Ubora wa Kuhubiri au kufundisha haupimwi kwa elimu kubwa ya biblia, au mifano mizuri, au utashi fulani wa kupangilia maneno. Hapana, bali ni uwezo wa kupenya katika mioyo ya watu.
Haimaanishi kuwa na elimu ya biblia haichangii ubora wa fundisho au hubiri..inachangia sana lakini hiyo ni kama gamba la juu sana..ambalo linaweza lisitoe pia matokeo yoyote.
Pale fundisho linapoweza kuingia ndani ya moyo wa mtu, kupambanua, kuchoma, kulainisha, kupindua-pindua, kukarabati, kuponya hadi kumfanya mtu kuwa na mwitikio wa dhahiri wa nje. Hilo ndio linaitwa fundisho au hubiri kibiblia.
Sasa tendo hilo mpaka kufikiwa, si jambo rahisi hata kidogo, hakuna utashi wa kibinadamu unaweza kufanya hivyo.
Kwasababu hakuna anayejua ndani ya mtu mwingine kuna nini?
Lakini lililo gumu zaidi ni kuwa hata yeye mwenyewe hajijui vema, kama anahitaji matengenezo katika eneo fulani la moyo wake. Anaweza akawa ana hofu akadhani huwenda chanzo cha hofu hiyo ni ule ugonjwa uliomshika, kumbe chanzo ni kingine kabisa.
Kwasababu mwanadamu mwenyewe moyo wake ni fumbo kubwa.
Yeremia 17:9
[9]Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?
Umeona jinsi ilivyo ngumu sana. Ikiwa yeye mwenyewe hajijui, wewe mtu wa tatu utayajulia wapi yaliyomo moyoni mwake? Lakini Mungu anataka uyahubiri yahusuyo moyo wake.
Usifikiri unapomwona mtu, labda ana huzuni, au furaha au ana tabia za ulevi, wizi, , ukadhani anahitaji fundisho linaloendana na hiyo tabia unayoiona kwa nje.
Unaweza ukakosa shabaha kwa maili nyingi sana, ukifikiri tu hivyo.
Utamwona analia, pengine ni mgonjwa, amefiwa, amepoteza kila kitu kama ilivyokuwa kwa Ayubu na wewe unamfuata na fundisho la faraja, ukadhani kuwa ndio uponyaji wake utakapotokea.
Kumbe Mungu anajua anataka makemeo, na makaripio ili aponywe.
Wakati mwingine utasimama kwenye mkusanyiko wa watu wengi labda mia. Huko huko wapo wanaohitaji faraja, wanaohitaji unabii, wanaohitaji maonyo, wanaohitaji maarifa, wanaohitaji kufunguliwa. Sasa wewe unasimama na fundisho lako lenye mlengo mmoja wa makemeo, unadhani wote watahudumiwa na hilo. Kama ukikosa namna ya ki-ungu, unaweza ukawa unazungumza maneno yako.
Na lengo la Mungu ni watu wote wahudumiwe na Neno.
Hapo ndio linakuja suala la hakuna mbobezi wa fundisho au hubiri. Inahitaji hekima nyingine itokayo juu, ya kuhubiri usichokuwa na ufahamu nacho, au ujuzi nacho.
Siku ile ya Pentekoste, kilichotendeka mpaka ikapelekea watu wale kuchomwa mioyo, na hatimaye kuamini kwa idadi ile kubwa ya watu.
Haikuwa kwasababu walipaza sauti sana, au walihubiri kwa ujasiri sana, au maneno yao yalikuwa na elimu kubwa ya theolojia..
Hapana angalia utaona yalikuwa ni maneno ya kawaida kabisa… lakini yaliyoundwa na Roho Mtakatifu kwa namna ambayo yalipenya katika moyo wa kila mmoja.
Utaona, hatua ya kwanza walinena kwa lugha ambazo hata wao wenyewe hawakuzijua, lugha hizo zilikuwa zinawahubiria wengine.. zinanena mambo yao ya sirini, zinawakemea, zinawafariji, zinawaponya, zinawashuhudia Kristo.
Mpaka baadaye wanamaliza kunena tayari injili imeshahubiriwa wasijue ni kitu gani kimehubiriwa.
Petro aliposimama kumalizia maneno yake, wote wamenywea wanasubiri tu kupewa maelekezo ni nini cha kufanya baada ya pale..
Matendo ya Mitume 2:37
[37]Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
Hao ni watu wasio na elimu yoyote, walikuwapo waandishi, na mafarisayo wenye elimu lakini hakuna matokeo yoyote ya mafundisho yao.
Hata leo hii mimi na wewe.. Tujue kuwa kuhubiri na kufundisha hakutegemei sana ujuzi, au utashi, bali kunategemea zaidi Roho Mtakatifu.
Kwanini Roho Mtakatifu?
Kwasababu yeye ndiye anayeweza kuzama ndani ya mioyo ya watu na kujua shida zao, na kuwaponya.
Ni nini tunapaswa kufanya, ili fundisho likazame moyoni, lisitoke kwa makisio yetu?
Jambo kuu ni Kuwa na maandalizi ya kutosha.
Maandalizi hayo yapo kwa namna mbili.
1) Kumwandalia Roho Mtakatifu njia ya kuanzia..Ndio hapo unahitaji kwanza kusoma na kuandaa somo / fundisho. Kumbuka Ni lazama utenge muda kuandaa fundisho ambalo utalihubiri. Andika, na ujue pa kuanzia, bila kuwa na maandalizi hayo, unasema nitaenda tu kuzungumza. Ujue tayari umeizuia njia ya Roho Mtakatifu kufundisha.
2) Lakini hilo peke yake halitoshi, hatua nyingine ni kuomba maingilio ya Roho Mtakatifu yawe makubwa. Hapo ndipo unatenga muda mrefu wa kuomba, ili Roho Mtakatifu akatembee kwenye vyumba vya ndani kabisa ambavyo wewe hujui, wakati utakaposimama na kufundisha, kushuhudia.
Sasa ukimaliza hapo. Jiandae kwenda kusema ulichokusudia.. kumbuka mhubiri anayetumia dakika kumi kufundisha lakini amekuwa na maandalizi ya masaa matano kwenye kusoma na maombi. Ana nguvu zaidi ya yule atakayefundisha masaa matano, halafu alijiandaa kwa dakika tano.
Mwisho Ukienda kufundisha na kuona mazungumzo yako yanasogea nje ya mada, au taarifa nyingine zinakuja kichwani mwako tofauti na zile ulizoziandika kwenye daftari ujue ni kazi za Roho Mtakatifu usizizuie.
Baadaye utakuja kusikia tu shuhuda, na hata kama hazitasemwa, ujue Neno lako halijakwenda bure.
Tukiwa wahubiri na waalimu wa namna hii. Roho nyingi za watu zitaokolewa.
Kuhubiri ni kusema tusichokijua, cha wengine.
Shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Jina la Bwana YESU libarikiwe, karibu katika kujifunza Neno na Maombi. Kusoma Neno bila Maombi, au kuomba bila Neno ni sawa na kitamba cha bendera kisicho na mlingoti, kupitia mfululizo huu wa tafakari hizi tutapata mwongozo sahihi wa kuomba kupitia maandiko ya kwenye Biblia.
PENDO LA MUNGU.
Bwana YESU alitufundisha kuwa Amri ya kwanza ni “Kumpenda Bwana na ya pili ni kuwapenda majirani kama nafsi zetu”.
Mathayo 22:36 “Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? 37 Akamwambia, MPENDE BWANA MUNGU WAKO KWA MOYO WAKO WOTE, NA KWA ROHO YAKO YOTE, NA KWA AKILI ZAKO ZOTE. 38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO. 40 Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii”.
Mathayo 22:36 “Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?
37 Akamwambia, MPENDE BWANA MUNGU WAKO KWA MOYO WAKO WOTE, NA KWA ROHO YAKO YOTE, NA KWA AKILI ZAKO ZOTE.
38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO.
40 Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii”.
Na tena alisema…
Yohana 14:21 Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.
1. OMBA ONGEZEKO LA UPENDO WA MUNGU NDANI YAKO (Tumia dakika 30)
i. Kwa moyo wako wote.
ii. Kwa roho yako yote
– Hapa utamwomba Bwana kuwa upendo wako ukatoke rohoni, katika kumtafuta kwasababu Neno linasema waabudua watamwabudu baba katika roho na kweli.
iii. Kwa akili zako zote.
– Hapa utaomba Bwana akuwezeshe kumtumikia yeye kwa ujuzi aliokupa, (ule wa asili na ule wa kujifunza) kama ni msomi basi kupitia elimu yako hiyo umtumikie MUNGU, na kuyafanya mapenzi yake.
iv. Kwa Nguvu zako zote.
– Nguvu zinaweza kuwa za mwili kama wewe ni kijana, lakini pia zinaweza kuwa za kifedha, katika maeneo hayo yote mwombe BWANA akusaidie uweze kumpenda MUNGU na kufanya mapenzi yake, Utoe muda wako au mali zako katika kumtumikia MUNGU.
2. OMBA UPENDO KWA JIRANI. (Tumia dakika 30)
Neno la MUNGU linatufundisha kuwa “Tujaponena kwa lugha zote na kufanya ishara zote kama hatuna Upendo sisi sio kitu”
1Wakorintho 13:1 “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao”.
Na tena inasema…
Waebrania 13:1 “Upendano wa ndugu na udumu”.
i. Omba Upendo kwa ndugu wa kiroho (Wachungaji na washirika wenzako)
ii. Omba Upendo kwa ndugu wa kimwili (Wana familia)
3. KEMEA KILA ROHO INAYOJIINUA KUPOOZA UPENDO WA MUNGU, NA WA KINDUGU
Kemea kwa jina la YESU KRISTO kila pando la chuki kanisani kwako, katikati yako na wakristo wenzako, katikati yenu kama familia.
Ulishawahi kutafakari kwanini yule mwanamke aliyemzaa yule mtoto wa kiume, kupewa uwezo wa kukimbilia nyikani, kama njia ya kuepushwa na joka lile?
Kwanini asichuliwe mashambani, au mjini, au milimani, kinyume chake iwe nyikani.
Ufunuo 12:13-14
[13]Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume. [14]Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
[13]Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.
[14]Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
Nyikani ni mahali ambapo hapana uzuri wowote, hapana mahitaji yoyote ya msingi, mahali pasipovutia, kwasasa tunaweza kusema ni nyakati za ukame, ambazo huoni, jambo lolote, huoni hatua yoyote dhahiri,ijapokuwa unajitahidi sana..huoni mafanikio yoyote, huoni mazingira rafiki..
Wakati mwingine ni kipindi cha kupungukiwa kwa muda mrefu, upo pale pale.
Tunapofikia hatua hii, mara nyingi tunamlilia Mungu atuondoe huko, tunahuzunika, tunanyong’onyea, tunasinyaa kiroho, tunamlilia Mungu kwa juhudi nyingi atuvushe..
Ni kweli kabisa jangwa si zuri, lakini wakati mwingine Bwana hulitumia kutuepusha na yule mwovu. Njia pekee iliyompasa huyu mwanamke kuepushwa na joka lile, ilikuwa ni kukimbilia jangwani, na si vinginevyo.
Hivyo ujikutapo katika nyakati mbalimbali ngumu, maadamu upo ndani ya Kristo na unaendelea vema katika imani, fahamu pia huko ulipo Mungu anakuandaa na unatimiza kusudi la Mungu.
Tuwapo katika mazingira yoyote, suluhisho si kulalamika bali ni kuomba, kushukuru na kuitafuta hekima.
WhatsApp
Hauhitaji nafasi kubwa kuzijua siri za Mungu.
Naamani alikuwa ni mtu mkuu, jemedari wa vita, lakini alikaa na ukoma uliomtesa kwa muda mrefu, bila ufumbuzi wowote wala tumaini lolote la kupona.
Katika ushujaa wake, na cheo chake hakuwahi kujua siri za uponyaji zipo wapi, isipokuwa kijakazi wake ambaye hajatajwa hata jina lake, aliuona uzima wa Bwana wake, mahali ulipo, mbali sana na taifa lake, kwa mtu wa Mungu aliyeitwa Elisha.
Kijakazi huyu ndiye aliyefungua njia ya Naamani kupokea uponyaji wake mkamilifu
2 Wafalme 5:1-4
[1]Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake BWANA alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma. [2]Na Washami walikuwa wametoka vikosi, wakachukua mfungwa mmoja kijana mwanamke kutoka nchi ya Israeli; naye akamhudumia mkewe Naamani. [3]Akamwambia bibi yake, Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria! Maana angemponya ukoma wake. [4]Mtu mmoja akaingia, akamwambia bwana wake, akasema, Yule kijana mwanamke aliyetoka nchi ya Israeli asema hivi na hivi.
[1]Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake BWANA alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma.
[2]Na Washami walikuwa wametoka vikosi, wakachukua mfungwa mmoja kijana mwanamke kutoka nchi ya Israeli; naye akamhudumia mkewe Naamani.
[3]Akamwambia bibi yake, Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria! Maana angemponya ukoma wake.
[4]Mtu mmoja akaingia, akamwambia bwana wake, akasema, Yule kijana mwanamke aliyetoka nchi ya Israeli asema hivi na hivi.
Huhitaji kuwa mtu fulani, wala huhitaji kuwa hodari duniani, kuwa msomi sana, jasiri sana, kuzidhihirisha nguvu za Mungu, au kuwahudumia watu wake, au kuwaponya na kuwafundisha, unahitaji tu, unyenyekevu ambao unadhihirishwa kwa kumcha Bwana. Kisha yeye mwenyewe Mungu kwa hekima yake ataitengeneza njia yake anayoijua mwenyewe kuwasaidia wengine kupitia wewe.
Ndio maana Neno la Mungu linasema;
1 Wakorintho 1:26-29
[26]Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; [27]bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; [28]tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; [29]mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.
[26]Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;
[27]bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;
[28]tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko;
[29]mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.
Wekeza zaidi kwenye kumcha Mungu, zaidi ya juhudi za kibinadamu kwasababu hekima yake ni mbali sana na mavumbuzi ya wanadamu.
Katika maandiko ukikutana na kisa kinaishia kwa kusema ‘hata leo’. Basi kuwa makini hapo kwasababu lipo la kukusaidia.
Kwamfano Ibrahimu alipopanda kule mlimani kumtolea Mungu sadaka kwa Isaka, Mungu alimpa kondoo badala yake, Kwa tukio hilo Ibrahimu akapaita mahali pale Yehova-yire. (Maana yake Mungu-mpaji). Hivyo jambo lile maandiko yanasema liliendelea kutamkwa na watu kwa wakati mwingine mwingi sana kama usemi uliohai ‘Yehova-yire’, Mungu atupaye.
Mwanzo 22:13-14
[13]Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. [14]Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire, kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana.
[13]Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.
[14]Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire,
kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana.
Mfano mwingi ni wakati wa Yoshua alipoiangamiza nyumba ya Akani, msaliti, biblia inasema;
Yoshua 7:26
[26]Kisha wakakusanya juu yake chungu kubwa ya mawe hata leo; naye BWANA akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale likaitwa, Bonde la Akori, hata hivi leo.
Ikiwa na maana bonde hilo liliendelea kuitwa vile vile hadi wakati wa mwandishi. ‘Ipo sababu’.
Mfano mwingine ni kipindi cha Yehu alipoyavunja mahekalu ya Baali..
2 Wafalme 10:27
[27]Wakaibomoa nguzo ya Baali, na kuiangusha nyumba ya Baali, wakaifanya choo hata leo.
Ikiwa na maana mpaka wakati mwandishi anaandika hicho kitabu eneo hilo lilikuwa ni choo.
Mahali pengine ni hapa..
Israeli kuwa hatarini kuvamiwa na wamoabu, wakamlilia Mungu, kisha kawaambia hawatapigana vita bali watakwenda kuokota nyara, kazi yao iwe ni kusifu na kuimba tu. Maadui zao wakauana wao kwa wao Na eneo lile wakaliita bonde la baraka hata leo.
2 Mambo ya Nyakati 20:25-26
[25]Nao Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao, wakaona kati yao wingi wa mali, na mavazi, na johari za thamani, walivyojivulia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka nyara, maana zilikuwa nyingi sana. [26]Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka; maana ndipo walipombarikia BWANA; kwa hiyo jina lake mahali pale pakaitwa Bonde la Baraka hata leo.
[25]Nao Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao, wakaona kati yao wingi wa mali, na mavazi, na johari za thamani, walivyojivulia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka nyara, maana zilikuwa nyingi sana.
[26]Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka; maana ndipo walipombarikia BWANA; kwa hiyo jina lake mahali pale pakaitwa Bonde la Baraka hata leo.
Mahali pengine ni wakati wa kifo cha Yuda, lile shamba lililonunuliwa liliitwa konde la damu mpaka nyakati za mwandishi..
Mathayo 27:8
[8]Kwa hiyo konde lile huitwa konde la damu hata leo.
Sasa biblia kusema ‘hata leo’ sio tu kutoa uthibitisho wa tukio kwamba kweli lilitokea ..lakini ni vema kujua tafsiri yake rohoni…kwamba kuna minyororo aidha ya baraka au laana inatembea mpaka leo.
Kwamfano watu waliposema Yehova-yire walijua Mungu ni mpaji wakati wote…hivyo wakamwona katika mazingira hayo..ndio maana wakasema ‘hata sasa’ si tu wakati wa Ibrahimu.
Neno hilo lipo hai hata leo rohoni. Ukiamini Mungu aliyomtendea Ibrahimu anakwenda kukutendea na wewe, utapokea…kwasababu lipo hivyo hata leo.
Anaposema mahali pale pakaitwa bonde la baraka hata leo. Ni kweli rohoni hata leo bonde hilo lipo.
Ukiamini kwamba katika kumwimbia Mungu unaingia katika bonde la baraka. Utapokea vingi kwa Mungu, sawasawa na walivyopokea Israeli kipindi cha Yehoshafati vitani.
Hivyo mambo mengi na matukio mengi yanaendelea kutembea katika roho hata sasa…Je! Macho yako yanaona?
Ukiwa mwovu kama Akani, kumbuka bonde la Akori lipo mpaka leo, ikiwa utakuwa msaliti kama Yuda konde la damu lipo hata leo utazikiwa huko.
Chagua mema, yaishi mema, upokee mema
Shalom.
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Moja la lango ambalo Mungu hulitumia sana, kutufikishia sisi taarifa zake, ni ndoto. Na kama ni lango la Mungu basi ni vema tufahamu kuwa ibilisi hatalipenda. Hivyo atahakikisha taarifa hizo anazivuruga au hazitufikii vema, kama tu vile anavyohakikisha watu hawaliewi Neno, au mahubiri, Ndivyo anavyofanya na kwenye ndoto pia.
Taarifa zitokazo kwa Mungu zinaangukia katika makundi matatu;
1) Tahadhari
Hizi ni taarifa za maonyo, au hatari zinazokuja mbeleni. Mfano wa taarifa hizi ni kama zile zilizomfikia Yusufu, alipokuwa Israeli, akaambiwa akimbilie Misri, kwasababu Herode anataka kumuua mtoto, na aliporudi baadaye, akaonywa tena asikae Yerusalemu, bali aende Nazareti.
Mathayo 2:19-22
19 Hata alipofariki Herode, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri, 20 akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto. 21 Akaondoka akamchukua mtoto na mamaye, akafika nchi ya Israeli. 22 Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki huko Uyahudi mahali pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko; naye akiisha kuonywa katika ndoto, akasafiri pande za Galilaya,
Lengo la taarifa hizi ni mtu kuchukua hatua, aidha ya kivitendo au ya kimaombi.
Kwamfano Mungu anaweza kukuonyesha ajali, au msiba fulani. Hapo ujue hasaa unahitajika kuchukua hatua kimaombi kuharibu hizo roho za mauti, kwa kinywa chako.
2) Unabii
Hizi ni taarifa za mambo yajayo, Yale yatakayotokea baadaye, kwenye maisha yako, huduma, familia, nchi, au taifa. Mfano wa ndoto hizi, ni kama ile ya Farao juu ya miaka saba ya shibe na njaa, (Mwanzo 41) na Nebukadreza, juu ya ile sanamu kubwa, iliyowakilisha falme nne, zitakazokuja kusimama ulimwenguni (Danieli 2).
Halikadhalika Mungu anaweza kukuonyesha, maisha yako baadaye yatakuwaje, huduma yako baadaye, itasimamaje, maono yako baadaye yatafikia wapi, anaweza kukuonyesha mambo ya siku za mwisho, matukio yajayo, kuhusu nchi, watu, familia. Hatua unayopasa kuichukua ni kuomba, na kuandaa mazingira sasa. Mfano Farao aliposaidiwa tafsiri ya ndoto yake na Yusufu, alichukua hatua ya kuweka hazina ya vyakula kwasababu njaa ilikuwa inakuja mbele. Mungu akikuonyesha huduma yako itakuwa kubwa, anza leo kujiwekea hazina ya maarifa ya Neno la Mungu, anza kutendea kazi wito wako,. Akikuonyesha unawaombea watu wengi wanapona, anza leo kuwaombea watu hata kama hawaponi, omba hivyo hivyo kila siku, usikae tu ukasubiri ije kutimia huonyeshi jitahada yoyote, akikuonyesha biashara yako imekuwa, ongeza juhudi kufanya kazi.
3) Baraka
Mungu anaweza kuachia Neno la Baraka kwako, kwamfano ukaota, ndoto njema, labda unatiwa mafuta na Kristo, au unaambiwa maneno ya mafanikio kama vile Sulemani alipotokewa na Mungu na kuelezwa atapokea Hekima, na kuwa na mali nyingi. Uotapo ndoto ambazo ni za mafanikio kwako, uamkapo, hakikisha unazinenea kwa Imani. Unasema
“Na iwe kwangu kwa jina la Yesu Kristo”. Kama tu vile unavyobatilisha ndoto za maovu, labda mauti, vivyo hivyo hizi unazipokea kwa kinywa chako. Ni muhimu sana.
Ibrahimu aliota ndoto
Mwanzo 51:1-6
Baada ya mambo hayo neno la Bwana likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana. 2 Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski? 3 Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu. 4 Nalo neno la Bwana likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi. 5 Akamleta nje, akasema, Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. 6 Akamwamini Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.
Sasa kinachotokea ni kwamba ndoto nyingi sana, za taarifa mbalimbali kutoka kwa Mungu zinapotea akilini mwetu, na tunaona kawaida,
Ndoto hupotea kwa aidha namna mbili;
Namna mojawapo inaweza kutokea kwa mtu. Usikae ukafikiria kisa hukumbuki chochote, ukadhani hukuota ndoto yoyote. Zipo ndoto ulizoota. Hivyo ni vema ukajifunza namna ya kukabiliana na lango lako la ndoto. Ndio maana utaona wengine tukio likishatokea ndio anakumbuka kuwa alishawahi onyeshwa tukio hilo. Hiyo haitakiwi.
Nifanye nini ili nikumbuke ndoto zangu?
Njia tatu zinazoweza kumfanya mtu akumbuke ndoto.
i) Kuomba:
Kila asubuhi uamkapo, katika maombi yako, hakikisha unashika Kichwa chako, kisha unasema maneno haya
‘Baba, nafungua lango la ndoto zangu, yote uliyosema nami usiku nilipolala, ninayoyakumbuka na nisiyoyakumbuka yakawe bayana sasa kwa kwa jina la Yesu, ndoto zilizoibiwa na ibilisi, kumbukumbu zangu, na fikra zangu zilizofutika, navirejesha vyote ndani ya ufahamu wangu sasa kwa jina la Yesu Kristo’.
Ukijifunza kuomba namna hiyo, tayari umekaribisha msaada wa Mungu, mahususi katika eneo lako la ndoto na hivyo urahisi wa kukumbuka unakuja.
ii) Utulivu (Kutafakari)
Ukishaomba, pendelea kupata utulivu, kisha tafakari kwanza Neno la Mungu. Kila asubuhi hakikisha unapata kwanza mkate wa uzima ambao ni Neno, tafakari Neno kwa muda kidogo, jiulize vifungu hivi vinamaana gani, je! Siku ya leo nitaviwekaje katika maisha yangu? Fanya tu hivyo tembea maeneo mbalimbali ya kwenye biblia, kisha tafakari tena juu ya maisha yako ya rohoni, juu ya maono yako, juu ya familia yako utajiboreshaje, baadaye juu ya ratiba zako za siku..
Katika wingi wa kutafakari, mara nyingi Mungu hurejesha ndoto zilizosahaulika, utashangaa katika tafakari Fulani hapo hapo unakumbuka kuna jambo uliota, linaloendana na tukio hilo. Ujue huo ni ujumbe wa Mungu.
Ukikosa muda wa kutosha asubuhi, Fanya hivyo muda wa usiku kabla ya kulala, Pata utulivu mwingi peke yako, Utakumbushwa ndoto nyingi.
iii) Mazungumzo
Njia nyingine ambayo humfanya Mungu arejeshe ndoto zetu kirahisi, ni katika mazungumzo, kumbuka kila eneo la maisha yako au wengine, yamkini Bwana alishawahi kusema na wewe, kwa njia ya ndoto, lakini hujui.
Kwamfano ukiwa na mwenzako, au wenzako, mnazungumza sana, Habari njema za kanisa, katika mazungumzo ya muda mrefu ikiwa lipo ambalo Bwana alikuonyesha, utaona kumbukumbu hiyo inakujia, au labda mnazungumza kwa kina Habari ya siku za mwisho, Kumbukumbu ya ndoto kama hiyo itakujia, au malengo ya maono yako.
Hivyo mazungumzo mazuri na yenye maana hurejesha fikra zilizopotea. Kwahiyo, jijengee desturi ya kuwa na mazungumzo mema.
Zingatia pia si kila ndoto hutoka kwa Mungu, ili kuweza kutofautisha ndoto za Mungu na za shetani, fungua link hii, uweze kupitia..>>>> https://wingulamashahidi.org/2019/09/03/nitajuaje-kama-ndoto-ni-ya-mungu-au-ya-shetani/
Mungu akubariki.
Kuna ndege anaitwa kiruka njia, ambaye anatajwa kama mmoja wa ndege najisi, kwenye Kumbukumbu 14:15, lakini ndege huyu anasifa moja ambayo, huwa ina funzo kubwa sana la kiroho.
Tofauti na ndege wengine, ambao huruka aidha mchana, au usiku, kujitafutia chakula, kwamfano mwewe, mbayuwayu, korongo, tai, ni ndege wa mchana, lakini pia bundi, popo, ni ndege wa usiku, wote hawa hufanya kazi aidha majira ya kutwa nzima ya mchana, au usiku kucha.
Lakini kiruka njia, huruka zaidi, majira ya alfajiri sana, na jioni sana. Majira haya huyapendelea kwasababu, ni wakati wa mageuko ya siku, ambayo ndege wote wawindaji hujiandaa Kwenda mapumziko, au kuamka. Kwamfano muda wa jioni kama vile saa 12, ndege wakali wawindaji kama vile tai, mwewe, kipanga, n.k. wanaacha uwindaji, na kutafuta makao yao kupumzika, lakini pia wakati huo huo ndege wakali wa usiku kama vile bundi, hujiandaa kutoka waende kwenye mawindo yao saa mbili, Kwahiyo huo muda hapo Katikati mazingira kwake huwa si ya upinzani mkubwa.
Kwasababu yeye ni ndege dhaifu, na anaweza kuwindwa na ndege wakubwa, majira hayo kwake ni salama zaidi. Vivyo hivyo ule muda wa alfajiri sana, miale ya jua inapoanza kuonekana kwa mbali sana, hutoka na Kwenda kuwinda, muda huo ndege wa usiku ndio wanakwenda kulala, huku ndege wa mchana wanajiandaa kutoka, mpaka inapofika saa 12 asubuhi, tayari ameshamaliza uwindaji wake.
Licha ya kuwa wakati huo, ndege wengi hawapo hewani, lakini wakati huo, wa alfajiri sana na jioni sana, ndio makundi ya wadudu wengi wa ardhini hutoka kuruka juu, ikiwemo mbu, kumbikumbi, mchwa, nondo, mende n.k. kwasababu yeye hula wadudu, anaweza kukamata wadudu hata elfu moja ndani ya saa moja tu. Hivyo kwa muda mfupi sana akawa ameshashiba, zaidi ya mihangaiko mingi ya kutwa nzima, kugombania vyakula, na masumbufu mengi.
Ndege huyu mchana hupumzika zake, kwenye miti, na usiku pia, lakini hutumia alfajiri yake na jioni yake vizuri. Ndio maana ni vigumu kujulikana, kwasababu shughuli zake anazifanya wakati anga ni tulivu.
Hutufundisha nini?
Bwana alituambia tuwatafakari ndege (Mathayo 6:26)
Ni lazima tuthamini mida hii miwili, kuitumia kuwa uweponi mwa Bwana, Bwana Yesu alipendelea sana, kuamka alfajiri kuomba,
Marko 1:35 Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.
Ipo faida kubwa sana kuamka mapema kuomba kwasababu, muda huo anga ni tulivu, wakati watu wamelala, wewe unapokea thawabu za siku kutoka kwa Bwana. Kuna usemi unaosema biashara ni asubuhi, kwasababu wameona Riziki nyingi huwaga majira hayo, vivyo hivyo rohoni, ukijifunza kuomba majira hayo, na jioni pia kabla hujaimaliza siku, Basi utaona tofauti kubwa sana, na wepesi mwingi wa masumbufu ya siku.
Hawa ndege katika Walawi 11:13-19 ndio ndege gani kwasasa?
MTEGO HUTEGWA BURE, MBELE YA MACHO YA NDEGE YE YOTE.
Je tamaa ni dhambi kulingana na Yakobo 1:15?
Kitendo cha kumtia mtu adabu ndio kuadibu. Maana yake kuchukua hatua za makusudi kuadhibu, au kukaripia, au kuonyoosha mwenendo lakini kwa lengo la kujenga sio kulipiza kisasi.
Neno hilo utalipata kwenye vifungu hivi.
Zaburi 94:12
[12]Ee BWANA, heri mtu yule umwadibuye, Na kumfundisha kwa sheria yako;
Zaburi 94:10
[10]Awaadibuye mataifa asikemee? Amfundishaye mwanadamu asijue?
Mungu akiitwa Baba, basi tujue kuwa sisi ni watoto wake, na kama ni watoto wake basi atatuadabisha pale tunapokosea..
Kubali kuadibiwa na Bwana…
Beliari ni nini? (2Wakorintho 6:15)
‘laana ya torati’ maana yake ni nini?
Mapokeo ni nini?
Biblia inatuonyesha Mungu ndiye muumba wa vitu vyote
Mwanzo 1:1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
Lakini hatujui ni nini kilitokea baadaye kikaifanya dunia kuwa ukiwa, mpaka akaanza kuirekebisha tena dunia aliyoiumba mwanzo..
Kwasababu mstari wa 2..unasema nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji,
Mungu akaanza tena kuifanya ikaliwe na watu, akaleta tena nuru kutoka kwenye giza, akayatenga maji, na kuyaweka sehemu stahiki, akalitokeza anga..akamuumba mwanadamu.
Dunia ikawa nzuri tena, lakini baadaye mwanadamu akaasi, akaiharibu duniani, mpaka ikaangamia kwa maji.
Bado Mungu hakuikatia tamaa dunia yake, akawaongeza, Nuhu na wazao wake, baadaye akamchagua Ibrahimu ili kumwandaa mkombozi atakayeikomboa dunia kikamilifu, akaja Kristo ulimwenguni ndio mwokozi wetu.
Watu wakaokolewa, ijapokuwa waliendelea kuiharibu dunia, bado Mungu akawa kwenye mwendelezo wa uumbaji wake unaoharibiwa .
Na kama tunavyojua Kristo aliahidi kurudi tena duniani mara ya pili, kuwanyakua watu wake, kisha kuukarabati huu ulimwenguni na kuufanya kuwa mbingu mpya na nchi mpya.(Ufunuo 21)
Hivyo kama ukichunguza asili ya tabia ya Mungu, si kufanya kitu mara moja, kisha pale kinapoharibika anakikatia tamaa ..
Hapana utaona hukiumba tena na tena na tena…kwa miaka na miaka na miaka..tena huanzia mbali sana mpango wake wa ukarabati..
Na sisi ni lazima tujue tumeumbwa kwa mfano wake na sura yake..ikiwa unaona hakuna mwenye hekima duniani kumzidi Mungu, na kila lifanyalo ni bora, na kamilifu basi jifunze kuiga tabia zake ufanikiwe…
Mungu wetu alikuwa na siku moja katika juma ya kupumzika, wewe si ‘busy’ zaidi ya Mungu mpaka siku zote saba katika juma, mwaka mzima unafanya kazi mpaka unakosa muda wa kumwabudu Mungu wako.
Vivyo hivyo ni lazima kutambua kuwa kazi zake zimepitia changamoto nyingi sana za kuharibiwa zaidi ya zako lakini amekuwa katika uumbaji wake kila siku..Na wewe pia kuharibiwa kwa maono yako, si sababu ya kukata tamaa na kusema sitaendelea mbele…inuka anza tena na tena..
Unamtumikia Mungu, ile huduma iliyokaa ndani yako, ni kama imekufa, mwanzoni uliona hatua lakini sasa huoni, pengine ni kutokana na kuwa umedhulumiwa, umeibiwa, umefukuzwa..inuka tena na tena, anza upya..
Kuacha kazi uliyokwisha itaabikia na kuitolea jasho jingi, ni ishara ya kuwa bado tabia ya Mungu haijaumbika ndani yako.
Kumbuka mpaka leo hii Mungu anaendelea kufanya uumbaji wake, ijapokuwa kazi hizo zingepeswa zikamilike tangu kule mwanzo…Wewe ni nani usifanye matengenezo yako yaliyokufa kila siku?
Anza sasa. Fanya kazi na Mungu.
MBONA MMESIMAMA HAPA MCHANA KUTWA BILA KAZI?
USIMPE MWANAO VITU SASA.
2 Samweli 23:9-10
[9]Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao; [10]huyo aliinuka, akawapiga Wafilisti hata mkono wake ukachoka, na mkono wake ukaambatana na upanga; naye BWANA akafanya wokovu mkuu siku ile; nao watu wakarudi nyuma yake ili kuteka nyara tu.
[9]Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao;
[10]huyo aliinuka, akawapiga Wafilisti hata mkono wake ukachoka, na mkono wake ukaambatana na upanga; naye BWANA akafanya wokovu mkuu siku ile; nao watu wakarudi nyuma yake ili kuteka nyara tu.
Kibaolojia mwili wa mwanadamu unapokamata kitu, kwa muda mrefu sana, kwa nguvu, huwa unatabia ya kukakamaa katika hali hiyo hiyo hata kama mtu huyo hatakuwa na nia ya kuendelea kukishikilia kitu hicho.
Ndicho kilichomkuta huyu shujaa wa Daudi, alipokutana na jeshi la wafilisti angali yupo peke yake. Aligundua kitu pekee ambacho kingeweza kumtetea ni upanga wake. Hivyo aliukamata kwa nguvu sana bila kuuachia, akaanza kupambana na wafilisti wale kwa muda mrefu, hakujua kuwa mkono wake utabakia katika hali ile ile…yeye aliendelea tu kupigana vita, mpaka baadaye aliposhangaa kuona hana jitihada yoyote tena ya kuushika upanga, ni kama vile ulikuwa ni sehemu ya kiungo chake…kazi yake ilikuwa ni kurusha tu mkono kuupeleka anapotaka, huku upanga ukiwa tu pale pale kiganjani hautoki…
Kikawaida hali ikishafikia hatua hiyo huwa inamgharimu mtu masaa mengi hata siku, ili kung’atuka kutoka kwenye kitu kilichoshikamana naye..wakati mwingine ili kuharakisha uponyaji, wengine hutumia maji ya uvuguvugu na kuchua kiganja kwa muda baadaye kunyosha kidole kimoja baada ya kingine…
Sasa askari wa mwilini ni kivuli cha mtu wa rohoni. Yeye naye ana mikono na analazimika wakati wote kuwa na upanga…Lakini si upanga tu, wa kushika, bali ule Ugandao na mkono.
Waefeso 6:11-14,17
[11]Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. [12]Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. [13]Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
[11]Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
[12]Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
[13]Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
[14]Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,..
[17]Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
Kama maandiko yanavyotuonyesha hapo Mtu wa rohoni, hulazimika kubeba upanga wake, ambao ni Neno la Mungu.
Tunapoonyesha nia ya kuling’ang’ania Neno la Mungu, mwanzoni ni kama tutatumia jitihada zetu, lakini haitakuwa hivyo mbeleni …baadaye litashikamana na sisi..maana yake haitakuwa jitihada tena kuliishi.
Jambo lolote la kiroho, mfano maombi ya masafa marefu, mwanzoni ukianza utaona kama ni jitihada zinatumika lakini ukiendelea mara mbili, mara tatu utaona ni kawaida..
Mambo yote ya rohoni iwe ni upendo, unyenyekevu, utaanza kwa jitihada fulani lakini Kwasababu umekusudia tu kung’ang’nia kwa nguvu, utagandamana navyo.
Kumbuka hakuna wepesi wowote utakuja bila mtu kutia nia kwanza. Anza sasa kutendea kazi Neno la Mungu.