Jabari ni nini, kama linavyotumika kwenye biblia?

by Admin | 13 September 2020 08:46 pm09

Jabari maana yake ni mtu hodari, asiyeogopa, shujaa.

Isaya 49:24 “Je! Aliye hodari aweza kunyang’anywa mateka yake, au jeshi lao waliofungwa halali wataokoka?

25 Naam, Bwana asema hivi, Hata jeshi la wafungwa wake aliye hodari watapokonywa mikononi mwake, na mateka yake aliye JABARI wataokoka; kwa maana nitateta na yeye atetaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu”.

Unaona, Jabari ni mtu shujaa lakini kibiblia kuna majabari wa aina mbili,

  1. Jabari katika kutenda maovu, na katika kutumainia mambo ya mwilini kama vile mali n.k.
  2. Na majabari katika kutenda mema na kuishindania imani, na kuvipiga vita vya kiroho.

 

Zaburi 52:1Kwa nini kujisifia uovu, EWE JABARI? Wema wa Mungu upo sikuzote.

2 Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila

3 Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli.

4 Umependa maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila.

5 Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung’oa katika nchi ya walio hai.

6 Nao wenye haki wataona; Wataingiwa na hofu na kumcheka; 7 Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa nguvu zake. ALIUTUMAINIA WINGI WA MALI ZAKE, NA KUJIFANYA HODARI KWA MADHARA YAKE.

8 Bali mimi ni kama mzeituni Umeao katika nyumba ya Mungu. Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.

9 Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako.

Waebrania 11:33 “ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba,

34 walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, WALIKUWA HODARI KATIKA VITA, walikimbiza majeshi ya wageni.

35 Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora;

36 wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani;

37 walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya;

38 (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi.

39 Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi;

40 kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi”.

 

Swali ni Je! Wewe ni Jabari katika nini?

Jibu unalo, lakini ikiwa upo katika ouvu, au mambo ya kidunia, basi Yesu anaweza kukufanya kuwa Jabari lake teule ikiwa tu leo utampokea..Ukipomkea  atakusamehe dhambi zako zote, atakufanya kuwa mwana wake,atakuondolea laana zote, atakupa Roho wake Mtakatifu bure, atakupa amani, na kikubwa zaidi atakupa na uzima wa milele .

Unasubiri Nini? Tangu ulipoanza kuitumikia dunia imekupa nini? Hivyo usikawie, ikiwa umedhamiria kwa moyo wako wote, kumkaribisha Yesu katika maisha yako, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Sasa Ikiwa ufuata maaelekezo hayo hapo juu, basi kuanzia sasa wewe ni JABARI la Bwana Yesu. Na utamwona atakavyoanza kutembea na wewe kukutengeneza..

Bwana akubariki.

1Wakorintho 16:13 “Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari”.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Biblia inamaanisha nini inaposema “Tusitweze unabii”?

Baradhuli/Mabaradhuli ni nini au ni nani kwenye biblia?

WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.

Areopago ni nini? Kwanini mtume Paulo walimpeleka huko?

NA YEYE ALIYEKETI JUU YA WINGU AKAUTUPA MUNDU WAKE JUU YA NCHI, NCHI IKAVUNWA.

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/09/13/jabari-ni-nini-kama-linavyotumika-kwenye-biblia/