BWANA MUNGU NASHANGAA KABISA lyrics

by Admin | 29 July 2020 08:46 pm07

BWANA MUNGU NASHANGAA KABİSA lyrics ~Swahili  (How Great Thou Art).


Toleo la kwanza kabisa la Wimbo huu liliandikwa na mtu mmoja raia wa Sweden, aliyeitwa Carl Boberg wimbo huu aliuandika mnamo mwaka 1885 baada ya kuvutiwa na mazingira aliyopishana nayo alipokuwa akitoka Kanisani yeye na marafiki zake. Anasema muda wa mchana walipokuwa njia hali ya hewa iliwabadilikia ghafla, wakaona wingu la tufani likitokea kwa mbali, na mara hiyo hiyo kukaanza kumulika mianga mingi kama ya radi angani, upepo mzuri ukaanza kuvuma juu ya mashamba yaliyokuwa pembeni, Na kisha manyunyu ya mvua matulivu  yakaanza kudondoka juu yao, na baada ya muda kidogo, wingu lile la tufani likapotea, muda huo huo ukatokea upinde mzuri wa mvua angani..

Na alipofika nyumbani na kufungua madirisha atazame nje, aliona ufukwe ya mji wake kama vile kioo, akatazama upande wa pili akasikia ndege wazuri wakitoa milio yao na kwa mbali kegele za kanisa zikilia, Hapo ndipo wimbo huu ulipomjia kichwani kuutunga na kuuandika.

****

Bwana Mungu nashangaa kabisa,

Nikifikiri jinsi ulivyo,

Nyota, ngurumo, vitu vyote pia,

Viumbavyo kwa uwezo wako.

Roho yangu na ikuimbie,

Jinsi wewe ulivyo mkuu,

Roho yangu na ikuimbie,

Jinsi wewe ulivyo mkuu.

Nikitembea pote duniani,

Ndege huimba nawasikia,

Milima hupendeza macho sana,

Upepo nao nafurahia.

Roho yangu na ikuimbie,

Jinsi wewe ulivyo mkuu,

Roho yangu na ikuimbie,

Jinsi wewe ulivyo mkuu.

Nikikumbuka vile wewe Mungu,

Ulivyompeleka mwanao,

Afe azichukue dhambi zetu,

Kuyatambua ni vigumu mno.

Roho yangu na ikuimbie,

Jinsi wewe ulivyo mkuu,

Roho yangu na ikuimbie,

Jinsi wewe ulivyo mkuu.

Yesu Mwokozi atakaporudi,

Kunichukua kwenda mbinguni,

Nitaimba sifa zako milele,

Wote wajue jinsi ulivyo.

Roho yangu na ikuimbie,

Jinsi wewe ulivyo mkuu,

Roho yangu na ikuimbie,

Jinsi wewe ulivyo mkuu.

*****

Tujiulize na sisi tunao utaratibu kwa kukaa chini na kuushangaa utukufu wa Mungu na kumtukuza?..Au kila kitu tunaona ni kawaida tu..Kumbuka Sifa kamili kama hizi mbele za Mungu ni bora kuliko dua na sala tunazompelekea kila siku.

Mungu anataka kuona, na sisi tukiufurahia uumbaji wake, kwa kumwimbia.

Ubarikiwe.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo ya biblia kwa  email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.

MWAMBA WENYE IMARA

CHA KUTUMAINI SINA lyrics

USITUPE LULU ZAKO MBELE YA NGURUWE.

KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/07/29/bwana-mungu-nashangaa-kabisa-lyrics/