USINIE MAKUU.

by Admin | 12 November 2020 08:46 pm11

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, Karibu tujifunze biblia.

Neno la Mungu linasema katika..

Warumi 12:3 “Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu ASINIE MAKUU KUPITA ILIVYOMPASA KUNIA; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha Imani”.

Sasa kunia makuu kunakozungumziwa hapo ni kupi?

Tukiendelea mbele kidogo katika mistari hiyo inayofuata tutapata jibu kamili…

“4 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja;

5 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.

6 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;

7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;

8 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.”

Umeona?. Maana yake ni kwamba…Usiwaze moyoni mwako, na kujiona kuwa… “unaweza kuwa na karama zote au nyingi”.

Kwamfano mtu mmoja, atataka yeye ndio awe mchungaji, yeye ndio awe Nabii, yeye ndio mwalimu, yeye ndio Mtume, yeye ndio Muinjilisti n.k… Kwaufupi karama zote za rohoni yeye ni zake. Anajiona yeye hawezi kuwa na karama moja tu”..yeye hawezi kuwa mwinjilisti tu peke yake ni lazima atakuwa ni Nabii pia..hawezi kuwa Mwalimu peke yake ni lazima atakuwa Mwalimu na Nabii mkuu, hawezi kuwa Mtume tu peke yake, ni lazima atakuwa ni Mtume na Nabii mkuu.. N.k Sasa hiyo ni mifano tu, ambayo ndio biblia inatuonya kwamba Tusinie Makuu kuliko tunavyopaswa kunia.

Roho ya kunia Makuu, inaua roho ya unyenyekevu ndani ya mtu, na hatimaye kuundoa kabisa uwepo wa Mungu ndani ya mtu.

1Petro 5: 5 “…Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema”

Na karama tulizopewa sio za mashindano wala za kujionyesha yupi bora Zaidi, au yupi mwenye neema kubwa zaidi. Karama yeyote inayotumika kwa matumizi hayo, tayari imeshavamiwa na shetani. Karama tulizopewa ni za kuhudumiana ili kuwakamilisha watakatifu na kazi ya huduma itendeke ili mwili wa Kristo ujengwe. na sio kuringishiana wala kuzitumia hizo kujinyanyua juu ya wengine.

Waefeso 4:11 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;

12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe”;

Bwana atusaidie.

Kama bado hujampokea Kristo, mlango wa Neema upo wazi sasa, ila hautakuwa hivyo siku zote. Hivyo geuka leo, na kumkabidhi Maisha yako, kwasababu muda tuliobakiwa nao hapa duniani sio mwingi, wakati wowote parapanda ya mwisho inalia na Kristo atalinyakua kanisa lake, kitakachosalia huku duniani ni hukumu. Hivyo mimi na wewe tusiwe miongoni mwa watakaoangukia kwenye hukumu ya Mungu.

Kumbuka kuzimu ipo na mbingu vile vile ipo. Na Uzima au Mauti, tunachagua tukiwa hapa hapa duniani, baada ya kifo hakuna nafasi ya kufanya uchaguzi. Hivyo fanya uamuzi uliobora sasa kabla siku zako za kuishi hapa duniani hazijaisha.

Maran atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

NITAIFAHAMU VIPI KARAMA YANGU?.

KARAMA YA MUNGU NI UZIMA WA MILELE.

NJONI, NUNUENI MLE NA MNYWE.

BONDE LA KUKATA MANENO.

Kati ya Unyakuo,dhiki kuu, utawala wa miaka 1000 kipi kinaanza

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/11/12/usinie-makuu/