NA ABARIKIWE KILA AKUBARIKIYE, NA ALAANIWE KILA AKULAANIYE.

by Admin | 23 November 2021 08:46 pm11

SWALI: Nini maana “nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani;”..Je! Ni kwa namna gani tunapaswa tulibariki taifa la Israeli.  Je! Ili tubarikiwe tunapaswa, tufunge na kuliombea Taifa la Israeli usiku na mchana, au tuwe na bendera za taifa lile makanisani kwetu au majumbani mwetu?.

Ni kwa namna gani tutapokea Baraka kwa kulibariki tu taifa hilo?


JIBU: Maneno hayo, kwa mara ya kwanza tunaona Mungu akiyatamka kwa Ibrahimu katika;

Mwanzo 12:1 “Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;

2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;

3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa”.

Maandiko hayo hayatupi tafsiri ya kwamba tukeshe kuliombea taifa la Israeli usiku na mchana ili tubarikiwe, hapana utaona maneno hayo, Mungu alisema akilenga wakati ambapo watu wanapanga kuliangusha, au kuliporomosha au kuliletea vitisho taifa hilo, aidha kwa kulivamia, au kuliloga, n.k. kwa namna yoyote ile, hapo ndipo anayejaribu kufanya hivyo anakumbushwa,kuwa aibarikiye Israeli, atabarikiwa, na ailaaniye Israeli atalaaniwa.

Jambo kama hilo tunalithibitisha kwa Yule Balaamu mchawi, ambaye aliajiriwa na Balaki, ili aende kuwalaani Israeli, (yaani kuwaloga) kwa ushirikina ili wasifanikiwe kuvuka katika nchi ya Balaki. Lakini Ilikuwa nusura Mungu amuue Yule Balaamu, kwa kitendo tu hicho cha kujaribu kuliloga taifa teule. Kinyume chake ikabidi alibariki ili tu awe salama..Mpaka yeye mwenyewe akakiri,na kusema hapana uchawi katika Israeli wala uganga..

Hesabu 23:21 “Hakutazama uovu katika Yakobo, Wala hakuona ukaidi katika Israeli. Bwana, Mungu wake, yu pamoja naye, Na sauti kuu ya mfalme i katikati yao.

22 Mungu amewaleta kutoka Misri, Naye ana nguvu kama nguvu za nyati”.

Hiyo ni kuonyesha kuwa, hata sasa yapo mataifa mengi ambayo yameshatangaza uadui na Israeli, mojawapo ni Somalia, na Libya, embu yaangalie mataifa hayo leo hii yapoje., na hiyo yote ni kwasababu yamejaribu kuleta vita na vitisho kwa taifa teule la Mungu, na matokeo yake ni kuwa yamepigwa, kila kukicha ni vita. Na mengine yanalitamkia maneno ya laana kama vile Palestina,, na mengine kuliwekea vikwazo.  Embu Yatazame ustawi wao hayo mataifa au hao watu leo hii walivyo.

Halikadhalika, taifa ambalo halitaki shari na Israeli, bali linalitakia mema amani na mafanikio daima, basi taifa hilo au Mtu huyo Mungu  atambariki. Hivyo  umeona hapo, inalenga katika habari ya amani na shari, yaani pale ambapo unalazimishwa utamke mabaya, uwalaani, uwatukane,  au upigane vita kinyume chao, hapo unapaswa uende kinyume chake, uwabariki, na kuwatakia amani. Ndipo utakapobarikiwa.

Lakini sio kuacha kufuata kanuni za Mungu za kimaandiko na kukesha kuliombea taifa la Israeli ili tubarikiwe. Mpaka tunasafiri kwenda kule Yerusalemu, kupokea Baraka hizo, Mungu havutiwi sana na sisi tunapofanya hivyo, anavutiwa na sisi pale tunapoishi kulingana na Neno lake, hivyo tu. Kwahiyo, usipeleke fikra zako sana Israeli, bali zipeleke kwenye maisha yako, vilevile maombi yako, yaelekeze kwa watu wenye dhambi leo hii ulimwenguni. Kesha kuwaombea hao, na kuiombea Injili.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp  yanayotumwa kila siku basi fungua bofya hapa ujiunge >>> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

ALAMA ZA BENDERA YA ISRAELI ZINAWAKILISHA NINI?

Israeli ipo bara gani?

Mataifa ni nini katika Biblia?

Bwana Yesu alimaanisha nini kusema “yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari?”

REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.

Je Mkristo kutembea na walinzi (Bodyguards),ni sawa?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2021/11/23/na-abarikiwe-kila-akubarikiye-na-alaaniwe-kila-akulaaniye/