Je! Hamna nyumba za kulia na KUNYWEA?.Mstari huu unahalalisha unywaji wa pombe?

by Admin | 26 February 2020 08:46 pm02

Je! mstari huu unahalalisha unywaji wa pombe?…(1Wakorintho 11:21 “kwa maana kila mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula; hata huyu ana njaa, na huyu AMELEWA.

22 Je! Hamna nyumba za kulia na KUNYWEA? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo.”)


JIBU: Watu wengi hususani wale wanaohalalisha ulevi katika makanisa yao ndio wanaoushikilia wakidhani kuwa Paulo alihalalisha ulevi kwamba waumini wakitaka kunywa mpaka walewe basi waende wakalewee majumbani kwao na sio kanisani.

Lakini Hebu tafakari huu mfano… “Watu wawili wamegombana katika nyumba ya Mungu (kanisani)…mpaka kufikia kupigana..Mhudumu wa kanisa akawakuta..na kwa hasira akawaambia “mmekosa sehemu za kupigania mpaka mnapigania kanisani”…Je! Kwa sentensi hiyo Mhudumu huyo atakuwa amehalalisha mapigano?…Jibu ni la! Hajayahalalisha hata kidogo…bali kwasababu anaiheshimu nyumba ya Mungu ikamlazimu yeye kusema vile. Kwamba nyumba ya Mungu sio ulingo wa mapambano..sio sehemu ya kufanyia dhambi wala mapambano…kama wameshindwa kuiheshimu nyumba ya Mungu na kutaka kuendelea kupigana basi wakapiganie sehemu nyingine huko lakini si nyumbani kwa Mungu.

Na hapa Mtume Paulo ndio anawaambia kwa ukali watu ambao wanaigeuza nyumba ya Mungu sehemu au vituo vya ulevi na ulafi. Watu ambao hawaiheshimu nyumba ya Mungu wala meza ya Bwana watu waovu, wana wa ibilisi. Hao ndio anaowaauliza je hawana nyumba za kunywea pombe zao?…maana yake wasiigeuze nyumba ya Mungu kuwa Bar… Kama tu Bwana alivyowafukuza wale watu hekaluni na kuwaambia wasiigeuze nyumba ya Baba yake kuwa pango la wanyang’anyi.

Picha kamili ya kinachoendelea katika kanisa la leo…watu wanakwenda kanisani ni walevi, wengine wanapafanya ni sehemu ya kunywea pombe kabisa rasmi bila aibu, wakitumia maandiko machache machache ya uongo waliyoyageuza kama walivyoligeuza hili…wengine  wanapageuza kanisani ni mahali pa kwenda kutafuta wachumba wa kufanya nao uasherati, wengine wanapageuza mahali pa kwenda kupata burudani za nyimbo na mahubiri ya kuwachekesha n.k..

Hivyo tunaonywa vikali kwamba tumheshimu Mungu..kanisani sio sehemu ya kwenda kujiuza..wala si sehemu ya kwenda kutafuta makahaba…Unapovaa vimini na suruali na kuingia navyo kanisani ni unakwenda kupageuza pale danguro (ni sawa na unakwenda kujiuza pale)..na hivyo ni kujitafutia laana badala ya Baraka..

Kama umeamua kuwa hivyo ulivyo huna mpango na Mungu basi upo huru kuishi maisha unayoyataka wewe na  unayoyachagua wewe..Toka kanisani nenda disko na nguo zako hizo, kule ni sehemu sahihi kwa mavazi hayo, nenda bar kule ni sehemu sahihi ya kulewa pombe lakini si katika nyumba ya Mungu. Nyumba ya Mungu ni nyumba takatifu ya sala, na ya kumwabudu Mungu, na ya Mungu muumba wa mbingu na nchi kwenda kukutana na sisi. Hivyo iheshimu.

Ubarikiwe. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

JE KUJIUA NI DHAMBI?

BUSTANI YA NEEMA.

DANIELI: Mlango wa 8

USIPOKUWA MWAMINIFU, NAFASI YAKO ITACHUKULIWA.

VICHEKESHO NA UTANI MADHABAHUNI

AMANI YA BWANA /AMANI YA MUNGU.

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/02/26/je-hamna-nyumba-za-kulia-na-kunywea-mstari-huu-unahalalisha-unywaji-wa-pombe/