by Devis | 17 July 2025 08:46 pm07
SWALI: Katika sehemu nyingi kwenye maandiko tunaona, Mungu akiwaagiza watu wake Wamsifu au wamwabudu katika uzuri wa utakatifu, nini maana ya uzuri wa utakatifu?
1 Mambo ya Nyakati 16:29
[29]Mpeni BWANA utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mje mbele zake; Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu;
Zaburi 29:2
[2]Mpeni BWANA utukufu wa jina lake; Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utautakatifu.
Soma pia..
Zaburi 96:9, 2Nyakati 20:21
JIBU: Kuna mambo mawili hapo.
Jambo la kwanza ni “Uzuri” na jambo la pili ni “utakatifu”
Hasemi tumwabudu Bwana katika utakatifu…hapana bali anasema tumwabudu Bwana katika uzuri wa utakatifu..
Kwa namna nyingine anamaanisha hivi; tuuone uzuri ulio katika utakatifu ndio tumwabudu yeye Katika huo.
Tunaweza tukaujua utakatifu…ambao mfano wake ni kama vile maisha ya upendo, haki, usafi, adabu, amani, utu wema. n.k. Lakini tusione uzuri wa mambo kama hayo mioyoni mwetu au maishani mwetu…wengine wanaona kama utakatifu wa Mungu ni kitu cha kutisha, lakini kumbe Sio..
Siku tukiona uzuri wake ndio hatutakuwa na unafki pale tunapoambiwa tufanye jambo lolote katika utakatifu..
Kwasababu tusipoona hilo, hatma yake huwa ni kutimiza ibada kama tu agizo fulani au utaratibu wa kidini au nidhamu fulani lakini sio katika furaha na faida tuipatayo katika huo utakatifu.
Kwamfano Ibada tu yenyewe ni tendo takatifu lakini je tunaifurahia ibada na kujiona tunanufaika sana mioyoni mwetu katika hizo au tunamtimizia Mungu tu haki yake ya kuabudiwa, lakini hakuna chochote kitufurahishacho ndani yake?
Ibada ifanywayo katika uzuri wa utakatifu ni lazima itaambatana na sifa hizi;
Itakuwa Katika Roho na kweli (Yohana 4:24)
Itafanywa Katika Moyo mweupe( Zaburi 24:3-4). Mfano kusamehe, na amani moyoni.
Itajaa shukrani na kumfurahia Mungu:
Zaburi 139:14
[14]Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa
Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu,
Itamwadhimisha Mungu na kumfurahia sana, kwa maajabu yake na matendo yake makuu, kwa viwango visivyo vya kawaida
Itaambatana na maisha ya utakatifu:
Warumi 12:1
[1]Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
Maisha yetu ni ibada tosha, mwonekano wako, uvaaji wako, usemi wako, tabia yako, vitaakisi utakatifu wa Kristo.
Je umeuona uzuri wa Mungu, uzuri wa ibada, uzuri wa kukusanyika, uzuri wa uumbaji wake, ambavyo ndio uzuri wa utakatifu? Kama ni ndio basi utamsifu na kumwabudu pia katika tabia zake.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Nini maana ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli?
Ibada ni nini,Na je ili ikamilike inapaswa iwe na nini na nini?
DHABIHU ZA ROHO NI ZIPI? (1Petro 2:5)
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/07/17/nini-maana-ya-kumwabudu-bwana-katika-uzuri-wa-utakatifu/
Copyright ©2025 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.