JUKUMU LA MUHIMU LINALOKWEPWA NA WENGI.

by Admin | 26 August 2020 08:46 pm08

Jukumu moja na kuu tulilonalo sisi ni KUMJUA SANA YESU KRISTO. Wengi wanalikwepa jukumu hili. Na Zaidi wanapenda sana kutafuta kuwajua watumishi wa Yesu kuliko ya Yesu mwenyewe.

Waefeso 4:13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani NA KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo”.

Jitathmini ukiona kuna mahali unamjua mtumishi, zaidi ya Bwana wake mwenyewe ambaye ni Yesu, basi kuna tatizo mahali na pia una laana.(1Wakorintho 16:22)

Kama mtumishi wa Kristo akizungumziwa vibaya inakuuma Zaidi ya Yesu akifanyiwa mzaha, basi kuna tatizo katika uhusiano wako na Yesu.

Kama comedy za kumtania Mwokozi Yesu hazikuhuzunishi sana kama za kumtania  mchungaji wako, au mwalimu wako, basi kuna tatizo mahali.

Kama unakuwa mkali dini yako inapozungumziwa vibaya, au dhehebu lako au mwalimu wako anayekufundisha Neno la Mungu kanisani, na wakati huo huo unakutana na comedy inayomkebehi Kristo waziwazi na wala haikuhumizi  sana Zaidi inakuchekesha!, hebu jitafakari tena, inawezekana humjui kabisa Yesu, wala hayupo maishani mwako.

Kama Maisha yako ya binafsi ya siri, hujawahi kukaa ukazungumza  na mwokozi wala kumshukuru, basi kuna shida.

Dada/kaka usitumie nguvu nyingi kutafuta kumpendeza mtumishi, wala usiwe mshabiki wa dini, wala usiwe mshabiki wa mtumishi wa Mungu.

Tafuta kumjua Yesu, na kumjua Yesu sio kuhama na kubadilisha kanisa…Ni hapo hapo ulipo tu!..Unachopaswa kukifanya baada ya kumpokea Kristo ni kukinunua kitabu kinachoitwa Biblia. Usitegemee ile ya ku-download kwenye simu yako.. Ya kudownload ni nzuri baada ya kuwa na ya KITABU chenye kurasa za karatasi.

Hivyo kinunue hichi kitabu kinachoitwa Biblia. Ukishakipata! Anza kukisoma mwenyewe!..Mungu kakupa macho, kakupa na uwezo wa kusoma, hawezi kukunyima uwezo wa kuelewa!..

Kinachosababisha wengi wasiielewe biblia ni kusoma kwa kutimiza wajibu tu!..na sio kwa kutoka ndani ya mioyo yao, wanasoma tu kwasababu wameambiwa wasome, au kwasababu tu wanahisi ndio wanampendeza Mungu, na anasoma kwa mwezi mara moja…Hivyo biblia inakuwa ni kitabu kigumu sana kwao kukielewa. Na pia wanasoma mstari mmoja kisha wanarukia mwingine…Hawapendi kusoma mwanzo wa kitabu hadi mwisho.

Hivyo soma biblia mwenyewe kwa macho yako mawili. Ukikutana na jambo gumu kuna nguvu Fulani ya asili ambayo Mungu kaiweka ndani yetu itakayokupeleka katika kuutafuta ukweli Zaidi, hapo ndipo kitakuja kitu cha kutafuta msaada Zaidi kwa mahubiri ya watumishi wa Mungu, utaona kuna kitu kinakusukuma kwenda sehemu Fulani labda kanisa Fulani, au kwenye semina Fulani, au katika mahubiri Fulani.. ambapo utaona utapata majibu ya maswali yako, au utakwenda kusoma jumbe Fulani ambazo utaona zitakufaidisha roho  yako. Na kwa njia hiyo ndipo mafunuo ya Roho yanapokuja.

Lakini huwezi kusema naondoka kanisa hili nahamia lile kama hujapata sababu yoyote ya kimaandiko ya kufanya hivyo.. Wengi wanahama kanisa kwasababu tu wameambiwa ukweli..hivyo ule ukweli unawauma na kuishia kuhama, wengine kwasababu wamesikia wakisengenywa, wengine kwasababu wameona kanisani kumepungua watu hivyo na wao wanaondoka…mambo ambayo hayana mashiko kabisa!..Mtu wa namna hiyo hajaongozwa na Mungu, bali kafuata akili zake mwenyewe.

Lakini mtu wa kweli ambaye anaongozwa na Roho, huwa anaondoka sehemu moja hadi nyingine, ni kwasababu anatafuta uelewa wa maandiko Zaidi, anatamani kumjua Yesu zaidi na kukua kiroho.. huyo ndiye anayeongozwa na Roho. Anaona kuna umuhimu wa kutafuta kujifunza Neno Zaidi, kutafuta kufunga Zaidi na kusali. Na si kwasababu kasikia kasengenywa, au kasemwa, au kaudhiwa.

Hivyo siku zote usilisahau hili ndugu yangu mpendwa.. MJUE SANA YESU. Huyo ndio ndiye Mkuu wa Uzima, na ndiye mwenye funguo za Uzima,  na ndiye aliyekabidhiwa mamlaka yote ya mbinguni na Duniani..Tunavyozungumza sasa yupo anaishi! Na atarudi tena kulichukua kanisa lake, Ana nguvu nyingi sana, yeye hadhihakiwi sio yule unayemwona kwenye picha, sio unayemwona kwenye Tv, Yesu ni Mungu, akijifunua kwetu kikamilifu, hata hapa duniani tunaweza tusitamani kuendelea kuishi, Hivyo tumjue yeye kila siku, tujinyenyekeze mbele zake, ajifunue kwetu zaidi na zaidi. Anatamani kujifunua kwetu sana, ni sisi tu.

Bwana atubariki sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

JE UDHAIFU WANGU UNAWEZA KUZUIA INJILI?

Kuna haja gani ya kumwamini Yesu aliyezaliwa kama sisi?

WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.

WANA JUHUDI KWA AJILI YA MUNGU, LAKINI SI KATIKA MAARIFA.

MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.

RUDIA, TENA NA TENA KUMWOMBA MUNGU USIKATE TAMAA.

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/08/26/jukumu-la-muhimu-linalokwepwa-na-wengi/