Pomboo ni nini katika biblia?(Kutoka 25:5, Ezekieli 16:10)

by Admin | 17 September 2020 08:46 pm09

Pomboo ni nini?


Pomboo ni aina ya samaki jamii ya nyangumi anayeishi baharini, Anajulikana kwa jina maarufu la DOLPHIN, Ni samaki anayezaa, pia ananyonyesha, lakini zaidi ya yote anasifa ya kuwa mnyama mwenye akili nyingi kuliko wote ulimwenguni baada ya mwanadamu. Na kuwa na tabia ya uokozi. Tazama picha juu.

Samaki huyu ni rahisi kufundishika, na ni rahisi kuishi na wanadamu.

Katika biblia pomboo(Dolphin) ametajwa sehemu nyingi, hususani katika matumizi ya ngozi yake, ambayo ilitumika katika kutekengeza hema ya kukutania, pamoja na vitu vingine vitengenezwayo kwa ngozi, kama vile viatu vya thamani.

Hivi ni baadhi ya vifungu katika biblia vinavyomtaja Pomboo.

Kutoka 25:3 “Sadaka utakayopokea mikononi mwao ni hii; dhahabu, na fedha, na shaba,

4 na nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na nguo za kitani safi, na singa za mbuzi;

5 na ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na NGOZI ZA POMBOO, na miti ya mshita,

6 na mafuta ya ile taa, na viungo vya manukato kwa yale mafuta ya kupaka, na kwa ule uvumba wenye harufu nzuri”;

 

Kutoka 26:14 “Nawe fanya kifuniko cha ile hema, cha ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake KIFUNIKO CHA NGOZI ZA POMBOO.

15 Nawe fanya hizo mbao za maskani za mti wa mshita, zenye kusimama”.

 

Kutoka 35:5 “Katwaeni kati yenu matoleo kwa Bwana; mtu awaye yote aliye na moyo wa kupenda, ayalete matoleo; dhahabu na fedha na shaba;

6 na nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na kitani nzuri, na singa za mbuzi;

7 na ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na NGOZI ZA POMBOO, na mbao za mshita”;

 

Ezekieli 16:9 “Kisha nikakuosha kwa maji; naam, nalikuosha kabisa damu yako, nikakupaka mafuta;

10 nikakuvika nguo ya taraza, nikakupa VIATU VYA NGOZI YA POMBOO, nikakufunga nguo ya kitani safi kiunoni mwako, nikakufunika kwa Hariri”.

Mistari mingine ni kama hii;

(Kutoka 35:23, 36:19, 39:34, Hesabu 4:6,8,10,11,12,)

Ni kwanini Mungu aliruhusu hema ya kukutania ifunikwe na ngozi ya samaki hodari (pomboo)?

Kumbuka, wana wa Israeli, waliwashinda maadui zao kabisa kabisa, kwa njia ya habari tu,.pale walipojaribu kuvuka kama wao waligharikishwa,.Hivyo ni kama samaki hodari Mungu aliwavusha baharini pasipo wao kuzama..

Hiyo ni kuwakumbuksha kuwa kila watakapokusanyika mbele ya Hema, na kuitazama hiyo hema iliyofunikwa kwa ngozi ya pomboo, wakumbuke wema wa Mungu aliowafanyia wakati wanaivuka bahari ambayo kwa namna ya kawaida haiwezekani mwanadamu yeyote kuivuka isipokuwa samaki tu peke yake..

Hivyo wamtukuze yeye, na kumpa shukrani zote peke yake.

Bwana akubariki.

Tazama maana maneno mengine ya biblia chini;

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Yeshuruni ni nani katika biblia?

Kitabu cha YASHARI kinachozungumziwa katika 2Samweli 1:17-18, ni kitabu gani?

Areopago ni nini? Kwanini mtume Paulo walimpeleka huko?

Kamsa ni nini kwenye biblia? (Sefania 1:16, Wimbo 3:8)

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

MPINGA-KRISTO

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/09/17/pomboo-ni-nini-katika-bibliakutoka-255-ezekieli-1610/