Katika biblia Madhehebu ya Wanazorayo yalikuwaje? (Matendo 24:5)

by Admin | 10 September 2021 08:46 pm09

Tusome

Matendo 24:5 “Kwa maana tumemwona mtu huyu mkorofi, mwanzilishi wa fitina katika Wayahudi wote duniani, tena ni kichwa cha madhehebu ya Wanazorayo”.

Katika biblia kipindi ambacho Bwana Yesu yupo ulimwenguni, yalikuwepo madhehebu makuu mawili katikati ya wayahudi ambayo ni Mafarisayo na Masadukayo.

Matendo 5:17 “Akaondoka Kuhani Mkuu na wote waliokuwa pamoja naye, (hao ndio walio wa madhehebu ya Masadukayo), wamejaa wivu,”

Tusome pia..

Matendo 15:5 “Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika torati ya Musa”.

Hayo ndiyo madhehebu mawili makuu, na yote yalikuwa yanaamini katika torati ya Musa, tofauti ilikuwa ni katika kuamini kiama..Mafarisayo waliamini kuna ufufuo lakini Masadukayo walikuwa hawaamini hayo.

Lakini baada ya Bwana kuondoka lilizaliwa dhehebu lingine ambalo nalo liliamini katika torati ya Musa, lakini lilienda mbele zaidi kuamini kuwa Yesu aliyetokea Nazareti ndiye Masihi.

Hivyo dhehebu hilo likaitwa dhehebu la Wanazorayo…kufuatia mji wa Nazareti ambao Bwana alilelewa…na yeyote aliyeishi Nazareti aliitwa mnazorayo..

Mathayo 2:23 “akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazorayo.”

Lakini je! madhehebu hayo yote, yalifanikiwa kumjua Kristo? 

Ukweli ni kwamba mitume wa Bwana Yesu, hawakuwa wafuasi wa madhehebu yoyote ya kidini yaliyokuwa wakati ule. Wala siku ile ya Pentekoste Roho Mtakatifu hakutua, katika mojawapo ya madhehebu hayo.

Bali alitua juu ya watu waliokuwa wamefanyika wanafunzi wa Bwana Yesu, sio kwa dini bali kwa kusikia na kuyatenda yote aliyoyafundisha. Hata sasa ndivyo Roho Mtakatifu anavyofanya juu ya watu.

Hatui kwenye madhehebu ya kidini, bali kwa watu waliomtii Kristo kwa kutubu dhambi zao.

Je umempokea Yesu maishani mwako na kujazwa Roho Mtakatifu?..kama bado hujampokea ni heri ukafanya hivyo sasa maana muda uliobakia ni mchache sana.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.

Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

KWANINI NI YESU KRISTO WA NAZARETI?

NGUVU YA MNADHIRI WA BWANA.

Kwanini wakristo walipomuona Petro akigonga walisema “Ni malaika wake”?

JE CHANJO YA KORONA NI ALAMA YA MNYAMA?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2021/09/10/madhehebu-ya-wanazorayo/