Neno beramu lina maana gani katika biblia?

by Admin | 14 September 2020 08:46 pm09

Beramu ni nini?


Beramu ni jina lingine la neno BENDERA. Hivyo mahali popote kwenye biblia unapolisoma neno hili basi fahamu kuwa linamaanisha bendera.

Hesabu 1:52 “Na wana wa Israeli watazipanga hema zao, kila mtu katika marago yake mwenyewe, kila mtu hapo ilipo beramu yake mwenyewe, kama majeshi yao yalivyo”.,

Vipo vifungu vingi katika biblia, vinavyolitaja neno hili hatuwezi kuvihorodhesha hapa vyote, kwahiyo kama unahitaji kuvijua baadhi yao, basi soma kitabu cha Hesabu sura ile ya pili yote utakutana na Neno hili sehemu kadha wa kadha.

Lakini beramu/bendera sikuzote inasimama badala ya nini?

Tunafahamu kuwa kila bendera tunayoiona mahali fulani imesimamishwa, aidha kwenye mji, au chama, au jamii n.k. huwa  ina maana yake.

Nyingine zimebeba historia ya jamii husika/taifa, nyingine zimebeba tunu, nyingine zinaeleza tabia ya nchi, au vitu vya asili vya nchi n.k.

Hivyo hata rohoni napo, kila mmoja wetu kwa namna moja au nyingi ni lazima atakuwa ameshikilia bendera mojawapo inayomwakilisha yeye.

Na ndio maana leo hii ukienda kwenye mabalozi yote, ni lazima uone bendera ya nchi yake inayoiwakilisha imesimamishwa pale. Hiyo ni kukutambulisha kuwa umefika katika makao ya muda ya nchi ile.

Hivyo mambo yote yahusuyo nchi hiyo huko ugegenini utasaidiwa ukifika pale, huduma zote utapewa sawasawa tu na kama ungekuwa katika nchi yako.

Vivyo hivyo na hapa duniani, kila mmoja wetu ni balozi wa mahali Fulani. Na tunatambuliwa kwa beramu/bendera zetu rohoni.

Ikiwa wewe ni mwenye dhambi, moja kwa moja unapeperusha bendera ya kuzimu, kwa matendo yako maovu, ambayo asili yake ni kuzimu na mkuu wake ni ibilisi.

Lakini kama wewe ni mtakatifu, nawe pia ni lazima upeperushe bendera ya ufalme wa mbinguni kwa matendo yako, ambayo ni lazima yawe ya kumpendeza Mungu, na pili uwe unaihubiri injili(kuwashuhudia wengine habari njema).

Kama hayo mawili huyafanyiki ndani yako na unasema umeokoka, hakuna beramu/bendera yoyote unayoipeperusha ya ufalme wa mbinguni duniani.

Hivyo jitathimini maisha yako ni beramu gani unaipeperusha, katika hichi kipindi kifupi tuliobakiwa nacho hapa duniani. Je, ni ya mbinguni au kuzimu?

Lakini ikiwa leo hii unasema mimi na dhambi basi, nataka Yesu anibadilishe maisha yangu kuanzia leo , nataka anifanye kiumbe kipya nianze na mimi kuipeperusha beramu ya Yesu maishani mwangu. Basi uamuzi huo ni wa busara sana kwako, ambao utaufurahia maisha yako yote. Bwana anasema:

Na uzuri ni kuwa yeye mwenyewe anasema “yeye ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe” (Yohana 6:37)..

Hivyo kama upo tayari na umemaanisha  kufanya hivyo leo, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba.>>>KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

https://wingulamashahidi.org/ikabodi-maana-yake-ni-nini/

Jabari ni nini, kama linavyotumika kwenye biblia?

Neno Korbani linamaanisha nini? (Marko 7:11)

Mahuru ndio nini?

UNYAKUO.

Areopago ni nini? Kwanini mtume Paulo walimpeleka huko?

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/09/14/neno-beramu-lina-maana-gani-katika-biblia/