Je! Ni dhambi kwa kijana aliyeokoka kuvaa suruali za kubana (model), kunyoa mitindo (mfano kiduku), ?

by Admin | 2 September 2019 08:46 pm09

JIBU: Kumbuka mavazi tangu zamani licha tu ya kuwa na matumizi ya kujisitiri yalitumika pia kueleza hali ya mtu rohoni jinsi ilivyo. Kwamfano kwenye biblia utaona kulikuwa na mavazi ya kifalme (2Nyakati 18:9, Esta 6:8), Ni mavazi yaliyoweza kumtofautisha mfalme na watu wengine wa kawaida.Kulikuwa na nguo za magunia, tunalithibitisha hilo sehemu nyingi katika biblia, mtu akionekana amevaa mavazi ya magunia iliashiria kuwa yupo katika majonzi na maombolezo makubwa ya rohoni, pengine kwa kufiwa au kuomba toba mbele za Mungu…

Pia biblia inataja kuwa kuna mavazi ya kikahaba, (Mwanzo 38:14 ) ukisoma Mithali 7:10 inasema “Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;…mtu yeyote aliyekuwa ameonekana ameyavaa hayo” Kulikuwa na mavazi ya kikuhani pia ambayo yakivaliwa, yanamjulisha Yule ni Kuhani nk. yote hayo mtu alipokuwa akivaa yalikuwa yaashiria kitu Fulani rohoni.

Vivyo hivyo hata sasa, mavazi yanabeba tafsiri Fulani ya mtu rohoni. Kama binti wa kike anatembea barabarani kava kimini, au suruali, au top, au nguo nyepesi inayoonyesha maungo yake ya ndani, huyo tayari ni kahaba, kwasababu mavazi hayo yanavaliwa na wale makahaba wa KASINO na DISCO, ndio kitambulisho chao kule., mfano leo hii ukikutana na gari linye kibao juu kimeandikwa TAXI, huhitaji mpaka lisimame na kuliuliza kama kweli ni TAXI, moja kwa moja tokea likuwa kule mbali utalipunga mkono, lisimame kisha utapanda, kwani kibao chenyewe kinajieleza juu kwa gari lile ni la umma,

halidhadhalika ukimwona binti anatembea na nguo hizo hauhitaji kumthibitisha kama yeye ni kahaba tayari mbinguni na duniani anaonekana kama ni kahaba. Sasa kwa kijana wa kiume, suruali za milegezo, suruali za kubana (zinazojulikana kama utumbo wa kuku), hizo zinajulikana ni za wasanii wa kidunia na wanamtindo wa ulimwengu huu ambao hata habari na Mungu hawana…Lengo lao kubwa ni kuitangaza miili yao na mitindo yao.. Sasa Jiulize wewe kijana wa kikristo unayesema umeokoka unavaa milegezo,na suruali za kubana n.k. mbinguni na ulimwenguniunadhani unaonekanaje?, wewe na wanamuziki wa ulimwengu huu ni kitu kimoja hata kama utakana, ndivyo ulivyo..

Halidhadhalika unanyoa viduku, na kusuka, na kufuga rasta mtu akipita barabarani akakuita kama mmoja wapo wa wasanii wa ulimwengu wanaofanya hivyo au akikuita Bob Marley mvuta bangi utakwazika?.

Biblia inasema.

Warumi 12:1 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.

2 Wala msiifuatishe NAMNA YA DUNIA HII; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu”.

Hilo neno hapo juu NAMNA YA DUNIA HII, linamana ya FASHION. Kabla haujafikiria kuvaa suruali ya kubana, embu mvishe kwanza Yesu, kabla hujafikiria kunyoa kiduku mnyoe kwanza Yesu, ukiona hizo nguo hawezi hata kuzitazama mara mbili , inakupasaje wewe kama hayo mambo hayamstahili Mungu, wewe unayavaa ya nini?. Hivyo ni DHAMBI kwako..

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

FASHION! NI DHAMBI KWA BINTI ZA MUNGU.

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

UMUHIMU WA KUZALIWA MARA YA PILI.

JE! WEWE NI MWANA WA IBRAHIMU?.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

HUDUMA YA (ELIFAZI, BILDADI, NA SOFARI).


Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/02/je-ni-dhambi-kwa-kijana-aliyeokoka-kuvaa-suruali-za-kubana-model-kunyoa-mitindo-mfano-kiduku/