Dini ni nini, na Imani ya kweli ni ipi?

by Admin | 23 September 2019 08:46 pm09

Dini ni nini? Dini ya kweli ni ipi? na Imani ya kweli ni ipi?

Dini ni tendo linalotokana na Imani fulani (mambo ya rohoni), pale tu mtu anapoamini uwepo wa Mungu au hata uwepo wa shetani au hata kitu chochote kisichoonekana cha kuabudiwa basi hapo hapo dini inazaliwa, ndipo hapo utaona mtu anajiwekea  miiko Fulani ya kufuata au utaratibu Fulani au ustaarabu Fulani kwamfano wanaoamwamini Buddha utaona wanao taratibu zao za kufuata ili kumwabudu mungu wao  ipasavyo ndipo hapo utakuta ni lazima wote wavae mavazi Fulani, au wapitie madarasa Fulani, au waishi maisha Fulani ya kujinyima au kutokushirikiana na jamii Fulani ya watu au kufunga, au kutokula aina Fulani ya vyakula n.k sasa hiyo ndiyo inayoitwa dini..

Vivyo hivyo na katika ukristo, mtu yeyote mwenye imani ya kweli ya YESU Kristo ni lazima atakuwa na kiwango Fulani cha dini ndani yake, kwamfano ukiwa mkristo ni lazima utajikuta  wewe mwenyewe unajijengea utaratibu wa kuomba kila siku, utajikuta unajijengea utaratibu wa kufunga mara kwa mara, licha tu ya biblia kuagiza lakini utajikuta unahudhuria ibada kanisani kila wakati, utajikuta unajijengea utaratibu wa kutoa sadaka na kuwasaidia na wengine n.k.…Na ndio maana biblia inasema..

Yakobo 1:26 “Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.

27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.”

Hivyo dini ya kweli ni ipi? Ni hiyo hapo juu kwenye mstari wa 27..Lakini sasa hiyo  haimpi tiketi ya moja kwa moja kwenda mbinguni , bali inamrahishia tu njia ya kwenda mbinguni..tofauti na Imani nyingine kwao kushika dini ndio kuokoka, lakini katika ukristo usipomwamini YESU KRISTO na kuoshwa dhambi zako katika damu yake hata kama unashika dini vipi mbinguni huwezi kwenda…

Unaweza ukawa unafunga lakini kama maisha yako yapo mbali na Kristo kuzimu utakwenda, unaweza ukawa unahudhuria ibada kila siku na kushika mambo yote unayoambiwa kanisani kwako kufanya lakini kama hauna Roho Mtakatifu ni bure…Tofauti na dini nyingine ambao kwao  dini ni kitu cha kujivunia..

Hivyo kwa ufupi Dini ni njema kama itakuwa imeambata na imani ya kweli ipasavyo, ni sawa na shule yenye maabara na walimu wazuri, inamjengea mwanafunzi mazingira mazuri ya kufaulu siku za mwisho lakini shule pekee haimfanyi mwanafunzi afaulu mitihani kama hatakuwa na bidii yake binafsi..

Baada ya kujua dini ni nini na dini ya ukweli ni ipi…Ni vizuri kujua Imani ya kweli ni ipi?..Imani ya kweli ni ile iliyopo katika kumwamini Yesu Kristo kama mwana wa Mungu na aliyetumwa kuja kuwaokoa wanadamu. Hiyo ndiyo imani ya kweli..Imani nyingine tofauti na hiyo ni imani ya uongo na unayopotosha na kupeleka watu mautini.

Hivyo huu Si wakati wa kijivunia dini tena…bali kujivunia wokovu katika Yesu Kristo…Hivyo kama hujaokoka na kuingia katika Imani ya kumwamini Yesu Kristo..Bado hujachelewa ingawa mlango wa Neema upo karibuni kufungwa hivyo mgeukie Kristo leo kwa kutubu dhambi zako zote na kuoshwa kwa damu yake, naye atakusamehe na kukurehemu.

Bwana akubariki sana.

Group la whatsapp Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp


Mada Nyinginezo:

KUNA TOFAUTI GANI KATI YA SALA NA DUA?

JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?

HADITHI ZA KIZEE.

AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA.

TABIA YA KIPEKEE USIYOIJUA KUHUSU NENO LA MUNGU.

SWALI LA KUJIULIZA!

NI NINI KINAKUPATA UNAPOIPUUZIA INJILI?

KWA VILE ALIVYOKUWA MTU WA HAKI.


Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/23/dini-ni-nini-na-imani-ya-kweli-ni-ipi/