu;
[2]wanawake wazee kama mama; wanawake vijana kama ndugu wa kike; katika usafi wote.
Na,
1 Timotheo 5:20
[20]Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope.
Mwandishi anatoa maelezo katika mazingira mawili tofauti. Mazingira ya kwanza ni katika eneo la marekebisho na mazingira ya pili ni katika eneo la makosa ya makusudi.
Kwamfano katika vifungu hivyo vya kwanza, anavyosema Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu;analenga hasaa katika makosa ambayo yanajitokeza katikati ya huduma au maisha ya kikristo, kwamfano pengine mtu katika kuhudumu kwake kaonyesha uvunjifu fulani wa nidhani ya kimadhabahu, au kasema lugha isiyo ya staha, au kavaa vazi lisilo na heshima, au kabagua wengine, au kawadhulumu wengine, n.k. ambayo imesababishwa na uchanga wa kiroho au madhaifu ya kibinadamu.
Katika mazingira kama hayo Paulo anamhimiza Timotheo, kulingana na marika yao asitumie kukemea bali awaeleze kwa upole, nao watajirekebisha, akitambua kuwa wapo katika hatua za kuutafuta ukamilifu.
Lakini katika hivyo vifungu vya pili. Analenga Zaidi kwa wale wanaodumu kutenda dhambi. Wanaojua kabisa wanachokifanya sio sahihi, lakini wanaendelea kudumu kufanya hivyo, Paulo anasema hawapaswi kuvumiliwa bali kukemewa mbele ya watu wote.
Kwamfano mtu ni mzinzi, na tabia hiyo anaendelea nayo kanisani, au ni mlevi, au mchonganishi, sasa hawa wanapaswa wakemewe hadharani bila kujali marika yao, ili wengine wasiige Tabia hizo. Kwasababu wakiachwa wataendelea kulichachusha kanisa.
Makanisa mengi leo hii yamekumbwa na matatizo makubwa mpaka kusababisha jina la Kristo kutukanwa Nje, ni kutokana na kuvumiliwa kwa watu wa namna hii wanaodumu katika kutenda dhambi.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Kuna hukumu za aina ngapi?
Mikono iliyotakata ni mikono ya namna gani? (1Timotheo 2:8).
USIZISHIRIKI DHAMBI ZA WATU WENGINE.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/01/27/watu-wanapaswa-wakemewe-au-wasikemewe-kulingana-na-1timotheo-51-na-20/
Copyright ©2025 unless otherwise noted.