Nyinyoro ni nini?

by Admin | 9 December 2020 08:46 pm12

Tusome..

Wimbo 2:1 “Mimi ni ua la uwandani, Ni nyinyoro ya mabondeni. ”

Hapo kuna vitu viwili, 1) Ua la uwandani, na 2) Nyinyoro ya mabondeni.

Sasa kwa urefu juu ya Ua hili la uwandani unaweza kufungua hapa  ili tuende pamoja >> Ua la Uwandani

Lakini tutaiangalia sehemu ya pili inayozungumiza Nyinyoro ya mabondeni...

Sasa Nyinyoro ni jamii ya maua ijulikanayo kama “Lil” kwa lugha ya kiingereza.. (Tazama picha juu). Ua la uwandani au kwa lugha nyingine “Ua la Sharon, lenyewe linaota sehemu tambarare”. Lakini jamii ya haya maua ya Nyinyoro (au Lily) yanasitawi sehemu za mabonde na miteremko. Ni maua mazuri sana kwa mwonekano kama hayo ya maua mengine ya Sharon.

Sasa hilo ua ni nani?

Si mwingine zaidi ya Mwokozi wa Ulimwengu, yeye ndiye Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho…Yeye ndiye Ua la Sharon linalostawi sehemu tambarare na ndiye Ua la Nyinyoro linalostawi mabondeni, ndio Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho..

Kama vile maua yavutiavyo na yatoavyo harufu nzuri, ndivyo Yesu alivyo mzuri naye, hakuna aliyemtumainia akajuta, wala kumkinai, amejaa Mema, na raha. Wana raha na heri wote wanaomkimbilia. Je wewe ni mmoja wao?

Kama bado hujampokea basi umekosa kitu cha muhimu sana katika maisha yako, hivyo fanya hima leo, mpokee na utapata raha nafsini mwako..

Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha”.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

Sharoni ni nini au ni wapi kibiblia?(1Nyakati 5:16)

Areopago ni nini? Kwanini mtume Paulo walimpeleka huko?

Bwana Yesu alimaanisha nini kusema “Saa yangu haijawadia?”

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/12/09/nyinyoro-ni-nini/