Wevi na wanyanga’anyi waliomtangulia Yesu walikuwa ni wapi?

by Admin | 13 November 2020 08:46 pm11

SWALI: Bwana Yesu asifiwe mtumishi habari ya uzima, samahani nini swali;  Yohana 10:7-8 inasema;

“7 Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo.

8 Wote walionitangulia ni wevi na wanyang’anyi; lakini kondoo hawakuwasikia”.

Hapo sijaelewa Bwana alichokimaanisha aliposema wote waliomtangulia walikuwa ni wevi na wanyang’anyi?


JIBU: Mstari huo hauzungumzii, wale waliomtangulia Bwana yaani Manabii na makuhani  wa agano la kale hapana, kwani wao ndio waliokuwa wanamwandalia njia yeye, aliye mlango wa kondoo wenyewe.

Bali mstari huo ulikuwa unawazungumzia watu waliokuwa wanajifanya kuwa wao ndio masihi ( yaani Mwokozi) kama yeye. Hao ndio alikuwa anawasemea hapo, kwamba ni wevi na wanyang’anyi na kwamba kondoo wa kweli wa Mungu hawakuwafuata.

Kumbuka wana wa Israeli kwa muda mrefu walikuwa wanangojea masihi ambaye atawaokoa katika shida zao, na dhambi zao kama ilivyotabiriwa katika torati. Hivyo ilikuwa ni jambo la kawaida kutangulia ma-kristo wa uongo wengi kabla yake wakijifanya wao ndio. Utalithibitisha hilo katika maneno ya Yule Gamalieli, mwalimu wa torati, pale alipokuwa anahojiana na wakuu wa makuhani juu ya mitume walichokuwa wanakifanya kwa habari ya Yesu..Alisema;

Matendo 5:35 “akawaambia, Enyi waume wa Israeli, jihadharini jinsi mtakavyowatenda watu hawa.

36 Kwa sababu kabla ya siku hizi aliondoka Theuda, akijidai ya kuwa yeye ni mtu mkuu, watu wapata mia nne wakashikamana naye; naye aliuawa na wote waliomsadiki wakatawanyika wakawa si kitu.

37 Baada ya mtu huyo aliondoka Yuda Mgalilaya, siku zile za kuandikiwa orodha, akawavuta watu kadha wa kadha nyuma yake, naye pia akapotea na wote waliomsadiki wakatawanyika.

38 Basi sasa nawaambia, Jiepusheni na watu hawa, waacheni; kwa kuwa shauri hili au kazi hii ikiwa imetoka kwa binadamu, itavunjwa,

39 lakini ikiwa imetoka kwa Mungu hamwezi kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu”.

Unaona, hapo anasema alitangulia, Theuda, na Yuda Mgalilaya, na walikuwepo na wengine wengi  pia biblia haijawazungumzia tu. Kwahiyo  wezi na wanyang’anyi Yesu aliokuwa anawazungumzia hapo ndio hawa.

Hata sasa wevi  na wanyang’anyi Bwana Yesu aliwatabiri watakuwepo katika siku za mwisho. Ndio wale aliowaita Makristo wa uongo na manabii wa uongo.

Mathayo 24:24 “Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule”.

Hivyo Kristo ameshatuonya, ni wajibu wetu kuwa macho, na hiyo inakuja kwa kuwa wakristo kweli kweli na kumruhusu Roho Mtakatifu kutenda kazi ndani yetu.

Swali ni Je! Umeokoka? Na Kama umeokoka Je! Umesimama? Kumbuka, makristo hawa watajaribu kuwadanganya yamkini hata wateule, hiyo ni kuonyesha kuwa ni jinsi gani ilivyo ngumu kuwatambua kama wewe utakuwa ni mkristo jina tu, au mkristo vuguvugu. Hizi si nyakati tena za kukaa gizani.

Ni heri ukaanza maisha yako upya na Kristo leo. Ikiwa bado hujaokoka, na unataka leo kumpa Yesu maisha yako, basi uamuzi huo utakuwa ni wa busara sana kwako. Kama jibu ni ndio .Fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya toba na kupokea maagizo mengine ya rohoni>>>>  SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

USIIGEUZE NYUMBA YA MUNGU KUWA PANGO LA WANYANG’ANYI.

UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?

WALIOITWA NI WENGI, ILA WATEULE NI WACHACHE.

FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.

MTETEZI WAKO NI NANI?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/11/13/wevi-na-wanyangaanyi-waliomtangulia-yesu-walikuwa-ni-nani/