Kwanini kabila la Dani na Efraimu hayaonekani yakiorodheshwa miongoni mwa yale makabila 12 ya Israeli katika Ufunuo 7?

by Admin | 3 September 2019 08:46 am09

SWALI: Yakobo aliyeitwa ISRAELI:Alikuwa na wana 12 (Benyamini,Yusufu,Yuda,Lawi,Asheri,Isakari,Gadi,DANI,Zabuloni,Naftali,Reubeni,&Simeoni) Ambao kabila za Taifa la Israeli ziliitwa kwa majina ya hao wana 12 wa Israeli. Wana wawili wa Yusufu, Benyamini na Manase nao pia wanatajwa kuwa miongoni mwa makabila ya ISRAEL..Hivyo wana wa watoto wakiume wa Yakobo (WALIOFICHWA KUTAJWA KAMA KABILA ZA ISRAEL.Mfano wa Manase & Efraimu) nao pia wakitajwa kama kabila za Israel, hilo ni ono tosha kwamba Nchi ya ISRAELI imeundwa na zaidi ya KABILA 12 hivi? (SWALI:Bwana Mungu anapoenda kuupachika mzeituni halisi kwenye shina lake kulingana na Warumi 11} tunafunuliwa watakaopata hii neema ya mzeituni halisi kupachikwa ni KABILA12 tu za ISRAELI tunazizoma kwenye Ufunuo7:

Swali hapo ni kwanini hapo KABILA LA DANI na lile la Efraimu Yamenyimwa hiyo Neema (hayajatajwa hapo) kwenye hiyo ufunuo mlango wa 7?


JIBU: Shalom ndugu.. Makabila ya Israeli ni 12 tu, Efraimu na Manase, walihesabiwa tu miongoni mwa makabila 12 kwa upendeleo wa Yusufu kutoka kwa baba yake lakini makabila halisi yaani watoto wa Yakobo ni 12 tu, ambao wanatambulika kuliunda taifa la Israeli…na ndio wale ambao majina yao yanaonekana katika milango ya kuta za mji ule Yerusalemu mpya..(Ufunuo 21:12)..

Hao ni wale watoto halisi 12 wa Yakobo, kama tu vile misingi ya mji ule ilivyokuwa 12 kufunua wale mitume 12 wa Bwana… Sasa ni kwanini Efraimu na Dani, hawaonekani pale kwenye Ufunuo 7…Sasa kitu cha kutazama hapo ni kwamba kiuhalisi ni kabila moja tu halipo pale, nalo ni kabila la DANI, lakini kabila la Efraimu lipo, ndio lile kabila la Yusufu lililotajwa pale…Ikumbukwe kuwa Yusufu aligawanyika mara 2, Manase na Efraimu, Haiwezekani liwepo kabila la Yusufu halafu tena liwepo kabila la manase na Efraimu kwa mpigo, hapo basi Yusufu angepaswa awe na watoto wengine tofuati na hao wawili ili atengeneze kabila lake mwenyewe, lakini kama wale ni watoto wake, basi Kabila lake lazima ligawanyike tu,..

Hivyo unapoona Biblia inasema Kabila la manase halafu tena inasema kabila Yusufu ujue basi alimaanisha kabila la manase na kabila la Efraimu, vile vile unapoona mahali biblia inasema Kabila la Yusufu halafu tena kabila la Efraimu, basi ujue linamaanisha kabila la Manase na kabila la Efraimu…

Soma (Hesabu 1:32, 13:11)   Lakini tukirudi kwenye kabila la Dani ambalo tunaona limeondolewa, biblia haijatoa sababu ya moja kwa moja kwanini limetolewa, lakini tukirudi nyuma, tunaweza tukahisi sababu moja, kumbuka Mungu huwa hapendezwi na mambo maovu hususani uabuduji sanamu,..Na ukirudi kwenye agano la kale utaona ni kabila moja tu la Dani ndio lililokuwa ovu kiasi cha kutokumwogopa Mungu hadi kwenda kunyanyua sanamu na kuiweka katika mji wao (soma Waamuzi 18)..Hilo likawa chukizo kufikia hatua ya Mungu kuwaondoa katika neema ya wokovu aliokusudia kuuleta baadaye juu ya Israeli,..Hiyo inaweza kuwa ni sababu mojawapo zinaweza kuwepo sababu nyingine tusizozijua, pengine hadi hapo Mungu atakapotufunulia..

Lakini katika ulimwengu ujao Dani atakuwepo, Efraimu na Manase watarudi chini ya viuno vya Baba yao Yusufu na kuhesabiwa kuwa kabila moja.  

Ubarikiwe sana.


 

Mada Nyinginezo:

UFUNUO: MLANGO WA 7 & 11

UFUNUO: MLANGO WA 14

MPAKA UTIMILIFU WA MATAIFA UTAKAPOWASILI.

CHAKULA CHA ROHONI.

SWALI LA KUJIULIZA!

USILITAJE BURE JINA LA BWANA!


Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/03/kwanini-kabila-la-dani-na-efraimu-hayaonekani-yakiorodheshwa-miongoni-mwa-yale-makabila-12-ya-israeli-katika-ufunuo-7/