by Admin | 17 August 2020 08:46 pm08
Historia ya wimbo wa tenzi – Ndio dhamana Yesu wangu. (Blessed assuarance)
Wimbo huu ulindikwa na mwanamke mmoja aliyeitwa Fanny Crosby, Mwanamke huyu japo aliishi kwa miaka 95 akiwa kipofu,lakini hakuacha kuitumia neema Mungu aliyompa kutangaza injili kwa njia ya Nyimbo zenye muundo wa Tenzi za rohoni na nyinginezo, katika maisha yake alifanikiwa kuandika nyimbo zaidi ya 8000, Na hii nyimbo “Ndio dhamana Yesu wangu” Ikiwa mojawapo, Nyingine inayojulikana sana mpaka leo ni “Usinipite mwokozi” yeye pia ndio aliyeiandika nyimbo hii alipokuwa amewatembelea wafungwa gerezani(angalia historia yake chini).
Sasa Siku moja alipokuwa amemtembelea rafiki yake nyumbani kwake aliyeitwa Phoebe Knapp, ambaye alikuwa ni mtunzi wa sauti za nyimbo, wakiwa nyumbani kwake Phoebe alianza kupiga mdundo wake aliokuwa ameutunga, kisha baada ya muda alimuuliza Fanny, Je unaweza kuniambia mdundo huu ni wa nyimbo gani?
Ndipo Fanny akamwambia “Ndio dhamana Yesu wangu”. Basi hapo ndio pakawa mwanzo wa mdundo na utunzi wa wimbo huo (1873).
Ndio dhamana Yesu wangu.
Ndiyo dhamana, Yesu wangu; |
Hunipa furaha za mbingu; |
Mrithi wa wokovu wake, |
Nimezawa kwa Roho wake. |
Habari njema, raha yangu, |
Yesu ndiye Mwokozi wangu, |
Habari njema, raha yangu, |
Yesu ndiye Mwokozi wangu. |
Kumsalimu moyo wangu, |
Mara namwona raha yangu; |
Aniletea malaika, |
Wananilinda, tutaokoka. |
Habari njema, raha yangu, |
Yesu ndiye Mwokozi wangu, |
Habari njema, raha yangu, |
Yesu ndiye Mwokozi wangu. |
Sina kinyume; nashukuru, |
Mchana kutwa huja kwangu; |
Usiku kucha kuna nuru; |
Mwokozi wangu; ndimi nuru. |
Habari njema, raha yangu, |
Yesu ndiye Mwokozi wangu, |
Habari njema, raha yangu, |
Yesu ndiye Mwokozi wangu. |
Hali na mali; anitwaa! |
Mara namwona anifaa, |
Nami nangonja kwa subira; |
Akiniita, nije mara. |
Habari njema, raha yangu, |
Yesu ndiye Mwokozi wangu, |
Habari njema, raha yangu, |
Yesu ndiye Mwokozi wangu. |
*****
Uimbapo wimbo huu kumbuka ni kipofu ndiye aliyeuandika, nawe pia unaposema “Ndio dhamana Yesu wangu” Basi awe kweli wokovu wako. Mpende yeye bila unafki na kumtumikia kwasababu ndiye aliyekufa kwa ajili yako.
Je! Umeokoka? Unajua kuwa Unyakuo upo karibu sana, kwasababu tunaishi katika kanisa la mwisho lijulikanalo kama Laodikia? Na kwamba hatutakuwa na kanisa lingine zaidi ya hili? Siku hizi zimekwisha, Hivyo kama upo tayari kumpa Yesu maisha yako leo ili wimbo huu uwe na maana kweli kwako. Basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>>KUONGOZWA SALA YA TOBA
Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
USINIPITE MWOKOZI Lyrics
YOTE NAMTOLEA YESU_Tenzi za Rohoni.
BWANA MUNGU NASHANGAA KABISA lyrics
CHA KUTUMAINI SINA lyrics
KUMTEGEMEA MWOKOZI Lyrics/Swahili.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
MPINGA-KRISTO
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
UFUNUO: Mlango wa 1
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/08/17/historia-ya-wimbo-wa-tenzi-ndio-dhamana-yesu-wangu/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.