Tofauti kati ya ufalme wa mbinguni na ufalme wa Mungu ni ipi?

by Devis Julius | 23 May 2021 08:46 pm05

JIBU: Watu wengi wanajaribu kutoa  tofauti katika  maneno hayo mawili, lakini ukweli ni kwamba yanamaanisha jambo lile lile moja, ufalme wa mbinguni ndio ufalme wa Mungu.

Na ndio maana kuna mahali Bwana Yesu  alisema maneno haya kwa wanafunzi wake;

Mathayo 19:23 “Yesu akawaambia wanafunzi wake, Amin, nawaambieni, ya kwamba itakuwa shida tajiri kuingia katika UFALME WA MBINGUNI.

24 Nawaambia tena, Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano, kuliko tajiri kuingia katika UFALME WA MUNGU”.

Ukichunguza hapo utaona Bwana Yesu alikuwa anamaanisha kitu kimoja katika hayo maneno mawili, ufalme wa Mungu na ule wa mbinguni..Hivyo unapokutana na mwandishi mmoja anatumia sana neno ufalme wa mbinguni, na mwingine ufalme wa Mungu, usichanganyikiwe ujue wanamaanisha kitu kilekile kimoja.

Ni sawa na ule mfano wa “kuapa” ambao Bwana Yesu aliwaambia mafarisayo, wao walidhani kama ukiapa kwa mbingu sio kosa, bali ukiapa kwa yeye akatiye juu ya kiti cha enzi mbinguni ndio kosa…Wakijaribu kutofautisha kati ya Makao ya Mungu na Mungu mwenyewe.. Lakini Yesu aliwaita viongozi vipofu kwasababu  hawakujua kuwa ukishaitaja mbingu, tayari moja kwa moja umeshamtaja na Yule akaaye ndani yake .  Soma..

Mathayo 23:16 “Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao, Mtu atakayeapa kwa hekalu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa dhahabu ya hekalu, amejifunga.

17 Wapumbavu ninyi na vipofu; maana ni ipi iliyo kubwa, ile dhahabu, au lile hekalu liitakasalo dhahabu?

18 Tena, Mtu atakayeapa kwa madhabahu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga.

19 Vipofu ninyi; maana ni ipi iliyo kubwa, ile sadaka, au ile madhabahu iitakasayo sadaka?

20 Basi yeye aapaye kwa madhabahu, huapa kwa hiyo, na kwa vitu vyote vilivyo juu yake.

21 Naye aapaye kwa hekalu, huapa kwa hilo, na kwa yeye akaaye ndani yake.

22 Naye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kwa yeye aketiye juu yake”.

Vivyo hivyo unaposema Ufalme wa Mbinguni, unapaswa ufahamu kuwa unautaja Ufalme wa Mungu mwenyewe anayeishi huko. Jambo ni lile lile hakuna tofauti yoyote.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengi

Mada Nyinginezo:

ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.

DANIELI: Mlango wa 11

LISHIKILIE SANA LILE AGIZO LA KWANZA.

ITAKUFAIDIA NINI?

UFUNUO: Mlango wa 11

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2021/05/23/tofauti-kati-ya-ufalme-wa-mbinguni-na-ufalme-wa-mungu-ni-ipi/